Tatizo la wanawake kutoshika ujauzito

Nina rafiki yangu ambaye ana mwaka wa nne katika ndoa yao ana tatizo la kutoshika mimba. Wameshaenda hospitali nne tofauti na mumewe kuchekiwa na wameambiwa wote wawili hawana tatizo lolote. Nilipomuuliza je huwa wanafanya kwenye zile siku hatari alijibu ndio huwa wanafanya kwani kila mmojawao ana hamu na mtoto kwa muda huu na hajawahi kutoa mimba maishani mwake.

Tatizo kubwa linamsumbua huyu dada ni kuwa wanataka mtoto, pia mumewe na ameshamuambia mwaka huu ukiisha kama hajapata mimba ni lazima atatafuta mtoto nje ya ndoa ili aitwe baba.

Jamani naomba mumsaidie huyu rafiki yangu kwani hajui tatizo ni nini hadi hashiki mimba, yupo radhi hata kutumia tiba mbadala/ dawa ya asili itakayomsaidia kuweza kushika mimba haraka. Nakaribisha mawazo, ushauri n.k
 
Kutoshika mimba kuna sababu nyingi ajaribu kutumia vyakula food suppliments kama grape vine, zinc, antilipemic tea, vega power na 7 forces zingatia kuwa hizi ni food suppliment sio dawa akitumia atapata matokeo ya kushangaza
 
Kuto shika mimba kuna sababu nyingi ajaribu kutumia vyakula food suppliments kama grape vine, zinc, antilipemic tea, vega power na 7 forces zingatia kuwa hizi ni food suppliment sio dawa akitumia atapata matokeo ya kushangaza
Nashukuru sana ila zinapatikana wapi hizo food suppliments?:A S-coffee:
 
kuto shika mimba kuna sababu nyingi ajaribu kutumia vyakula food suppliments kama grape vine, zinc, antilipemic tea, vega power na 7 forces zingatia kuwa hizi ni food suppliment sio dawa akitumia atapata matokeo ya kushangaza
Ahsante mkuu!
 
Kutoshika mimba kuna sababu nyingi ajaribu kutumia vyakula food suppliments kama grape vine, zinc, antilipemic tea, vega power na 7 forces zingatia kuwa hizi ni food suppliment sio dawa akitumia atapata matokeo ya kushangaza
Pia kuna ADVANCED PRENATAL MULTIVITAMIN SUPPLEMENT na TRI-IRON FOLIC. Mke wangu alikuwa na tatizo ilo kwa mwaka mmoja GY wake akamwambia atumie hivyo vidonge, baada ya wiki sita tu akaconceive
Jaribu kutafuta kwenye maduka ya GNLD au baadhi ya pharmacy
 
Pia kuna ADVANCED PRENATAL MULTIVITAMIN SUPPLEMENT na TRI-IRON FOLIC. Mke wangu alikuwa na tatizo ilo kwa mwaka mmoja GY wake akamwambia atumie hivyo vidonge, baada ya wiki sita tu akaconceive.
Jaribu kutafuta kwenye maduka ya GNLD au baadhi ya pharmacy

Thank you so much.
 
Mhh. Interestin, sos, same problem here, sema tu sisi hatujafika huko kwa kutafuta watoto wanje. Help please.
 
Kama pesa ipo asipoteze muda aende India atapata ufumbuzi kamili na kwa uwezo wa Mungu kabla mwisho wa mwaka atakuwa na mtoto au kama imedelay atakuwa mja mzito.
 
Nina rafiki yangu ambaye ana mwaka wa nne katika ndoa yao ana tatizo la kutoshika mimba. Wameshaenda hospitali nne tofauti na mumewe kuchekiwa na wameambiwa wote wawili hawana tatizo lolote. Nilipomuuliza je huwa wanafanya kwenye zile siku hatari alijibu ndio huwa wanafanya kwani kila mmojawao ana hamu na mtoto kwa muda huu na hajawahi kutoa mimba maishani mwake.

Tatizo kubwa linamsumbua huyu dada ni kuwa wanataka mtoto, pia mumewe na ameshamuambia mwaka huu ukiisha kama hajapata mimba ni lazima atatafuta mtoto nje ya ndoa ili aitwe baba.

Jamani naomba mumsaidie huyu rafiki yangu kwani hajui tatizo ni nini hadi hashiki mimba, yupo radhi hata kutumia tiba mbadala/ dawa ya asili itakayomsaidia kuweza kushika mimba haraka. Nakaribisha mawazo, ushauri,..... n.k

Nilipoweka red font, nataka kusisitiza kuwa hao wanandoa wana tatizo (Pengine daktari na vipimo vilivyofanywa havijaweza kulibaini). sijui wamefanya vipimo gani lakini vipimo basic kwa mwanamke ni Ultrasound scan (Kubaini abnormality katika via vya uzazi kama uvimbe, nk) na Hysterosalpingogram (Kubaini kama mirija -fallopian tubes zimeziba) Vipo vipimo vingine zaidi pia. Muhimu ni kujua je mwanamke ana mirija inayoweza kupitisha yai la uzazi , je mji wa mimba (Uterus) mazingira yake yanaruhusu/inauwezo wa kuruhusu kuungana kwa mbegu za kiume na kike nk
Kwa mwanaume kipimo cha msingi ni Sperm analysis (kutambua kama mwanume ana shahawa za kutosha, zenye "ubora" unaotakiwa kutunga mimba).

Kama wamefanya haya yote, na wakaoneka wako safi; je mwanamke mzunguko wake wa hedhi unaambatana na kushuka kwa yai (Ovulation) au anapata Anovulatory cycles? Gynaecologist wanajua namna ya ku-asses hali hii. nakushauri rejea mpitie vipimo walivyofanya kabla ya kutamka hawana tatizo.

Kauli ya jamaa kuwa anampa Ultimatum ni ya kushangaza na kutia mashaka sana. Madaktari waliomo JF wanaweza kutoa ushuhuda juu ya wanaume ambao huenda kwa madaktari kutaka "favour" ya majibo kuwa wao wako safi . Ni ukweli kuwa wanume mara zote huogopa sana kuwa wao ndio "wagumba" katika ndoa. Mara nyingi Huwa hawatoi hizo Ultimatum instead huchepuka tu nje ya ndoa na kwenda "kuprove" kuwa mwenye matatizo ni mwanamke. (I'm sorry for this last part , it wasn't neccessary but I am disgusted by that man's statement. Is he also ready to let his wife go get pregnant with another man?)
 
Niko na mme wangu it's about 3 years now toka tuishi pamoja. Kila tukikutana na kushiriki on danger days naishia kubleed damu nyingi sana na maumivu makali. Tulienda hospitali tukapima zinaa zote bila mafanikio, but nkikaribia kubleed nahisi dalili zoote za ujauzito then tunaishia uzuni kwa kubleed damu rundo. One doctor alibaini mbegu za mme wangu kutokua na nguvu za kutosha kutungisha akatupa ushauri na vyakula vya kutumia but tatizo liko palepale.

Juzi dokta mwingine kasema nina shida mimi kwenye mfuko wa uzazi, akanipa dawa nkatumia na ziliisha last week.

Please madaktari, hebu tupeni ushauri ili Mungu atufungulie tupate mtoto. G'time

Poleni kwa mgomo unaogusa maisha yenu.

Asitokee mtu kuwalaumu kana kwamba hatumjui adui ni nani.
 
Please majibu kwa asie na nia thabiti ya kujibu na mwenye kutaka kukebehi yataishia kutuua moyo na kutuongezea simanzi
 
Please majibu kwa asie na nia thabiti ya kujibu na mwenye kutaka kukebehi yataishia kutuua moyo na kutuongezea simanzi

Kweli mama utapata majibu stahiki na watakaokukejeli washindwe.Ubarikiwe
 
You should see a gynecologist. Maana hata kama mbegu za mumeo hazina nguvu wewe unaonekana una tatizo zaidi kwasababu wewe ndie unaeumia na kutoka damu kupitiliza.

Tena ningekushauri ukishaonana na wa kwanza ukapata kujua kinachokusumbua, tafuta mwingine upate second opinion just to make sure tatizo utakaloambiwa unalo ndilo. Usije ukaishia kupata dozi baada ya dozi bila mabadiliko/mafanikio yoyote.

Kila la kheri na poleni sana.
 
Back
Top Bottom