BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
Wewe kama una takwimu za kuonyesha kwamba nilichoandika si kweli kwa nini usiweke takwimu za kuonyesha kile nilichoandika si kweli!? Naona unabwabwaja bila kujua usemacho. Kutetea maslahi ya nchi yetu hata siku moja haiwezi kuonekana ni uhasidi/wivu kwa mtu mwenye akili timamu.
Kama kutetea maslahi ya nchi ni uhasidi basi hakukuwa na haja katika hiyo inayoitwa "mining act" iliyopitishwa hivi karibuni kuzuia usafirishaji wa Tanzanite ambazo hazijasafishwa ili kuliwewezesha Taifa lisafishe Tanzanite hizo nchini ama kwa kupitia wafanyabiasha ambao watakuwa tayari kusafisha Tanzanite. Hii itasaidia katika kuongeza ajira nchini na pia pato la Taifa kwanza kwa kupata kodi toka kwa watakaojiriwa katika makampuni ya usafishaji wa tanzanite na makampuni hayo pia kulipa kodi na wakati huo huo kuiuza Tanzanite ambayo imeshasafishwa katika nchi mbali mbali duniani kwa bei ya juu ukilinganisha na bei ya tanzanite ambayo haijasafishwa.

Wekeni takwimu hapa sio mazungumzo ya mitaani tu. Pia kumbuka kuna kitu kinaitwa value addition hao wanaopata zaidi wamechukua hii mali ghafi wakaifua vizuri na kuimarket inavyo stahili - kwa hiyo wanastahili faida kulingana na juhudi yao. Tatizo letu ni wivu na uhasidi - hivi ndio vinatufanya tulivyo !!