TANZIA: George Tyson Afariki - Msiba mwingine Tasnia ya Filamu

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Ni msiba Mwingine tena umetokea yule Mwandishi na muandaaji mahili wa Filamu za Bongo George Otieno Okumu maarafu kama George Tyson aliyekuwa mume wa Monalisa amefariki Dunia kwa ajali ya Gari alipokuwa safari akitokea Dodoma Kuja Dar.


c7a360599c89f3c74309cc542d9db722_L.jpg


My Take:
Ndani ya Wiki mbili vimetokea vifo 3 vya hawa wasanii wa Filamu kulikoni? Kuambiana, Recho na sasa Gaorge Tyson.

=========
Wanabodi, Baada ya msiba wa producer Adam Kuambiana na baadae msaani Recho, leo gazeti la MWANANCHI 31/05/14 07:59 limetuma sms kuwa
MWANDAAJI WA FILAMU AFARIKI: Mkurugenzi wa filamu George Tyson amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Gairo akitokea Dodoma usiku wa kuamkia leo.

My Take.

Kwa maoni yangu, George Tyson ndiye the best local movies producer tuliyenaye so far.

Alikuwa ni Mume wa kwanza wa Msanii wa Bongo Movies Monalisa.

Poleni sana Bongo Movies.

Poleni wafiwa.

RIP George Tyson.

546321_501263163218696_213164398_n.jpg


George Tyson
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro.
Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.

Chanzo:bongomovie

Screen-Shot-2014-05-31-at-3.46.30-AM.png

Gari alilopata nalo ajali.
Screen-Shot-2014-05-31-at-3.46.12-AM.png

Salamu za rambirambi kutoka kwa celebrities wa Tanzania
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema mongozaji wa filamu maarufu nchini George Otieno Tyson (Pichani) amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Morogoro. Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha

The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu. Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.

Batuli: - Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director......Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu

Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. ...mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen.....R.I.P George Tyson.

Agness Masogange: R.I.P George Tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako!

Flaviana Matata : This is very sad aisee, Rest In Peace Tyson. Mungu kakupenda zaidi, - monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu

Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week... tunamzika mwenzetu mwingine... George Tyson.... Dah... Im just speechless.. RIP brother... Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee.... Pole dada akee ... Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya thembonishow .... Pigo
kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha tu jamani.

Aunty Ezekiel - Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director .....Nakosa lakusema

Mohamed Mwikongi : Hakika yametufika, A film director George Otieno Tyson naye hatunae tena duniani.

George Tyson aliwahi kuwa mume wa mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa naye mtoto mmoja. Mung ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.


Mwili wa marehemu George Tyson ukihamishwa toka Morogoro kuelekea Dar
View attachment 161740Msanii wa Bongo Fleva AY akiwa amewasili na crew yake nzima kuja kumpa pole Mbonie Masimba, AY alitoa laki 6 kununua jeneza la marehemu Tyson hii ikiwa kama mchango wake kwa kuthamini kile alichomfania wakati akiwa hai. Sasa msafara unaelekea Bongo na mwili utafikia Hospital ya Kairuki iliyopo Mikocheni na naambiwa msiba uko upo Bahari Beach nyumbani kwa marehemu.
View attachment 161741mwili ukitolewa mochwariView attachment 161742mwili ukiingizwa kwenye gariView attachment 161743ambwene na wenzake wakiwa kwenye mishi.

Taarifa ya jeshi la polisi kuhusiana na ajali
TUSIME.jpg


Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi.

Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo chake. Pia watu watano walipata maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa.

Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.
Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWONGOZAJI WA FILAMU, Mkazi wa mbezi DSM.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu.

Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-

1. NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2. GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3. NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4. JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI

Uchunguzi wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi.

Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo wa kasi.

Mazishi ya George Tyson
attachment.php


Hatimaye mwili wa aliywkuwa muongozaji filamu hapa nchini raia wa kenya George Tyson aliefariki majuma kazaa yaliopita hapa nchini na kusafirishwa kwao kwa mazishi.Hatimaye unazikwa saa hizi huko kijijini kwao.

attachment.php


attachment.php


attachment.php
 

Attachments

  • IMG_20140609_163937.JPG
    IMG_20140609_163937.JPG
    43.6 KB · Views: 1,003
kazi yake mora haina makosa atafanya atakalo atafanya awezalo dunia ni yake haina........
 
RIP George,nimeumia kwa kweli nakumbuka ile movie yao ya kwanza kabisa,nimeisahau jina
 
Muongozaji wa Filamu mahiri na aliekuwa mume wa muigizaji maarufu wa filamu Monalisa, George Tyson amefariki dunia usiku huu kutokana na ajali ya gari iliyotokea Kibaigwa akiwa njiani kurudi kwenda Dsm. Mwili wa marehemu George Tyson umefikishwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mkoa wa Morogoro.
 
Inna lillahi, mbona Majembe ndo yanaondoka?
Rest in peace bongo movie....!
 
SASA SIJUI NANI NI MKWELI!!! NIMEZUNGUMZA NA RAIS WA SHIRIKISHO ANASEMA GEORGE AMEFARIKI, JUSTIN BAYO ANASEMA GEORGE YUKO HAI NA WAKO WODINI!
Ngoja tusubiri taarifa zaidi
 
SASA SIJUI NANI NI MKWELI!!! NIMEZUNGUMZA NA RAIS WA SHIRIKISHO ANASEMA GEORGE AMEFARIKI, JUSTIN BAYO ANASEMA GEORGE YUKO HAI NA WAKO WODINI!
Ngoja tusubiri taarifa zaidi



Embu ngoja tusubirie hadi asubuhi tutajua ukweli
 
Ile movie inaitwa GIRLFRIEND,aiisee this is more than sad news pole monalisa,pole mtoto wake Sonia na sasa kifo kimewatenganisha rasmii mana mlishatengana.
RIP George,nimeumia kwa kweli nakumbuka ile movie yao ya kwanza kabisa,nimeisahau jina
 
Back
Top Bottom