Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

huyu hilo swali atalikuta polisi central, akishindwa kujielezea lazima awe katika target za polisi

ila kweli kwamba silaha ni hatari sana tofauti na wengi wanavyofikiri, huwezi kumwambia hata mkeo akuchukulie ndani pia ni hatari kwa uhuru wako unaweza kwenda jela hivihivi kama taratibu zitafuatwa inavyotakiwa.

Bastola/Bunduki si nzuri sana kumiliki,ni hatari kwako pamoja na familia,kuna mazingira yanakulazimu kumiliki Bastola kwa mfano dereva wa malori,site engineer na kazi zinazofanana na hizo lakini kama ni sifa ka za mcharo kuringishia watu bar au majirani haikufai maana unaweza ukaja enda jela hivi hivi.
 
Uko uzi humu juu ya hii kitu. Search utapata mengi sana maoni.

1. Bunduki ni hatari kuliko maelezo, jiandae kwa hilo kwanza kabla ya kuamua kuwa nayo!!

2. Hata kama una hela kama BoT sisitiza kufuata taratibu zote zilizowekwa juu ya mchakato la sivyo utajuta hata kuwa na hizo pesa!!!

Ukiamua kumiliki bunduki basi umeamua kuwa na mume mwenza/mke wa pili hapo ndani!!! Anakuja kubadili mfumo wako wa maisha!!!
Shukran sana ndugu
 
Vijana watanzania bwana wakikamata milioni 10,Brevis na vyumba viwili mavulunza na wao wanataka kumiliki bunduki,ni shida kweli.....Kama hauna matatizo na mtu,sio dhulumati haina haja ya kuwa na bastola.

Ni kwaajili ya usalama wangu me mwenyewe na si kama ulivyosema mkuu...
 
Ni kwaajili ya self defense baada ya kupata vitisho(vitisho vya maisha) aidha ninunue silaha kuokoa maisha yangu pindi itakapohitajika au nisubiri kuuwawa

Utakapoulizwa hili swali polisi,useme ni kwa ajiri ya ulinzi binafsi tu,na wala si kwa sababu umetishiwa hutapewa kibari na badara yake utaambiwa hii kazi ya kudiri na aliyekutishia maisha uwaachie wao.

Kiuhalisia haitakiwi utafute bunduki baada ya kuchokozwa.utaitumia vibaya tu.
 
Ucpate Shida ,bunduki Ya Kwanza Kubwa Ya Kuwa Nayo Ni "Yesu Kristo" Kwnz Una Tsh.Ngp? Una Makampuni Mangapi? Sio Hata Wengi Tu Kwny Kitongoji Hawakujui. Mtegemee Mungu. Kwa Ushauri Njoo Kwny Mada Yangu Ya "Mungu Ameshuka Tanzania"
 
Ni kwaajili ya self defense baada ya kupata vitisho(vitisho vya maisha) aidha ninunue silaha kuokoa maisha yangu pindi itakapohitajika au nisubiri kuuwawa

Nani alikwambia Bastola inaokoa maisha? Mtu akiamua kukuua hata uwe na AK-47/AR-15 anakumaliza tu,maana kosa moja goli moja,Bastola ni kwa usalama wa kuwakimbiza vibaka tu wa mtaani.Yule Bilionea wa Arusha msuya alikuwa na bastola wakati anauliwa.Mimi naamini kama hauna beef na watu,sio dhulumati,hauli wake za watu,sio tapeli haina haja ya kuwa na bastola.
 
Nahitaji kumiliki silaha haswa Bastola (pistol). Ni njia gani nipite ili kufanikiwa kupata?
Je ni kununua kwanza au ni kujaza form ya maombi kwanza? Kipi kinatangulia?

Asanteni
 
Nimefurahia wote waliochangia,naomba nijuzwe sheria ya mtu kujilinda mwenyewe kwa kutumia silaha za moto kwa tanzania inasomekaje.mfano wajanja walikuja kwenye duka langu la mpesa na mapanga wakachukua mzigo tena nilikopa bank wakaondoka nao..

Je sheria inasemaje kama nina bastola,naruhusiwa kumpiga wapi?

je inakuwaje katika kujihami nikamjeruhi mtu mwingne labda mpita njia.

Je sheria inasemaje nikiamua kumkimbiza mhalifu sehemuyenye watu wengi kama mtaa wa kongo.

Nauliza haya mana nimeibiwa mara mbili ila marafiki zangu ambao wako kwenye vyombo vya usalama wananikataza nisimiliki bastola

wadau naomba mwenye majibu ya hili swali anisaidie,maana binafsi naona hayo siju wapi pa kununua,kusajiri na mengine ni additional tu.swali la huyu mdau ndo swali hasa.msaada jamani.
Cc,mbangaizaji,kitia ,mbu , zanziba na wengine
 
Back
Top Bottom