TARURA na Parking ya wizi

Chills

Member
Aug 24, 2018
51
74
Habari za jioni wadau!

TARURA na mfumo wao wa maegesho maeneo ya mijini imekuwa na udanganyifu mkubwa sana.

Imetokea mara 2 naangalia kama nadaiwa nakuta deni na ukifuatilia naonesha maeneo ambayo sijawahi kwenda na nilipata fursa ya kupata msaada wa mtu wa TARURA nikaambiwa walipiga picha system ikagoma na ikabidi waingize namba manually ndipo walipokosea na hivyo kunifutia deni.

Imetokea tena leo katika kuangalia nimekuta nadaiwa kama elfu 6 hivi nikamtafuta mtu wao anisaidie kuangalia inaonekana nilipaki maeneo ya Saba saba na Uwanja wa Taifa. Mimi maeneo yale kwa mara ya mwisho nimeenda zaidi ya miaka mi 3 iliyopita.

Je ni wangapi wanabambikiwa madeni?
Je napataje msaada kutatua kama simjui mtu TARURA?
 
mimi pia huwa sitoki na gari kabisa labda kwa miezi miwili mara moja tu kwa dharura lakini nikijaribu kuchech deni nakuta nadaiwa deni sehemu sijaenda kabisa na tarehe hizo mimi sijatoka na gari ipo moja ina namba ya gari nyingine lakini mimi ndio nadaiwa ukiingiza kumbukumbu inakuja namba ya gari sio yangu lakini deni gari yangu ndio inadaiwa
 
mimi pia huwa sitoki na gari kabisa labda kwa miezi miwili mara moja tu kwa dharura lakini nikijaribu kuchech deni nakuta nadaiwa deni sehemu sijaenda kabisa na tarehe hizo mimi sijatoka na gari ipo moja ina namba ya gari nyinge lakini mimi ndio nadaiwa ukiingiza kumbukumbu inakuja namba ya gari sio yangu lakini deni gari yangu ndio inadaiwa
Mfumo wao ni wa kilaghai sana, sijui sisi wananchi tunakimbilia wapi
 
Mimi mwenyewe nimebambikiwa sehemu ambayo sijawahi kupaki na karibu kila siku naingiziwa nimepaki Kamanga mwaza wakati niko dar es salaam. Bili imeshafika 11000 nabado inaongezeka.
Nimeshindwa kuwasiliana na Tarura kwasababu system yao haina contact yeyote.
Niliwasiliana na mkata tiketi akanipa namba ya ofisi yao ya kinondoni ndio akaniambia kituo cha kamanga kipo mwanza na hawezi kubadilisha mpaka mtu wa mwanza abadilishe.

Naomba kama huyo mtu wako anaweza kukuta namba za mhusika wa parking wa Tarura utuwekee hapa au waiweke kwenye system yao

Mimi niliona vituo nilivyo wahi kupaki kwenye system ya ya website.
 
Back
Top Bottom