Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Mkuu mimi ninavyofahamu kama unataka kumiliki kwa mara ya kwanza utaratibu ni huu:

1. Utanunua silaha kutoka maduka ya Mzinga Corporation au Tanganyika Arms Ltd au kutoka kwa mmiliki halali ambapo utakuwa na mkataba wa mauziano na pia kitabu cha umiliki wake (kama umenunua kwa mtu). Hiyo silaha hautapewa ila itabaki mikononi mwa uhifadhi wa Mzinga Corporation, Tanganyika Arms au central police station na wewe kupewa nakala ya Receiving Note kuonyesha kwamba silaha imebaki mikononi mwao kwa utunzaji. Kama ni silaha ya urithi basi kuwepo na muhtasari wa kikao cha wanandugu kilichoridhia wewe kumilikishwa silaha hiyo (wakati huo silaha inayotakiwa kurithiwa ikiwa mikononi mwa moja ya hizo sehemu nilizotaja hapo juu).

2. Utaenda polisi (mfano ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya) na kupewa fomu utakayotakiwa kuijaza maelezo yako kama jina, unapoishi, sababu za kuhitaji silaha, maelezo ya silaha uliyonunua.

3. Fomu yako itatakiwa ipate maoni ya serikali yako ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata yako (hawa watatakiwa pia kuandika muhtasari kuonyesha kuwa wamekujadili na kukukubalia). Hapa inaweza kuchukua siku chache tu au muda mrefu. Itategemea na UCHESHI wako.

4. Utatakiwa kupitisha fomu yako kwa hakimu au mwanasheria. Hapa ni suala la dakika chache tu na uchakavu kidogo.

5. Utatakiwa uende polisi forensic department kuchukuliwa alama za vidole kupata clearance certificate kuonyesha kuwa hauna kosa lolote la jinai. Kuchukua alama na kupata majibu ni ndani ya kama siku tatu hivi japo kuna uwezekano pia wa kupata majibu siku hiyo hiyo. Na kwa ujumla hapa hapana usumbufu wowote. Kuna malipo kidogo utalipia. Kama sikosei ni Tshs. 3,000/= au 5,000/=.

6. Ukiwa na muhtasari huo wa kamati ya kata, barua yako ya maombi (covering letter), clearance certificate ya Forensic department, fomu yako iliyokwisha sainiwa na ofisi ya serikali ya mtaa, kamati ya ulinzi na usalama ya kata, hakimu au mwanasheria utavipeleka ofisi ya kamanda wa polisi wa wilaya ili nae akusainie covering letter yako na ile fomu yenye maelezo yako na silaha. Hapa ndipo uchukua muda kwani lazima kuwe na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kitakachokaa na kujadili maombi ya watu wengi na wewe kutakiwa kuhojiwa mbele ya hiyo kamati ambayo vikao vyake ufanyika mara moja moja. Ukikubaliwa muhtasari wa kikao utaandaliwa na nakala yake kuambatanishwa kwenye maombi yako. Kama nilivyokwishasema hapa ndipo nyaraka zinaweza kukaa muda mrefu zaidi nadhani kuliko kwingine pote (hata miezi kadhaa) kwa sababu vikao vya kamati ufanyika mara moja moja.

7. Kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ndiye katibu wa kamati ata forward hizo nyaraka zako ili zikapitishwe pia na kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu, na hatimae kwa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai ambaye ndiye anaetoa kibali cha umiliki wa silaha husika. Huku kwa kamanda wa polisi wa mkoa, kamanda wa polisi wa kanda maalumu na pia kwa Mkurugenzi nyaraka hazikai sana.

8. Kibali hicho uwa valid kwa muda wa miezi mitatu na usipokilipia ndani ya muda huo utalazimika kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuongezewa muda wa kulipia kibali hicho.

9. Ukishalipia hicho kibali utaenda wizara ya mambo ya ndani makao makuu (kwa watu wa Dsm) ili ukaandikiwe kitabu cha kumiliki silaha kwa jina lako na pia chenye picha yako (Firearm Licence). Zoezi hili linahitaji muda mfupi tu siku hiyo hiyo.

10. Utachukua kitabu chako na kwenda ofisi ya kamanda wa polisi wa mkoa ili uandikiwe kibali cha kukuruhusu kununua risasi (haichukui muda-dakika chache).

11. Utaenda ulipohifadhi silaha yako (Mzinga au Tanganyika Arms au central police station) ukiwa na leseni yako na pia kibali cha kununulia risasi na hivyo kukabidhiwa silaha yako na pia kuuziwa risasi kwa idadi iliyokubaliwa kwenye kibali. Hapa utatakiwa kulipia storage charges za hiyo silaha tangu ulipoiacha hapo hadi siku hiyo unapotaka kuichukua.

12. Baada ya kupata leseni ya umiliki wa silaha kila mwaka (kuanzia Julai hadi Septemba) unatakiwa kulipia leseni yako. Baada ya Septemba utatakiwa kulipa na faini.

Kwa mtu anaebadilisha kunakuwa hakuna mlolongo mrefu kama hapo juu. Ataandika covering letter kwenda kwa kamanda wa wilaya anayoishi akiwa na vielelezo vyote vya silaha mpya na ya zamani. Lakini hakutakuwa na haja ya muhtasari wa vikao vya kamati za ulinzi na usalama vya ngazi ya kata na pia wilaya ambavyo ndivyo vinavyosababisha zoezi zima kuchukua muda mrefu na pia usumbufu usio wa lazima (hasa huku ngazi ya mtaa na kata kwani kama mjuavyo kila mtu anataka nafasi yake imwezeshe kupata mboga ya nyumbani na pia jioni kujenda heshima baa).

Angalizo: Mimi siyo polisi na wala siko ofisi zinazohusika kutoa leseni za umiliki wa silaha. Nilichoandika ndicho ninachofahamu kwa upande wangu kama mdau wa kawaida. Hivyo kunaweza kukawa na masahihisho fulani kwenye maelezo yangu kutoka kwa wenye ufahamu zaidi. Hata hivyo naamini kama masahihisho yapo basi yatakuwa si makubwa sana.
dah! kwa mtindo huu bora kupitia chocho tuu,,

ila pisto muhimu sna
 
Wakuu naomba kujua taratibu za kufuata kumiliki silaha kihalali, mahali wanapouza na njia za kufuata.

Kama kuna shortcut za vichochoron za kupata sio mbaya mkiniwekea hapa.
Mie ya kwangu mwaka sasa nasubiria kibali bado na kibali ndio issue kununua sio issue
 
Chicago unapa in 1 minute.... Nenda Mzinga watakupa maelekezo yote. Ukitaka harak nenda na m2zako wewe wape info zako watamaliza process wao. Wewe utapigiwa simu ukabebe mkwaju wako.
Hakuna shortcut ya kupata silaha Hata uwe Na million 10. Hiyo process ya kupata silaha Na has a pistol ni ndefu mno Na huwezi kuwaonga wote. Kumbuka Hata mkuu Wa wilaya Na mkuu Wa mkoa wanahusika kwa Nyakato tofauti katika hiyo process Na hapo hatujazungumzia TISS. Usimdanganye mwenzako.

Tiba
 
Wakuu habari,

Hili swali lina ni tatiza kidogo, nimejaribu kuperuzi peruzi lakini nimeishia kufahamu vigezo vya na hatua za kumiliki silaha lakini hakuna mahali nilipoona ni aina gani ya silaha unaruhusiwa kumiliki.
Mwenye kujua tafadhali..
 
1. Upinde na mishale yake.
2. Panga.
3. Rungu.
4. Sime.
5. Gobole.

Miliki hizo wala huhitaji kibali. Hata town unakatiza nazo haina shida.
 
Back
Top Bottom