Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
chama wakati mwingine tunapojadili masuala mazito ya kitaifa kama hili unatakiwa kuacha kuongea mambo ya kibwegebwege hapa.Dr. Masau alikuwa hatibu bure watanzania walilipa ada mbalimbali za tiba; kosa la mfanyibiashara la kutokuwa na mipango ya kibiashara inalaumiwa vipi serikali? Mkataba upo wazi hapakuwa na kipengele kinachomzuia mwenye jengo kunadi vifaa vya mpangaji iwapo atashindwa atalipa pango; Dr. Masau alitakiwa akope benki alipe deni lake huo ndio utaratibu wa kibiashara; haya mangine yote mnayopoteza muda wenu kuandika ni uzushi na udaku tu
Hospitali za serikali tunatibiwa kwa kulipia na hakuna huduma ya bure, hata zile huduma za bure zilizotangazwa kuwa zitakuwa bure kwa wazee na watoto wa umri wa chini ya miaka mitano hazipatikani bure.
Na hakuna mtu aliyesema kwamba alitakiwa atibu bure. Kinachoangaliwa hapa ni ule unafuu wa kupata tiba ama upasuaji wa magonjwa ya moyo hapa hapa nchini kwa gharama nafuu ukilinganisha na kama mtu angepelekwa India ambako wananchi wengi walikuwa hawawezi kwenda na hivyo wagonjwa wengi wa moyo wakaishia kufariki kwa sababu ya ufukara wao.
Lakini kuwepo kwa THI kulisaidia sana hata watu masikini waliweza kusafiri kutoka kona yoyote ya nchi ya Tanzania na kufika Dsm pale THI na kupata matibabu kwa gharama nafuu. Hapa JF tu wapo watu wanaoshuhudia namna ndugu zao walivyopata kutibiwa na hadi kupona pale THI na wanakiri kuwa kama sivyo basi ndugu zao wangeshaaga dunia siku nyingi.
Huo upuuzi wenu mnaofanya huko ccm na serikalini kila mtu kutaka share au 10% katika kila shughuli yoyote inayoanzishwa nchini uuache huko huko unapokuwa unajadili mambo makubwa kama haya. Kwakuwa mlizoea kujichotea mamilioni kwa kupeleka wagonjwa India ndio maana mkamuona Dr. Masau kuwa kitisho kwenu kwakuwa alikuwa amewanyima ulaji na hivyo mkaamua kumfanyia mizengwe. Watu wa ajabu sana nyie sijui ubinadamu wenu una tofauti gani na manyani.
Last edited by a moderator: