Tathmini ya Mahojiano na Rais Magufuli: Pascal Mayalla aongea Star TV

Kitu kikubwa walichofeli jana ni kukosa nafasi ya swali la nyongeza..........Magu alijibu kijuujuu sana afu nje ya maswali
 
Eti mwandishi wa habari anatamka live, "Sijajutia KURA yangu." Kweli?! Mtu kama huyu alisomea chuo gani cha habari?
mwanaweni hata mimi nilishangaa...mpaka leo bado ninajiuliza ilikuwaje..alisukumwa na nini???tutaamini vipi kama kweli alimpigia..kulikuwa na sababu gani ya/za msingi kusema
 
Nchi hii hatuna waandishi ,labda waandishi wa udaku

Duh...vipi Tanzania Daima hakuna waandishi kweli pale???, na vipi kuhusu mwanahalisi nako hakuna waandishi???? tehtehtehtehtehteh....mchezo huu mimi binafsi naupenda sana...waandishi wasipotimiza matakwa ya watu Fulani hao ni waandishi wabaya au uchwara ila wakitimiza matakwa ya kundi Fulani hao ni waandishi makini !!!!!!!!!!!!duh...
 
Kipindi kiko Live kujadili mambo yaliyoandikwa sana magazetini kubwa ni mahojiano ya jana kati ya Rais na wanahabari. Pamoja na wageni wengine Paskali yuko ipande wa wageni wa Dar kufanya tasmini
Kuna mdau anaitwa Mansoor Jumanne ameshangaa sana waandishi kwenda bila kuwa na ajenda,anashangaa wahariri kwenda bila kukaa na kujadili kabla ya kuongea na Rais kiasi kwamba hawakujua hata watanzania wanataka nini.Amekiri kwamba hatuna jukwaa la wahariri nchi hii,anaendelea....jamaa yuko vizuri,atakuwa mwanaJF huyu

Mansoor Anashangaa eneo la mikopo kutokuulizwa kabisa wakati ni swala lililogusa kabisa watanzania.Ansema waongozaji kina Rioba walikosa umakini wa kuwa na follow-up questions walikuwa wanaruka ruka tu.
Mgeni wa mwanza ndg.Mansoor anashangaa wahariri kutokuwa na data,walikuwa wakiuliza maswali juu juu tu na kukubali majibu marahisi,hakutegemea Rais asiwe na majibu ya kona kona.

Amemsifu Paskali Mayala kuuliza swali kwa ushahidi.Ameshangaa mwandishi aliyeuliza kuhusu madawa akapewa majibu ya kawaida na akanyamaza tu bila kufanya rejea ya kauli ya Makamu wa Rais na Waziri wa afya.Anasema maswali yalikuwa shaghara bagara.Maswali yaliyakuwa kuwa kwa category.mf maswali ya katiba,utawala bora,michezog nk

Anashangaa swali la tuhima za rushwa ya milioni 10 kupewa majibu mepesi na waandishi kuridhika,ile ilikuwa kashfa nzito na iliyoibuliwa na mtu rasmi Kiongozi wa upinzani bungeni akimtuhumu waziri mkuu kiongozi wa serikali bungeni

Wanafuata wageni wa Dar msimamizi ni Angalieni Mpendu,yule aliyeuliza swali la watoto kuvaa nusu uchi jana.Anaanza kwa kujitetea kuwa aliuliza swali la kiuchokozi

Mgeni wa dar anasema ule ulikuwa ni wito wa Rais kwa hiyo haikuwa lazima kuuliza maswali ya kuchomeka labda waombe tena

Mayala anaeleza kufurahi kwa kupata fursa ya kuhojiana na rais. Anakiri kuwa moderators wa jana walikwama kabisa kuongoza mjadala.Anasema walijaa uwoga sana.Ilitakiwa waandishi wasimuone Magufuli kama rais hilo lingesaidia kuondoa uwoga,anasema Tido wa BBC sio huyu wa leo, Dr.Rioba wa kipindi kile sio huyu wa TBC haaaaa haaaaa nacheka kidogo.Moderators hawakuwa wakimrudisha rais kwenye maswali ya nyongeza au maswali yalikosa majibu vizuri

Anasema swali lake lilijibiwa lakini alitegemea moderators wangesimamia swali lile lipate majibu ya kina

Mgeni wa Dar anasema sio busara kuona swali limempeleka rais kwenye kona alafu unalazimisha rais ajibu halafu ionekane rais kashindwa.

Paskali anakiri kuwa si kweli kwamba waandishi hawakujipanga,tatizo lilikuwa ni muongozo,pia anashngaa kila swali likiulizwa rais anaongelea mambo ya kupiga dili.Kitu ambacho sio kweli hali ni ngumu kwa kila mtu anatolea mfano suala la mikopo

Paskali Mayala anasema Jamiiforums imemjenga sana sana,kutokana na mijadala mikali inayotokea humu JF

Dotto Bulembo anahoji kwa nini wakati rais anahojiwa na waandishi Waziri alikuwa anawasilisha sheria ya Huduma za habari.Je haikuwa spinning?[/QUOT

Mwandishi wa habari aliyebobea hufanya utafiti kwanza ili kuwa tayari katika mahojiano yeyote na mkuu wa nchi, Mfalme ama Malkia.
Jana ndo kulionyesha upungufu wa ufahamu miongoni mwa baadhi ya waandishi na wahariri. Wakiuliza mambo ambayo hayana tija ama kushindwa kulitengeneza swali ipasavyo.

Kuna mmoja aliniacha hoi alipouliza mambo ya MICHEZO! Kwanza nilishituka nakuona vipaumbele vya huyo jamaa vinaishia michezoni. Maendeleo ya watu kwake ni Simba na Yanga na ligi kuu.

Sasa mwandishi kama huyo si angemuuliza waziri wa michezo? Ili kuwaachia wengine waulize maswali yenye uzito wa kusaidia!
 
dolevaby kiongozi umenivunja mbavu, Gen angeishia getini.
ndomanake Manake mtukufu angemuona kwenye Pres conference mambo mwaili moja wapo lingetokea kutolewa nje naaliemruhusu kazi basi au asipengewa nafasi yakuuliza kitu
 
Daah yaani Pascal Mayala kapanda chart ghafla.......yaani mie nilikuwa namuona wa kawaida sana na asiyepende kujifunza zaidi.
japo sijui aliuliza swali gani maana mie niliaacha kuangalia dk ya 25, baada ya kuona maswali ya ovyo ovyo nahao ma moderator yaani wakawa kama ma mc wa kwenye harusi..
 
Huyo mtangazaji Mansoor jumanne ni mtu makini sana, namfaham personally.
Na alichukua tuzo za investigative journalism EJAT zilizopita pale Mlimani city mwaka huu na ikumbukwe katoka chuon just last year
Usishangae mwakani ukakuta anaandikia Gazeti la Uhuru
 
Eti mwandishi wa habari anatamka live, "Sijajutia KURA yangu." Kweli?! Mtu kama huyu alisomea chuo gani cha habari?
Kwa Ile Siku Yule Jamaa Nilimuona Kinyaa Nikasema Moyoni Huyu Ndiyo Mwandishi Mwanaccm Anayesema Rais Ni Wa Hivyo.

Wanaccm Wenyewe Wanajua Kuwa Walikosea
Hata Mwenyewe Kasema Alikuwa Anabep Kwenye Ile Nafasi Sasa SIM Ikajipiga Kwa Bahati Mbaya Ndiyo Anapata Ile Nafasi
Maana Yake Haki Ilivurugwa Ndiyo Akapenyezwa
 
Waandishi Walipoambiwa Leo Mtakula Diko La Ikulu Basi Wakachanginyikiwa Na Kukaza Kuuliza Maswali Ya Vijuweni Halafu Dr Ryoba Na Tindo Tunawaona Wepesi Mno Nadhani Njaa Sijui Zinawapa Tabu

Dikodiko La Ikulu Limewafanya Wajione Siyo
Wahariri Weupe Kama Wazungu
Bora Ukijiona Huna Confidence Kwenye Hadhara Kutuma Mwakilish
 
Kipindi kiko Live kujadili mambo yaliyoandikwa sana magazetini kubwa ni mahojiano ya jana kati ya Rais na wanahabari. Pamoja na wageni wengine Paskali yuko ipande wa wageni wa Dar kufanya tasmini
Kuna mdau anaitwa Mansoor Jumanne ameshangaa sana waandishi kwenda bila kuwa na ajenda,anashangaa wahariri kwenda bila kukaa na kujadili kabla ya kuongea na Rais kiasi kwamba hawakujua hata watanzania wanataka nini.Amekiri kwamba hatuna jukwaa la wahariri nchi hii,anaendelea....jamaa yuko vizuri,atakuwa mwanaJF huyu

Mansoor Anashangaa eneo la mikopo kutokuulizwa kabisa wakati ni swala lililogusa kabisa watanzania.Ansema waongozaji kina Rioba walikosa umakini wa kuwa na follow-up questions walikuwa wanaruka ruka tu.
Mgeni wa mwanza ndg.Mansoor anashangaa wahariri kutokuwa na data,walikuwa wakiuliza maswali juu juu tu na kukubali majibu marahisi,hakutegemea Rais asiwe na majibu ya kona kona.

Amemsifu Paskali Mayala kuuliza swali kwa ushahidi.Ameshangaa mwandishi aliyeuliza kuhusu madawa akapewa majibu ya kawaida na akanyamaza tu bila kufanya rejea ya kauli ya Makamu wa Rais na Waziri wa afya.Anasema maswali yalikuwa shaghara bagara.Maswali yaliyakuwa kuwa kwa category.mf maswali ya katiba,utawala bora,michezog nk

Anashangaa swali la tuhima za rushwa ya milioni 10 kupewa majibu mepesi na waandishi kuridhika,ile ilikuwa kashfa nzito na iliyoibuliwa na mtu rasmi Kiongozi wa upinzani bungeni akimtuhumu waziri mkuu kiongozi wa serikali bungeni

Wanafuata wageni wa Dar msimamizi ni Angalieni Mpendu,yule aliyeuliza swali la watoto kuvaa nusu uchi jana.Anaanza kwa kujitetea kuwa aliuliza swali la kiuchokozi

Mgeni wa dar anasema ule ulikuwa ni wito wa Rais kwa hiyo haikuwa lazima kuuliza maswali ya kuchomeka labda waombe tena

Mayala anaeleza kufurahi kwa kupata fursa ya kuhojiana na rais. Anakiri kuwa moderators wa jana walikwama kabisa kuongoza mjadala.Anasema walijaa uwoga sana.Ilitakiwa waandishi wasimuone Magufuli kama rais hilo lingesaidia kuondoa uwoga,anasema Tido wa BBC sio huyu wa leo, Dr.Rioba wa kipindi kile sio huyu wa TBC haaaaa haaaaa nacheka kidogo.Moderators hawakuwa wakimrudisha rais kwenye maswali ya nyongeza au maswali yalikosa majibu vizuri

Anasema swali lake lilijibiwa lakini alitegemea moderators wangesimamia swali lile lipate majibu ya kina

Mgeni wa Dar anasema sio busara kuona swali limempeleka rais kwenye kona alafu unalazimisha rais ajibu halafu ionekane rais kashindwa.

Paskali anakiri kuwa si kweli kwamba waandishi hawakujipanga,tatizo lilikuwa ni muongozo,pia anashngaa kila swali likiulizwa rais anaongelea mambo ya kupiga dili.Kitu ambacho sio kweli hali ni ngumu kwa kila mtu anatolea mfano suala la mikopo

Paskali Mayala anasema Jamiiforums imemjenga sana sana,kutokana na mijadala mikali inayotokea humu JF

Dotto Bulembo anahoji kwa nini wakati rais anahojiwa na waandishi Waziri alikuwa anawasilisha sheria ya Huduma za habari.Je haikuwa spinning?
Jana ndio nilipata kuja ni kwa nini Mkapa alikuwa anawadharau sana waandishi wetu, kwa maswali yale Huwezi kuacha kuwadharau ndio maana JPM aliwaambia ulizeni mtachoka wenyewe!

Kwa tafsiri ya haraka ya kilichofanyika jana naweza kusema ilikuwa "Hafla ya waandishi wa habari ya kumpongeza raisi kwa kumaliza mwaka mmoja Ikulu"
 
Swali lilikuwa moja tu la pasco pekee, maswali mengine hayakuwa maswali bali yalijielekeza kama Maoni na ushauri ingawa wauliza maswali waliyafanya kama ndio maswali, nimefurahi sana angalau kwa sasa watu wa habari watajipanga upya na kujielekeza huko kunako dhaniwa kama muhimili wa nne wa dola usio rasmi
 
Unapokua Mwalimu mwenye chuki kwa Mwanafunzi fulani, siku huyo Mwanafunzi anapofaulu Mtihani unaweza usitambue uwezo wake bali ukaanza kuwaluamu Walimu wenzako kwa kutunga mitihani mirahisi.
 
Back
Top Bottom