Tatizo CHADEMA ni Uenyekiti: Kweli Humweka Mtu Huru!

Hongera sana ndugu bethlehemu kwa kusimamia Ukweli, Kama alivyosema mh Zitto, Uwongo hupanda Lifti ukafika mapema, Lakini Ukweli huja kwa ngazi, na kufika baadae ukatwaa nafasi yake. Sisi kama Jamii huru iliyoazimia kujenga Taifa la kidemokrasia, ni haki yetu kuukataa uwongo kama ilivyo wajibu wetu kuukubali ukweli, Itakuwa ni makosa kuuenzi uwongo kwa sababu unatupa faraja ya Muda tu.

Ukiangalia kwa anayotuhumiwa mheshimiwa Zitto, ni tuhuma tu, hakuna Uthibitisho wowote wa tuhuma hizo. kama ni Waraka, hakuna ushahidi unaomtia hatiani kuhusika nao. Kama ni kukihujumu Chama, Mwenyewe Mh Zitto ameomba achunguzwe, na ripoti iletwe chamani ionyeshe amekihujumu vipi.

Kinachomponza Zitto ni Umahiri Wake, Charisma yake, Upeo wake. MIONGONI MWA VIONGOZI WA CHADEMA WANAOMCHUKIA, SABABU KUU NI HUSDA ZAO, WIVU WAO NA HOFU YA UENYEKITI KAMA ULIVYOSEMA.
 
betlehem Kwanza ni lini uliitakia heri CHADEMA???
Kamwambie Zito amuulize Bwn Malema wa ANC umaarufu wake unampeleka wapi??
Wacha viburi vyenu CDM ni chama kipo watu wataondoka kina Zito watakiacha!! M/Kiti msimsumbue jibuni shutuma 11
Period.
 
Last edited by a moderator:
faizaFox upakaziaji wa ukoo sijui
Ukanda, dini, kabila hizo single zenu MaCCM zimechuja!! Sasa mnaelekea ukingoni!!
Wajinga mnaowasomba na maroli,
Kuwavisha matisheti na kuwalisha
Wali wamefunguka!! Mpambane kurudisha fedha zetu za Uswiss , wacha usanii wa Zito!! Vinginevyo muwe tayari kukimbia nchi!!
Mmekwisha tumaini lenu la Zito kwisha. By!!
 
Last edited by a moderator:
Ukweli utaja bainika mbona njia ya mwongo ni fupi! Kama zito ni muongo/mnafiki/msaliti ipo siku tutajua tu! Maana hata akina Shibuda walipokataa kuacha posho waliitwa wasailiti/wanatumiwa na CCM/wanaharibu chama/ wamenuliliwa/nk na wakaahidiwa kushughulikiwa lakini walipoanza kuchua posho leo hii kimya si msaliti/si mnafiki/hajanunuliwa na CCM/hana kosa tena nk. IPO SIKU UKWELI UTAJULIKANA tuache kukaririshwa nyimbo za msaliti/kanunuliwa/anaharibu chama bali tukae na tutafakari yasemwayo na wote walioko katika mzozo ukweli utapa mwenyewe na si wa kulazimishwa na mtu
 
Mbona hujajiapiza kutotoa na kupokea rushwa kwa namna yoyote ile? Kwa mantiki hiyo wewe ni mmoja wa mafisadi papa Tanzania. Huna lolote, viapo kibao kwa mambo madogo almradi umtetee mwanaCCM mwenzako Zitto.
 
Kwa atakaye kuwa na swali lolote aniulize .safari hii nitamjibu hapa hapa na kwa uwazi kabisa.Kwa hali ilivyo kwa sasa, hii ndio itakuwa njia bora kabisa!

Ndugu zangu, kwanza nawasalimu sana!

Kwa kipindi sasa nimekuwa nikijaribu kusisitiza kuridhiana na kurudisha uhusiano mwema miongoni mwa wanachadema kwa kukwepa kueleza wazi wazi kile kinachotokea dhani ya chama nikiamini kwamba wahusika wangenielewa na kuchukua hatua za haraka kwa kuwa wanaelewa vizuri kile wanachokifanya. Kwa bahati mbaya ni kwamba inaonekana jitihada hizo zimekwama na bado baadhi ya viongozi wa chama wanaendelea kuzunguka huku na kule wakifitinisha wanachama wenzao na wananchi. Hali hii ya uchonganishi naona sasa imefikia hatua mbaya kiasi kwamba naona hamna haja ya kuendelea kufichaficha mambo!.

Kwa mfano, Kufuatia hotuba aliyoitoa Mchungaji Msigwa huko Arusha 04/12/2013, ilikuwa kwa kiwango kikubwa imejaa uchonganishi na uchochezi miongoni mwa wanachama kufikia kiasi cha msikilizaji mmoja ndugu Exaud Mamuya kusema “ kutokana na speech ya Mh Msigwa, Zitto angetokea bahati mbaya angegombaniwa na kuraluliwa kama Simba aonavyo kitoweo.” Katika mazingira haya naomba sasa niwe muwazi zaidi kidogo.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Tatizo la msingi kwa sasa ndani ya CHADEMA, ni "u-mwenyekiti".Hizi mbio tunazoziona mitaani kwa sasa, na kurushiwa maneno kwa ndugu Zitto,ni matokeo tu lakini suala la msingi ni "u-mwenyekiti "ndugu zangu.Tatizo la msingi ni Zitto kuonekana anaonesha dalili za kugombea uenyekiti na kuonekana ana ushawishi ndani na nje ya chama hivyo asipochafuliwa na kufitinishwa haraka, anaweza akashinda uenyekiti kweli.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Imeonekana kwamba kutokana na umaarufu wa Zitto kutokana na mambo aliyokifanyia Chama na taifa kwa ujumla ukichanganya na uwezo wake binafsi, si rahisi kwa mtu mmoja kumchafua na akachafuka bali hilo linaweza kufanyika kwa ufanisi kwa kuunda kundi kubwa na ikiwezekana kuishawishi kamati kuu kufanya mchezo huo wa hatari, wakufedhehesha, na kukatisha tamaa kabisa; mchezo ambao ni dhambi kumbwa sana.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Kitu kinachofanyika kwa sasa, licha ya kwamba ni dhambi na udhalimu mkuu, kinasababisha wananchi kugawanyika makundi makundi bila sababu ya msingi. Kadhalika kunasababisha wote tuonekane kama watu ambao tunalenga kupigania vyeo na maslahi tu na tusio kuwa na maono wala uadilifu wa kiuongozi hali hiyo hutufanya tuonekane tuko radhi hata kumtoa mtu muhanga kwa dhuluma ili tufikie lengo..Hali hiyo haiwezi kuwa na manufaa kwetu binafsi, kwa chama wala kwa taifa letu.

Ndugu wana CHADEMA wenzangu,
Hatuwezi kuwa vionzi bora wala hatuwezi kupewa madaraka ya kuongoza nchi hii kwa kufanyiana hila, uzushi, fitna majungu na kuchonganishana wenyewe kwa wenyewe.

Ndugu wana CHADEMA, wenzangu,
Wakati wote tumekuwa tukimlaumu na kumkemea Naibu Katibu mkuu wa CCM, ndugu Mwigulu Nchemba kwa kufanya siasa chafu za fitna na kugombanisha watu. Sasa na sisi tunafanya nini sasa? Tunafanya nini sasa?tunafanya nini ndugu zangu!

MSIMAMO WANGU.

Mimi tangu nilipopata akili, nilijiapiza na nikamuomba mungu anisaidie kwenye mambo kadhaa!.

1.Nilijiapiza kujiepusha kwa uwezo na maarifa yangu yote kumdhulumu mtu yeyote kwa sababu yeyote na nikamuomba mungu anisaidie!.

2. Nilijiapiza kujiepusha kushirikiana na mtu yeyote kumuhujumu mtu yeyote kwa dhuluma na nikamuomba mungu anisaidie!.

3. Nilijiapiza kumkosoa mtu yeyote kwa njia ya hekma na busara na kumshauri ajirekebishe ikiwa anamdhulumu mwenzake kwa kutokujua au kwa makusudi na nikamuomba mungu anisaidie!.

Kwa sababu yeyote ile, sitakuwa tayari kuihalifu misingi yangu hii kwa sababu yeyote ile ,kwani kufanya kinyume na hapo, itakuwa ni kuchagua njia mbaya miongoni mwa njia mbaya kabisa !.


KWA SASA KILICHOBAKIA NI HIKI;

1. Mh. Mbowe! Muombe radhi Mh.Zitto kwani wewe unajua umemfanyia nini na unaujua vizuri mkakati unaoendelea. Mwenyekiti muombe radhi mwenzako yaishe tujenge chama na taifa letu!

2. Mh. Lema, umemkosea Zitto na wewe unaelewa hilo, muombe radhi tusoonge mbele tafadhali!,

3. Kilewo, Umefanya jambo ambalo si jema sana kwa kusambaza waraka wa kumchafua Zitto bila kujua au kwa kujua, muombe radhi Zitto yaishe tujenge chama na nchi yetu!.

4. Mchungaji Msigwa! Wewe ni mchungaji, tumia busara za kichungaji muombe zitto msamaha! Wewe umemchafua na unaendelea kuuchafua zitto kwa makusudi na hali unajua. Ni bora ukaomba radhi yakaisha.! hauwezi kupungukiwa na kitu Msigwa!

5. Yericko Nyerere na wenzako wewe tumekuwa tukiungana mkono katika mambo mengi na wewe unalijua hilo, ila katika hili mimi nafsi yangu inakataa!.Tumia uaminifu wetu kumuomba Zitto radhi kwani wewe unajua umemfanyia nini!.Yericko naomba kwa hili tuwe waaminifu na busara itawale.Naamini mungu atakuongoza vyema.

Nawasihi sana wale mnaoendelea kuzunguka mitaani. Tafadhalini sana wekezeni nguvu zenu katika kushughulikia matatizo ya watu badala ya kuwachonganisha wanachama ikiwa kweli ninyi ni waadilifu, wenye nia njema na chama pamoja na nchi hii. Hatuwezi kuwa na mapenzi mema kwa jamii kwa kuchonganishana ,kufitinishana na kuchafuana!

Ni matumaini yangu kwamba jambo hili la kuendelea kuzunguka watu wakichafuana litakoma na atakayeliendeleza wananchi watamuelewa vyema!.

Watu wengine bana. Ikiona unahamu ya kuandika unaandika weeeeeeee!!!. Kisha unaleta huku JF. Unafikiri hapa kuna CC ya CDM?.Mi naona hauna busara kuleta ----- wako hapa badala ya kupeleka huko huko kwenu.
 
WARAKA WA CHACHA WANGWE.


UTANGULIZI.



Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.


Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.


Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.

Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote.

Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.

Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang?anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.


Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-

MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=.

Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya

CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.


MADENI YA UCHAGUZI

Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.


Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI.


Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.

Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.


UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM


Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri.


Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha! Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.


Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa.

Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA


Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:

1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.


2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.



Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.

UTENDAJI WA KIBABE


CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR ? Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR ? Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM.



kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung?ong?o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii.

Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.



Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.


HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.

Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu.



Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.


Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro,


ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii. Naamini tutashinda.Mungu Ibariki CHADEMA Mungu Ibariki TANZANIA Mungu Ibariki AFRIKA
 
Ukweli utaja bainika mbona njia ya mwongo ni fupi! Kama zito ni muongo/mnafiki/msaliti ipo siku tutajua tu! Maana hata akina Shibuda walipokataa kuacha posho waliitwa wasailiti/wanatumiwa na CCM/wanaharibu chama/ wamenuliliwa/nk na wakaahidiwa kushughulikiwa lakini walipoanza kuchua posho leo hii kimya si msaliti/si mnafiki/hajanunuliwa na CCM/hana kosa tena nk. IPO SIKU UKWELI UTAJULIKANA tuache kukaririshwa nyimbo za msaliti/kanunuliwa/anaharibu chama bali tukae na tutafakari yasemwayo na wote walioko katika mzozo ukweli utapa mwenyewe na si wa kulazimishwa na mtu


utajulikana wakati zitto ameishakufa pengine

ifike wakati tujue kuwa sisi watanzania ni wanyama sana hasa kwenye mambo ya hela


walio safi na wazalendo ndio wanaohukumiwa bila hatia yeyote

kwenye tuhuma 11 za chadema kwa zitto hakuna sehemu zinazoonyesha zitto kununuliwa na ccm kama ambavyo akina mbowe wanavyowaamnisha watu
 
Mkuu betlehem, huwa nafuatilia sana mabandiko yako mengi hapa jukwaani na nimekuwa nikikuchukulia kama mtu mwenye uelewa mkubwa sana wa mambo haya ya kisiasa na nimekuwa nikiheshimu sana michango yako hapa. Najua ulikuwa tofauti sana na CDM mwanzoni lakini baadae ulisema umeamua kuwa upande wao.

Tatizo kubwa ninaloliona kwenye uzi wako huu ni kwamba umeamua kuchagua upande tayari na kwa maana hiyo umejitosa kuutetea kwa nguvu zako zote. Sitaki kuamini kabisa kwamba hata mtu wa aina yako anaweza kusimama na kutaka watu walete ushahidi juu ya mengi yanayosemwa dhidi ya huyo uliyejitosa kumtetea. Kuna mambo ambayo hayahitaji hata kuomba ushahidi ili kujua kwamba ni tatizo kwa huyu unayemtetea. Kwa mtazamo wangu mimi binafsi, sihitaji mtu yeyote kuniletea ushahidi ili eti nijiridhishe kwamba huyo unayemtetea ni mtu mwenye ubinafsi sana kwa maana ya yeye kwanza halafu taasisi (CDM) baadaye. Hili wala halihitaji ushahidi kutoka kokote isipokuwa ni wewe tu kufumbua macho na masikio yako ili uuone na kuusikia ukweli! Hivi unataka kuniambia unahitaji ushahidi gani ili kujua kwamba ZZK alikaidi makubaliano na wabunge wenzake wa CDM ya kugomea hotuba ya Rais wakati wa uzinduzi wa Bunge hili la sasa? Mtu ambaye anaenda kinyume na maamuzi ya pamoja ya taasisi wewe binafsi unamchukuliaje?

Kikubwa ambacho naona umekosea hapa ni kwamba ushauri wako si kwa ajili ya kumaliza mgogoro bali ni kwa ajili ya kuukuza. Nasema hivyo kwa sababu una upande tayari katika mgogoro husika na aina ya utetezi unaoutoa hapa ni sawa kabisa na ule ambao umekuwa na unaendelea kutolewa na watu ambao wako tofauti na CDM (rejea ushauri unaotolewa na watu wa CCM juu ya sakata hili). Kama ZZK anahujumiwa kisiasa, kwa nini isiwezekane na yeye akawa anahujumu wengine kisiasa? Ni kweli kwamba ndani ya CDM ni ZZK tu ndo mwenye uwezo wa kugombea na kuupata huo uenyekiti? Kama hivyo sivyo, kwa nini sasa huongelei wengine isipokuwa huyo tu?

Mkuu, kwa mtazamo wangu suala hili halitakwisha kwa hao uliowasema kuomba msamaha kwa ZZK bali ni kwa ZZK mwenyewe aidha kubadili mienendo yake na kukiri makosa yake ili kutokuacha maswali mengi au ajiondoe kwenye taasisi ambayo yeye (na wewe pia) anaamini haina demokrasia na kwenda kule ambako anaona kuna demokrasia. Hata kama hao uliowasema wamemzidi kete kisiasa ZZK, bado nadhani kwa kiasi kikubwa itakuwa ni kwa sababu yeye kawapa nafasi ya wao kufanya hivyo kutokana na makosa ya wazi kabisa ambayo huwa anayafanya!

you have used all your brains to scribe these

pole sana, haujui siasa na unalazimisha iwe kama unavyoona
 
Haswaaaaa,,,mbowe aache uchaguzi huru ufanyike zitto alikuwa mbali kisiasa na anajua,,,,babu anahubiri demokrasia ya kinafiki,,,,,msigwa nae analopoka ovyo tu. na ndo washauri wa mbowe.km wasomi mnawatukana chadema itabaki ya wajinga tu.
 
Zitto ni malaika siyo?yeye anakosewa tu na kamwe hakosei!I wonder what panel of fools constitute his team!
 
Zitto hapaswi naye kuomba radhi? Kama uko objective .......
kimsingi huyu jamaa katumia mda mrefu kuandika lakini mwisho sijaona matinki.kwa mtu makini huwezi kuibuka na kusema mbowe muombe radhi zit to maana unajua ulichomfanyia.juzi huyu jamaa alileta Uzi akiwasihi cdm wazungumze wayamalize lakini zit to arudishwe.cha msingi yeye angefunguka kama kuna habari anayo kuhusu mbowe kutumia Influence yake kama mwenyekiti kumuonea zzk katika maamuzi.zaidi ya hapo huyu sanasana atakuwa ama zzk mwenyewe au mmoja wa vijana wake.
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa tatizo ni wenyekiti na si vinginevyo.lkn watanzania wanajua mchango wa zitto si kwa chama bali kwa Taifa zima,ametumikia kamati nyingi na tumeona uwezowake kiuongozi,wote wanaombeza lazima tujiulize wamelifanyia nini taifa letu zaidi ya harakati uchwara na umahalufu wao binafsi, lEMA NA MSIGWA KUMPARAMIA ZITTO NI SAWA NA KUPE KUPARAMIA TEMBO NA HAWATATUAMINISHA UPONGO WAO TUMECHOKA SIASA ZA KINAFIKI.
 
Nakuunga mguu. Chadema kitasambaratika kwa sababu ya uenyekiti. Hivi kuna demokrasia ya kweli Chadema? Chadema ni taasisi binafsi au taasisi ya umma?
 
Mkuu uwa nathamini sana michango yako lakini niliposoma hapo chini( SIJASOMA HEKAYA NZIMA) nimekuona mtu wa OVYO SANA

Sijawahi kumwamini mia ya mia huyu ndugu na haya niliyategemea anytm."aweza sema asichomaanisha".
 
you have used all your brains to scribe these

pole sana, haujui siasa na unalazimisha iwe kama unavyoona

Mkuu, kwa bahati mbaya sana mimi si mwanasiasa na nayaona mambo haya si kwa macho ya kisiasa. Sijalazimisha kitu hapo kwenye mchango wangu isipokuwa nilikuwa nimetoa mawazo yangu tu ambayo nayo si lazima yakubalike.
 
Nakuunga mguu. Chadema kitasambaratika kwa sababu ya uenyekiti. Hivi kuna demokrasia ya kweli Chadema? Chadema ni taasisi binafsi au taasisi ya umma?
Chadema kwa Usanii,wao wanalalamikia tume ya uchaguzi sio huru,wao mbona hawaeshimu democrasia
 
Back
Top Bottom