Tanzania's 100 most influential people

the issue is not being a hero or not! How much influence in whatever direction does one exert? We want the people top 100 people with the most most influence on the Country.

Hawa wakina Lissu sijui.. they are not there> They simply dont command a large enough segment of public opnion, they are not business leaders katika Tanzanian industry, no political or other high national office, no academic works of great acclaim.. hayupo huyu. Shivji i can vouch, Slaa maybe..... lakini this is really high caliber...plz msijemkasema invisible or mkkj lol (sorry guys imebidi muwe mfano kidogo: ndio ujamaa wenyewe huo :p jokes)
 
Kuna Jamaa mmoja anaitwa Shariff aliwahi kuwa balozi kama sikosei UK na halafu akawa Waziri mdogo wa mambo ya nje awamu ya tatu. Huyu alipokuwa Balozi UK Watanzania wanaoishi nchi mbali mbali za nje walimpenda sana alikuwa mstari wa mbele katika kutatua matatizo yao mbali mbali ikiwamo wale ambao hawajapatiwa posho zao toka Tanzania au waliokuwa na matatizo ya hati za kusafiria. Hata alipokuwa waziri mdogo mambo ya nje kila nafasi ilipomruhusu alikuwa anatoa michango yake mbali mbali au ufafanuzi katika maswala ya Kitaifa na Kimataifa. Bahati mbaya sidhani kama Tanzania alifahamika sana kama alivyofahamika na Watanzania waishia nje. Alikuwa ni mtendaji mzuri sana na nashangaa sasa hivi simsikii kabisa, labda hakumuunga mkono mkuu wakati wa kinyang'anyiro cha 2005. Sidhani kama ameshafikisha umri wa kustaafu.
 
Kuna Jamaa mmoja anaitwa Shariff aliwahi kuwa balozi kama sikosei UK na halafu akawa Waziri mdogo wa mambo ya nje awamu ya tatu.

Unamzungumzia Dk. Abdukadeer Shariff aliyekuwa Naibu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. Huyu bwana aliposhindwa kura za maoni za kugombea Ubunge, aliamua kuachana na siasa, hivyo akasema anataka sasa kupumzika kwa kazi za kuongoza jamii.
 
mi nadhani hii idea ni nzuri lakini tatizo lazima tuwe na vigezo vinginevyo watu kama SHIGOGO, WEMA SEPETU,LIYUMBA NA WENGINEO WASIKUWA NA MILENGO INAYOELEWEKA NAO WATAINGIA KWA SABABU NAO NI MAARUFU KWENYE MAMBO YAO
 
Sawa kabisa Mfumwa, Kama kuna watu wanastahili kupewa ubunge wa kuteuliwa basi huyu bwana alistahili maana utendaji wake ulikuwa ni mzuri mno. I wish we had more dedicated leaders like him.
 
I agree with you kwamba hoja ni nzuri lakini nadhani mleta mada hakufanya utafiti wa kutosha wa kuweza kujua ni vigezo gani vitakavyoongoza hoja. Huu ni mfano wa shoddy work, ninamshauri mtoa mada afikirie vigezo vitavyoweza kuifanya hoja yake iweze kuwa hai.
 
Bubu ataka Kusema,
Mkuu cheza utakavyo cheza UKWELI ni kwamba the most Enfluencial people are our Leader na ktk list yote asilimia 90 ni MAFISADI... That is Tanzania ya leo na kila tunapojaribu kutazama nje ya hapo ni kujidanganya wenyewe ktk kuzidi kujenga taifa la Wadanganyika..siku zote sisi hujaribu kuufumbia macho Ukweli!..
 
I agree with you kwamba hoja ni nzuri lakini nadhani mleta mada hakufanya utafiti wa kutosha wa kuweza kujua ni vigezo gani vitakavyoongoza hoja. Huu ni mfano wa shoddy work, ninamshauri mtoa mada afikirie vigezo vitavyoweza kuifanya hoja yake iweze kuwa hai.

Huu ni mtazamo wako maana nimefafanua vizuri kabisa na kutoa mifano kama ya akina Michael Jordan, Oprah Winfrey na Magic Johnson. Mtu ambaye anaweza kuwa influential kwenye jamii yoyote anaweza kuwa anatoka katika nyanja yoyote ile katika jamii lakini katika umaarufu wake alioupata katika nyanja hiyo anaweza kabisa kuutumia umaarufu huo katika nyanja nyingine na nikatoa mfano wa Oprah pamoja na kuwa siyo mwanasiasa alikuwa wa mwanzo mwanzo kabisa katika kumsupport Obama pamoja na kuwa hajawai kufanya hivyo huko miaka ya nyuma. Watu walioelewa, wanachangia majina ya watu wanaodhani wanastahili kuwemo kwenye list hiyo, wewe unayeiona hoja hii haina uhai kaa pembeni tuachie sisi tuendelee nayo.

http://findarticles.com/p/articles/mi_m1077/is_7_59/ai_n6040997/
 
mi nadhani hii idea ni nzuri lakini tatizo lazima tuwe na vigezo vinginevyo watu kama SHIGOGO, WEMA SEPETU,LIYUMBA NA WENGINEO WASIKUWA NA MILENGO INAYOELEWEKA NAO WATAINGIA KWA SABABU NAO NI MAARUFU KWENYE MAMBO YAO

Liyumba naye ni mtu influential kwenye jamii ya Watanzania? Kwa lipi? Siku zote nilidhani mtu influential ni yule ambaye analeta positive impact kwenye jamii hiyo. Sasa Liyumba ana posiibe impact ipi katika jamii ya Kitanzania!?
 
Sawa kabisa Mfumwa, Kama kuna watu wanastahili kupewa ubunge wa kuteuliwa basi huyu bwana alistahili maana utendaji wake ulikuwa ni mzuri mno. I wish we had more dedicated leaders like him.

Haya si maajabu mengine! Mtu aliyekuwa na utendaji mzuri mno anakosa kura za maoni!
 
Haya si maajabu mengine! Mtu aliyekuwa na utendaji mzuri mno anakosa kura za maoni!

Labda kuwa kwake nje ya nchi kwa miaka mingi kulimuathiri, au wakubwa walimuwekea "kauzibe." maana kuna wengi tu waliopewa ubunge wa kuteuliwa pamoja na kuwa hawakustahili nafasi hiyo.
 
Ok, kama tunatakiwa kuwataja walio hai tu then,

YESU

Kila kona yupo, kila sehemu anatajwa.....
 
Huu ni mtazamo wako maana nimefafanua vizuri kabisa na kutoa mifano kama ya akina Michael Jordan, Oprah Winfrey na Magic Johnson. Mtu ambaye anaweza kuwa influential kwenye jamii yoyote anaweza kuwa anatoka katika nyanja yoyote ile katika jamii lakini katika umaarufu wake alioupata katika nyanja hiyo anaweza kabisa kuutumia umaarufu huo katika nyanja nyingine na nikatoa mfano wa Oprah pamoja na kuwa siyo mwanasiasa alikuwa wa mwanzo mwanzo kabisa katika kumsupport Obama pamoja na kuwa hajawai kufanya hivyo huko miaka ya nyuma. Watu walioelewa, wanachangia majina ya watu wanaodhani wanastahili kuwemo kwenye list hiyo, wewe unayeiona hoja hii haina uhai kaa pembeni tuachie sisi tuendelee nayo.

100+ Most Influential Black Americans | Ebony | Find Articles at BNET

Pamoja na maelezo yako mazuri lakini hayajabadilisha hoja yangu. Ninachokushauri ni kuwa hoja yako ni mfu na ninasema sio kwa nia mbaya, la hasha hoja ni nzuri lakini haina vigezo vinavyoiweka hoja hai.
 
Ok, kama tunatakiwa kuwataja walio hai tu then,

YESU

Kila kona yupo, kila sehemu anatajwa.....

Na shetani pia ndugu yangu...Ama umeshasahau mbinde mbinde za albino na waganga wa kienyeji? Vipi kuhusu unga unga wa bungeni?
 
Most Influential people

1.Viongozi wa Kidini
2.Viongozi wa Kisiasa
3.Wastaafu
4.Wafanyabiashara wakubwa

Ninaowafahamu kuwa ni Influential

1.Kawawa
2.Malecela
3.Kisumo
4.Msuya
5.Dr.Mahiga
6.Mzindakaya
7.Kingunge
8.Barongos
9.Rwegasiras
10.Mwinyi (Rais mstaafu)
11.Rostam
12.Mwapachus
13.Sheikh Mkuu
14.Kardinali Pengo
15.Mengi
16.Raza
17.Dr. Gharib Bilal
18.Rupia
19.Marealle
20.George Kahama
21.Retired Generals
22.Salim Ahmed Salim
23.
 
Pamoja na maelezo yako mazuri lakini hayajabadilisha hoja yangu. Ninachokushauri ni kuwa hoja yako ni mfu na ninasema sio kwa nia mbaya, la hasha hoja ni nzuri lakini haina vigezo vinavyoiweka hoja hai.

Na mimi nimekwambia wengine wanaiona siyo mfu na wameweka majina mbali mbali. Wewe unayoiona ni mfu tafuta thread nyingine yenye uhai. Kwani umelazimishwa kurudi kwenye thread ambayo ni mfu!? :confused:
 
- Msiwasahau wakulu wa Ze-Utamu, na wazee wa JF Kumkoma nyani, au?.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

Wa Utamu...Hmmm!!! nadhani wale wanachukiwa sana na siku wakijulikana basi watapata kipigo ambacho si cha kawaida, lakini wa JF naam pamoja na wengi kutumia majina bandia lakini baadhi yao michango yao inawafumbua macho Watanzania kwenye mambo mbali mbali ndani na nje ya nchi yetu.
 
Na mimi nimekwambia wengine wanaiona siyo mfu na wameweka majina mbali mbali. Wewe unayoiona ni mfu tafuta thread nyingine yenye uhai. Kwani umelazimishwa kurudi kwenye thread ambayo ni mfu!? :confused:

Samahani mkuu,
Nilichokuwa ninafanya ni kukosoa kwa maana ya kuleta changamoto ya kuboresha mada, kama hukosoleki mzee, pole kwa kukukwaza.

Ujumbe wa leo
"If you believe you are born with all the smarts and
gifts you'll ever have, you tend to approach life with a
fixed mind-set. However, those who believe that their
abilities can expand over time live with a growth
mind-set-and they're much more innovative."

- Dr. Marshall Goldsmith
 
Bila samahani Mkuu, Kama unavyoona watu wengine wanaelewa na nimetoa mifano rahisi kabisa inayoeleweka kwamba watu influential kwenye jamii wanaweza kutokea katika nyanja mbali mbali zikiwemo siasa, elimu, michezo, dini, burudani n.k. Sasa ni kipi ambacho hukukielewa katika ufafanuzi wangu!? Kama unaona ufafanuzi wangu una walakini kuhusiana thread hii basi anzisha nyingine ambayo utaweka katika namna ambavyo unataka wewe na bado watu tutachangia ndiyo uzuri wa JF. Hapana, mimi kama binadamu siko perfect na huwa nakubali makosa na kukosolewa pia hata hapa ukumbini nimeshawahi kuwaomba samahani watu wengi tu niliowakosea tena hadharani lakini kwenye hii thread sioni kama kuna matatizo yoyote.
 
Back
Top Bottom