TANZIA: Jaji Mstaafu Robert Kisanga afariki dunia

View attachment 683355
Jaji Kisanga (Aliyesimama)​



Jaji mstaafu, Robert Kisanga amefariki jioni hii Katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Kisanga aliwahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, pia alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kabla ya kustaafu mwaka 2008.

Anakumbukwa kwa hukumu ya Nyamuma. Kesi ya haki za binadamu ilifanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati yeye akiwa Mwenyekiti wa Tume huyo.


Aliyekuwa Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa aliipinga hukumu hiyo na Serikali haikutekeleza maagizo yoyote juu ya waathirika wa Nyamuma waliochomewa nyumba, uchomaji ulioongozwa na Marehemu Mabiti aliyekuwa DC wa kipindi hicho.
Pole sana kwa familia ya marehemu, pia familia ya mahakama kwa kumpoteza mtu muhimu katika usitawi wa familia na Taifa kwa ujumla.
 
Mbele yake Nyuma yetu.

Hii ni Safari ya Wote.

Hii ni Safari ambayo haina Ubaguzi, yaani yule mwenye NAULI atasafiri na yule ambae hana NAULI atasafiri pia.

Hii ni Safari ambayo si ya Tabaka la Watu fulani.

Hii ni Safari ambayo haikwepeki.

Hii ni Safari ambayo haichagui.

Hii ni Safari ambayo haina Muda/Wakti maalum.

Hii ni Safari ambayo haihitaji Maandalizi.

Hii ni Safari ambayo haikupi Muda wa kuagana na wako Wapendwa.

Hii ni Safari ambayo haikupi Muda wa kufungashiwa kwenye Sanduku/Mzigo lako/wako.

Hii ni Safari ambayo haikupi Muda wa kuwaomba msamaha uliowakosea.

Poleni sana Ndugu, Jamaa, Marafiki, pamoja na Watu wa karibu na Marehemu
Huu ni ukumbusho kua kila mmoja wetu atapitia njia hio. Hivyo tujiandae
 
nakumbuka hiyo kesi mkuu wa awamu ya 3 alimchukia na kumwekea mizengwe mingi sana ila huyu baba hakuterereka alibaki na msimamo huo hadi mauti yake. RIP Mzee Kisanga, umetangulia ukiwa unaamini ktk haki dhidi ya watawala. Mola akupumzishe ktk usingizi wa amani Amen.
 
jaji mkuu.jpg
 
Back
Top Bottom