Tatizo la kutoa hewa chafu (kujamba kupita kiasi)- Elewa chanzo, pata ushauri na tiba zake

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
90
1608118516654.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Wadau wangu naamini hamjambo kabisa.

Nikiwa kazini, nyumbani au hata nikikaa na wenzangu najisikia vibaya kwani huwa najamba sana na mjambo wenyewe ni ule wenye sauti.

Nifanye nini kuepuka hali hii?
---
Habari zenu ndugu zangu.

Ebana toka juzi sijielewi elewi, najikuta najamba sana, sijisikii kuumwa chochote bali najamba sana tu.

Nimeshindwa kung'amua tatizo linalonisibu coz najamba tu bila sababu, yani nikiwa peke yangu naachia mabomu hayo mpaka najiogopa.

Tatizo linaweza likawa ni nini ndugu zangu?

UFAFANUZI WA TATIZO HILI KUTOKA KWA WATAALAMU
Je, ni salama Kujamba? au inategemea na Harufu?
Wengi wetu lazima tumeshapitia hali ya kujamba sana kupita kiasi na kutukosesha raha. Japo kujamba ni kawaida na kila mtu anajamba kila siku, kuna watu wengine wanapata shida ya tumbo kujaa gesi na hivo kutoa gesi chafu mara kwa mara kuliko kawaida.Kitaalamu tatizo hili huitwa flatulence.

Ushuzi ni kitu gani
Ushuzi (fart) hutokana na gesi inayozalishwa tumboni kutokana na hewa tunayovuta na matokeo ya usagaji wa chakula tumboni, kwahivo kutokea kwa ushuzi inaweza kutofautiana kwa kila mtu kutokana na mazingira na hali yake ya mwili.

Kama ambavyo umewahi kujishuhudia mwenyewe kuna wakati unajamba ushuzi wenye harufu mbaya, wakati mwingine hakuna harufu, ama unaweza kujamba kwa sauti au pasiwe na sauti. Mtu mzima mwenye afya anajamba mara 14 mpaka 18 kwa siku, wakati mwingine anajamba hata bila kujijua kwasabau hakuna harufu au sauti.

Kwahivo unapotaka kuchambua hali ya afya yako ni muhimu zaidi kutazama harufu ya ushuzi na dalili zingine unazopata baada ya kujamba.

Je, kuna jambo lolote la Kuhofia kuhusu Kujamba kwako?
Inaweza kuwa ndio au hapana,kwasababu wakati mwingine inategemea na aina ya chakula ulichokula, mfano ukila vyakula vyenye kambakamba kwa wingi(high-fiber diet) na vyakula asili utapata ushuzi wa kawaida.

Lakini unapojamba kila mara kupita kiasi na ikiambatana na dalili zingine inaweza kuwa ni kiashiria kwamba kuna tatizo kwenye mfumo wako wa chakula.

Tatizo hili laweza kuwa ni mabadiliko ya mazingira ya ndani ya tumbo (microbiome), kutokana na kukua kwa bakteria wabaya au fangasi.

Kilichopo kwenye Ushuzi
Fahamu kwamba ushuzi unatengenezwa kwa gesi, na gesi gesi kuu ni Nitrogen, ambapo watafiti wanasema inachangia kwa asilimia 20 mpaka 90 ya gesi chafu inayotoka wakati umejamba.

Gesi zingine zinazounda ushuzi ni kama carbon dioxide ambayo huchhangia asilimia 10 mpaka 30, oxygen ambayo huchangia aslimia 10, methane ambayo inachangia asilimia 10 na gesi ya hydrogen inachangia asilimia 10 mpaka 50.

Muunganiko wa gesi hizi ndio unaofanya harufu mbaya ya ushuzi kwasababu baadhi ya gesi zina kemikali ya sulphur ambayo ndio kiambata kinachotoa harufu, sulphur hupatikana pia kwenye vyakula kama mayai na mboga kama kabeji.

Kwanini kuna utofauti wa asilimia za gesi zinazounda ushuzi na harufu?
Hii ni kwasababu hali ya ushuzi inatofautiana kwa mtu na mtu kutokana ni kiasi cha hewa aliyobugia, chakula alichokula na hali ya umeng’enyaji wa chakula tumboni. Unaweza kushangaa ni kwanini unajamba lakini hakuna harufu mbaya inayotoka.

Kiambata cha sulphur ndicho hufanya harufu kuwa mbaya zaidi ya kunuka, asilimia moja tu ya sulphur inaweza kuleta harufu mbaya kwenye ushuzi, kwahiyo kama aina ya chakula ulichokula kinategeneza sulphur kwa wingi basi ushuzi wako utakuwa unanuka.

Nini hasa kinasababisha Kujamba
Unaweza kuwa unajiuliza nini hasa hupelekea kujikusanya kwa gesi ambayo baadae unaitoa kwa njia ya kujamba. Japo visababishi vya ushuzi vinaweza kutofautiana kwa mtu na mtu lakini gesi inayotolewa ni ile ile haitofautiani.

Gesi iliyojikusanya tumboni hupita kwenye utumbo mdogo na baadae kutolewa nje kama unavyotoa haja kubwa. Wakati mwingine utoaji wa gesi hii unaweza kuambatana na maumivu hali inayoashiria pengine kuna chakula ulichokula kina tatizo, au hakijachakatwa vizuri na hivo kuchacha.

Tatizo lingine kujaa gesi tumbo kiakwaida huambatana na kujamba
Baadhi ya sababu kwanini gesi inajikusanya tumboni mwako na kukupelekea kujamba ni pamoja na
  • Kumeza hewa (aerophagia): Hii inamaanisha kumeza hewa pasipo matarajio ambayo inajikusanya tumbo na kisha unaitoa kwa njia ya kujamba au kwikwi. Sababu mojawapo kwanini unabugia hewa tumboni ni kwasababu unakula chakula haraka au kutotafuna chakula vizuri kabla ya kukimeza. Kwahivo kama unaona wewe ni mtu wa kula haraka , jaribu kurekebisha tabia hii, tafuna taratibu ili usimeze hewa pamoja na chakula.
  • Kukusanyika kwa hewa chafu: Kujamba ushuzi unaonuka maranyingi hutokana na gesi inayozalishwa na bacteria waliopo kweye utumbo mpana baada ya uchafu ambayo haujafozwa kuchacha.
  • Mabadiliko ya mazingira ya ndani kwenye mfumo wa chakula (microflora): Fahamu kwamba katika mfumo wote wa chakula kuanzia mdomoni, kwenye koo, tumboni, mpaka kwenye utumbo kuna bacteria wazuri na wale wabaya. Bacteria wazuri wanasaidia katika uchaataji wa chakula na pia kama kinga dhidi ya athari za bacteria wabaya. sasa inapotokea bacteria wabaya wamakuwa wengi kuzidi wale wazuri ndipo utaanza kupata matatizo kama gesi tumboni na chakula kutosagwa.
  • Constipation(Kupata choo kigumu na kukosa choo kwa muda mrefu: Inaweza kusababisha mkusanyiko wa gesi chafu na kukupelekea kujamba sana kwasababu ukiwa na tatizo hili kasi ya mmen’genyo wa chakula inapungua.
Kwanini watu wengi wanajamba kwa sauti na wengine wanajamba polepole na harufu ni mbaya zaidi?

Hii yaweza kusababishwa na mpangilio wa misuli ya utumbo mpana na eneo la haja kubwa. Baadhi ya misuli inakusaidia kubana ushuzi na kuutoa taratibu pasipo sauti.

Kama kila mara ukijamba sauti ni kubwa basi fahamu kwamba misuli ya eneo la haja kubwa(sphincter muscles) imelegea kiasi kiasi cha kuruhusu hewa kutoka bila ridhaa yako.

Je, kujamba kuna Faida yoyote kwako? au kuna Madhara?
Kujamba ni kitu cha kawaida na moja ya njia ya mwili kutoa hewa chafu, kama vile tunavyopumua kutoa nje carbondioxide.

Kwahivo kama unajamba usihisi kama ni jambo baya la kupambana nalo, maana wakati mwingine kujamba kunaweza kuwa ni ulinzi na kwama tumbo lako linafanya kazi vizuri.

Vyakula vyenye kambakamba mfano matunda, mboga za majani, viazi, magimbi, uwele na ugali wa dona husababisha gesi kwenye mfumo wako lakini bado vyakula hivo vinatoa mbolea kwa bactetia wazuri kukua ambao watakukinga dhidi ya magonjwa kam saratani y utumbo, kisukari, uzito mkubwa na kitambi na magonjwa ya moyo.

kwa upande mwingine ni kwamba kama unajamba sana kupita kiasi, inaweza kuashiria kuna tatizo la tumbo matatizo haya ni kama
  • Mwili kukataa aina fulani ya chakula(Food intolerance)
  • Kutoboka kwa kuta za utumbo mwembamba(leay gut syndrome) na kusababisha sumu na vimelea kuingia kwenye mzunguko wa damu.
  • Kukua kwa vimelea kwenye utumbo/small intestinal bacteria overgrowth(SIBO).
Utajuaje kama kujamba kwako si kwa kawaida
Cheki kama kujamba kwako kunaambatana na dalili hizi ndipo uchukue hatua. Dalili hizi ni kama
  • Kukosa nguvu na uchovu
  • Ngozi kucharuka na kupata rashes au chunusi
  • Aleji mfano kutokwa machozi na koo kuwasha
  • Kuharisha na kukosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
  • Kupata mkojo wenye damu au kinyesi chenye damu
  • Mumivu kwenye kwapa na katikati ya paja na viungo vya uzazi na
  • Mabadiliko ya joto la mwili, uzito, usingizi na mpangilio wa hedhi
Namna gani Upunguze Kujamba kupita kiasi
Haya ni matamanio ya kila mmoja wetu ili kupunguza aibu ya kujamba mara kwa mara pengine ukiwa na kundi la watu.

Kitu cha kwanza kubadilisha ni lishe yako. Tumbo lako laweza kuwa linapata shida ya kuchakata aina flani ya vyakula au tumbo kuhifadhi zaidi sulphur, fangasi na bacteria.

Zoezi hili ni la kuajaribu maana watakiwa kufatilia ni aina gani ya chakula inakufanya kujamba sana, na siyo kila chakula kinaleta gesi kwa kila mtu. Baadhi ya vyakula vya kutizama zaidi ni kama
  • Maharage: Maharage ni chakula kikubwa ksababisha gesi kulio vingine. Ni kwasababu vimejaa aina ya wanga inayoitwa polysaccharides, ambayo inachacha kiurahisi inapoingia tumboni. Huhitaji kuacha kabisa kula maharage, ila fanya kuloweka kwenye maji usiku mmoja kabla ya kuyapika ili kupunza gesi inayozalishwa.
  • Maziwa na bidha za maziwa: kushindwa kumeng’enya maziwa (lactose intolerance) ni tatizo kubwa na linawapata watu wengi. Hii ni kwa bidhaa zote za maziwa. Bidhaa za maizwa zina aina ya sukari zinazouwa galactose na glucose amabazo ni ngumu kuchakatwa kiasi cha kupelekea gesi tumboni.
  • Mboga zenye sulphur: Mbona mboga zenye sulphur kwa wingi kama kundi la cruiferous, hapa kuna kabeji, broccoli na caulifolower huletekeza gesi kuliko mboga zozote zingine kwasabau zina kambakamba kwa wingi zaidi. Zinapopikwa gesi inapungua kiasi kuliko kuliwa mbichi.
  • Vyakula vilivyosindikwa ma kusafishwa(artificial, processed foods): Baadhi ya vyakula vya viwandani vyenye mafuta mabaya vinaweza kuwa vigumu kuchakatwa na hivo kupelekea gesi tumboni. Lenga kula vyakula asili na kutumia mafuta mazuri kama ya nazi na oilve kama kiungo cha kupikia. Kadiri unavokula vyakula asili nivyo unarahisishia kazi tumbo kusaga chakula vizuri.
Badili Mtindo wa Maisha ili Kupunguza Tatizo la Kujamba kwa
  • Kufuta kwenye lishe yako vyakula ambavyo siyo rafiki.
  • Tumia virutubishi (probiotics) ambavyo vitasaidia kurudia bacteria wazuri tumboni. Vyakula hivi ni kama maziwa asili ya mtindi na sprulina.
  • Weka vionjo kwenye lishe yako: Vionjo hivi husaidia kuimarisha usagaji wa chakula na kuua vimelea wabaya tumboni. Vionjo hivi ni kama manjano(tumeric), tangawizi, mdalasini na pilipili.
  • Fanya mazoezi na kunywa maji ya kutosha: Vyote hivi kwa pamoja vitakusaidia kutoa uchafu nje ya mwili na kusafirisha virutubishi ndani ya mwili. Mazoezi ya squats ni muhimu zaidi.

USHAURI NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU
Hilo tatizo linaitwa INDIGESTION kwa lugha teule. Kama alivyogusia huyo mrembo hapo juu, tatizo hili linatokana na vyakula ambavyo vinapokuwa tumboni haviyeyushwi ipasavyo/vinayeyushwa nusu nusu (partial digestion).

Kwa kuongezea ni kuwa si lazima viwe ni vyakula fulani tu, bali tatizo laweza tokea pale unapokula chochote, hii ni serious kidogo.

Ili tuwe na uhakika na visababishi (causes) ni lazima mtoe taarifa zaidi ili tuweze kufanya kitu kinachoitwa DIFFERENTIAL DIAGNOSIS, hii itatupeleka kwenye tatizo husika kwa kuchuja tatizo moja moja. Mfano, hali hii hutokea baada ya kula vyakula fulani tu? Au baada ya kuwa stressed? Etc.
---
Pole mdau kwa tatizo lako. Hii inaonyesha mfumo wako Wa mwili haupo sawasawa .Kwa kawaida mwili wa mwanadamu inatakiwa 80% iwe alkaline na 20% iwe acid.

Sasa ww inaonyesha una wingi Wa acid kuliko alkaline. Pia utakuwa na tatizo la kupata choo.Kwa kawaida inatakiwa mtu ambaye mfumo wake upo vizuri apate choo Mara 3 kwa siku.Hii ni kutokana na anavyokula. Kwa maana iyo basi ni pm kwa kutatua tatizo lako maana ninauwezo Wa kutibu tatizo lako
---
Kama baadhi ya watu walivyokushauri ni vizuri ukienda hospital na kufanya vipimo vya tumbo ikiwemo ultra sound, yawezekana una dalili za mwanzo za vidonda vya tumbo, lakini pia yawezekana ww ni mlaji wa vyakula vyenye mafuta mengi ikiwemo kitimoto hivyo ndani ya tumbo kumejijenga layer ya mafuta na kusababisha tumbo kujaa gesi na kujamba kila mara.....ni vizuri ukipata ushauri wa kitaalamu hospital
---
Tumia mbegu za komamanga chukua mbegu hizo kausha kisha saga chukua unga huo kijiko kimoja chang'anya na maji ya moto kijiko kimoja cha chain kwa kikombe kunywa Mara mbili kwakutwa Mara sita uje hapa kutoa feedback
---
Ukipiga miayo, funika mdomo kwa kiganja chako cha mkono, au chochote. Kujamba sana pia husababishwa na hewa kujaa tumboni
---
Inawezekana ni dalili ya vidonda vya tumbo. Ila uthibitisho kamili ni vipimo vya kitaalam.

Pia jitahidi unapokula uache kubugia, yaani tafuna chakula ipasavyo kabla ya kumeza.

Kunywa maji mengi mkuu
---
kunywa maji mengi, epuka vyakula vyenye mafuta mengi, gesi nyingi kama maharage, fanya mazoezi na pia tumia dawa ya kupunguza gasi tumboni
---
Hatakiwi kutumia chochote kuondoa hiyo hali kwani hakuna tatizo lolote kiafya linalotokanalo na ujambaji, ila kama angekuwa hajambi au anapata ujambi Mara chache au la hapati kabisa, basi hilo lingeweza kuwa tatizo. Watu wengi huwa hawajui kuwa kujizuia kujamba ni jambo la hatari kiafya, na wanaoongoza kwa tabia hii ya kujizuia ni wanawake na hasa wawapo na wapenzi wao.

Nawashauri wote ushauri wa bure kabisa kuanzia sasa kwamba jambeni kwa kujiachia kabisa kwasababu kadri ujambavyo mara kwa mara ndivyo hutoavyo hewa chafu tumboni na hivyo kuwa salama zaidi kiafya.
---
JE, TUMBO KUJAA GESI LAWEZA KUWA CHANZO CHA MAGONJWA MENGINE MWILINI MWAKO?
Ndugu mpendwa, na ieleweke kuwa hali ya chakula kutokumeng’enywa tumboni mwako sio ugonjwa, bali ni baadhi ya dalili zinazokupata, kwa mfano; tumbo kuuma na kujaa gesi mara baada tu unapoanza kula chakula. Ingawa tatizo hili linaonekana kuwa la kawaida sana, lakini tatizo hili linaweza kutokana na vyanzo mbalimbali. Dalili za chakula kutokumeng’enywa unaweza kuzihisi mara kwa mara kila siku.
NUKUU: Hali ya kutokumeng’enywa kwa chakula tumboni inaweza kuwa dalili ya ugonjwa mwingine wa usagaji chakula tumboni mwako.
Je, Nini Dalili Za Tatizo Hili?
Watu wengi wenye tatizo hili wanaweza kuwa na dalili moja au zaidi, nazo huwa kama ifuatavyo:
Tumbo kujaa gesi wakati anapokula chakula
Tumbo kujaa gesi muda mrefu
Kuhisi maumivu ya tumbo la juu
Kuhisi kiungulia juu ya tumbo
Tumbo kuunguruma sana mara kwa mara na kuhisi maumivu chini ya kitovu
Kuhisi kichefuchefu na kutaka kutapika
NUKUU: Wakati mwingine watu wanaosumbuliwa na tatizo hili pia hupatwa na kiungulia, lakini health talk na jesca inasaema kumbuka kuwa kiungulia au chakula kutokumeng’enywa tumboni huwa ni hali mbili tofauti. Kiungulia huwa ni moto au maumivu unayoyahisi katikati ya kifua chako ambayo yanaweza kupenya mpaka kwenye shingo yako au mgongoni mwako wakati ama baada ya kumaliza kula.
Je, Nini Husababisha Chakula Kutokumeng’enywa Tumboni?
Chakula kutokusagwa au kumeng’enywa tumboni husababishwa na vyanzo vingi. Mara nyingi health talk na jesca inaeleza hali hii hutokana na mtindo wa maisha ya muhusika mwenyewe, hasa katika matumizi ya vyakula, vinywaji au madawa ya vidonge anayoyatumia. Visababishi vya tatizo hili huwa kama ifuatavyo:
Vyakula vyenye mafuta mengi sana, kama vile chips, roast, nk.
Vyakula vilivyokobolewa kama vile, ugali wa sembe, maandazi, chapati, nk
Utumiaji wa nyama mara kwa mara
Vinywaji vyenye caffeine nyingi,kama vile pombe, kahawa, nk
Uuaji wa chokleti,
Uvutaji sigara
Kuwa na wasiwasi
Mazoea ya kula au kula haraka haraka bila kujali kutafuna chakula vizuri
Na kuto kutafuna chakula vizur na kulainika huwa ndiy chanzo kinaanzia haapo mdomon
Matumizi ya madawa ya vidonge vya antibiotic au vyenye kupunguza maumivu mwili mwako kama vile panadol, nk. Yafaa sana kupata ushauri kwanza wa daktari kabla hujatumia madawa hayo.
Kwan tambua madawa huwa ni kuzuia maambukizi yasiendelee
Wakati mwingine hali ya chakula kutokumeg’enywa tumboni husababishwa na magonjwa au matatizo yanayokuwa tumboni mwako kama vile:fuatana nami
Vidonda vya tumbo
Uvimbe tumboni(Gastritis)
Mawe ya figo
Kuvimba kwa kongosho
Saratani ya tumbo
Utumbo kuziba
Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye utumbo mwembamba(intestinal ischemia)
Je, Nini Madhara Ya Chakula Kutokusagwa Tumboni?
Kwa kawaida tatizo hili linapodumu kwa muda mrefu bila kufanyiwa ufumbuzi, basi linaweza kusababisha madhara yafuatayo katika mwili wako:
1.Mzunguko wa damu kuharibika na kuwa mdogo
2.Mgongo au kiuno kuuma
3.Miguu, au mikono kufa ganzi
4.Mwili kuchoka mara kwa mara
5.Kukosa hamu ya kula
6.Macho kushindwa kuona vizuri
7.Mapigo ya moyo kwenda mbio
8.Kichwa kuuma
9.Kutojisikia raha na kukosa amani
10.Viungo kuchoka na kijisikia uchof / uchakavu wa viungo
 
Ukipiga miayo, funika mdomo kwa kiganja chako cha mkono, au chochote. Kujamba sana pia husababishwa na hewa kujaa tumboni
 
Inawezekana ni dalili ya vidonda vya tumbo. Ila uthibitisho kamili ni vipimo vya kitaalam.

Pia jitahidi unapokula uache kubugia, yaani tafuna chakula ipasavyo kabla ya kumeza.

Kunywa maji mengi mkuu
 
Kwani wewe unaishi Marekani? isiwe ule ugonjwa wa mkuu wa dunia unakunyemelea.... mimi najua mganga kuna jamaa mmoja yuko syria kwa wale jamaa wa isl nenda huko na mwambie shida yako
 
kunywa maji mengi, epuka vyakula vyenye mafuta mengi, gesi nyingi kama maharage, fanya mazoezi na pia tumia dawa ya kupunguza gasi tumboni
 
Wadau wangu naamini hamjambo kabisa.Nikiwa kazini,nyumbani au hata nikikaa na wenzangu najisikia vibaya kwani huwa najamba sana na mjambo wenyewe ni ule wenye sauti.Nifanye nini kuepuka hali hii?

Mkuu uko vizuri,ukiona hivyo ujue mfumo wa injili yako uko poa,maana kujamba ni mfumo wa kutoa hewa chafu ndani ya tumbo lako na kulifanya tumbo liwe katika utendaji mzuri kimfumo,wewe jambatu,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom