Tanzanian Lodge Named Best Hotel in The World

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Tanzanian Lodge Named Best Hotel in The World

singita.jpg

Singita Game Reserves

After receiving a score of 98.44 out of 100 on a list based on reader surveys, Travel + Leisure, named Singita Grumeti Reserves in Tanzania's Serengeti National Park as the best hotel in the world.

The hotel, singita.com, which is made up of two lodges and a tent camp, offers unparalleled luxury in the thick of the wild.

It is located on the migratory route traversed annually by more than a million wildebeest, providing guests with incredible photo opportunities from their bedroom windows.

Despite its remote location, Singita's guests are treated to five-star service and accommodations.

Rooms in the tents and villas start at around $1,095 per person per night; rates include daily game drives, food, and drink.

Two other Tanzanian hotels, Kirawira Luxury Tented Camp and -Serengeti Migration Camp all located in the Serengeti National Park, scored 96.71 and 96.50 respectively to make it in the top ten.

source: businessinsider
 
The question is: watanzania/bantus wanaruhusiwa kuingia hapo hotelini? Manake nasikia kuna baadhi ya hotels Zanzibar na bara kama wewe ni mweusi huingii!!....what a shame wananchi wananyanyaswa ktk nchi yao!!
 
Kingereza changu hafifu naomba kueleweshwa kidogo,
je hii hoteli ni ya mtanzania au iko tanzania tu?
 
Kingereza changu hafifu naomba kueleweshwa kidogo,
je hii hoteli ni ya mtanzania au iko tanzania tu?

Sio vibaya kuuliza, hii ni hoteli ya mkoloni kutoka USA, mbali na hii hoteli anamiliki eneo kubwa tu la ardhi lenye idadi kubwa ya wanyama ( kwa maneno yan,,anamiliki serengeti ndogo ndani ya serengeti) japo eneo lake lipo nje ya mipaka ya hii mbuga.

Yuko mbioni kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa, ili wateja wake wawe wanatua moja kwa moja huko. Wateja wake ni watu matajiri na watu maarufu duniani, kwa usiku moja kodi ya pango ni zaidi ya dola 1600 za kimarekani,, mbali na kuwaajiri watanganyika wachache hoteli haina any tangible economic impact kwa jamii zinazozunguka hili eneo, wanaishi kwenye ufukara wa hali ya juu, barabara unayosikia inapigiwa kelele na wanaotutawala wetu ni ili hizi facility zifikiwe kwa uharaka na ufupi
 
It is best not only because of the hospitality but read below.........
..........It is located on the migratory route traversed annually by more than a million wildebeest, providing guests with incredible photo opportunities from their bedroom windows.......

Its location add a value. sijui hapo watetezi wa wanyama pori wanasemaje.

Hongera zaaoooooooooooo
 
Sio vibaya kuuliza, hii ni hoteli ya mkoloni kutoka USA, mbali na hii hoteli anamiliki eneo kubwa tu la ardhi lenye idadi kubwa ya wanyama ( kwa maneno yan,,anamiliki serengeti ndogo ndani ya serengeti) japo eneo lake lipo nje ya mipaka ya hii mbuga.

Yuko mbioni kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa, ili wateja wake wawe wanatua moja kwa moja huko. Wateja wake ni watu matajiri na watu maarufu duniani, kwa usiku moja kodi ya pango ni zaidi ya dola 1600 za kimarekani,, mbali na kuwaajiri watanganyika wachache hoteli haina any tangible economic impact kwa jamii zinazozunguka hili eneo, wanaishi kwenye ufukara wa hali ya juu, barabara unayosikia inapigiwa kelele na wanaotutawala wetu ni ili hizi facility zifikiwe kwa uharaka na ufupi

Kulikuwa na sababu gani za msingi za kusiktisha ujenzi wa barabara toka Arusha hadi Musoma?
 
Zipo hotel nyingi tu za aina hiyo bana,!!!ila zio za wazawa na sidhani kama wanalipa kodi sidhani!!!hata maji wanatoka nayo kwao.......vijana wa kitz tu ndio attendant wa kawaida sana vyeo vya juu ni wakenya!na wakoloni
 
Hii hoteli inamilikiwa na Mmarekani mmoja millionaire anaitwa Tudor. Ndiye aliyepanga ile ziara ya rais Kikwete mwaka 2007 kwenye Wall Street New York. Na kila mara rais Kikwete akiwa maeneo ya Serengeti hupotelea huko. Sina hakika kama Mtanzania wa kawaida anakaribishwa pale, na hata kama wanakaribishwa, labda ni genge la akina Lowassa, Chenge, Rostum, ndio wanaoweza kumudu gharama za hoteli hiyo. Bill Gates alikuwepo huko karibuni. Niliwahi kuweka picha zake kweney Jamii Photos. Mnaweza ku-peruse na kuiona hoteli yenyewe. Ukiniuliza Tanzania inafaidikaje na "uwekezaji" wa aina hii kwa hakika jibu langu ni sijui.
 
barabara unayosikia inapigiwa kelele na wanaotutawala wetu ni ili hizi facility zifikiwe kwa uharaka na ufupi
Alaaaaa! Nimepata picha sasa kwa nini Serikali yetu inang'ang'ania hii barabara, pamoja na kupigiwa kelele na UNESCO, kumbe ni maelekezo toka kwa wawekezaji (ie wakwapuaji wa rasilimali zetu)!
 
Kwa kweli hii lodge ni master piece. Ila kwa mtazamo wangu hii siyo property ambayo mtanzania anaweza kujivunia nayo. Tunaweza kusema nchi inanufaika kwa mapato kutokana na park fees (kuna wakati huko nyuma kulikuwa na mpango wa kuwatoza wageni wanaokaa kwenye lodge hiyo extra park fees kama USD 500 kwa mtu kwa siku baadala ya USD 50 kwa mtu kwa siku), vinginevyo mimi nakerwa sana kuona mbuga zetu mashuhuri zimetekwa na hao wawekezaji kutoka nje. Kwa mfano, hakuna hata lodge moja ambayo iko kwenye National Park zetu inayomilikiwa na mzawa. Zote ni za hao wazungu, wahindi kupitia Agakhan Foundation na wahindi wengine kutoka Kenya. Kuna zile ambazo serikali ilishindwa kuziendesha nazo ni Lake Manyara National Park, Ngorongoro Wildlife Lodge, Seronera Wildlife Lodge na Lobo WildlifeLodge. Hizi zote ziliuzwa kwa mhindi mmoja anaeitwa Kotak wa GAPCO.! Tatizo kubwa la kiuchumi hapa kwetu ni hiki kisingizio cha Globalization (Ukoloni Mamboleo). Tanzania kuna watu serious ambao wangeweza kuzi run hizo hoteli kama wangewezeshwa kifedha, lakini umasikini wetu unatuhukumu na hizi Funding Institutions au mabenki yaliyozagaa hapa nchini hayana shughuli na watanzania hasa wazawa. Mikopo watapewa watu wenye pesa tu, sisi tutabakia kuwa washangiliaji siku zote tukiona hivi hivi urithi wa maliasili yetu ukibakwa kila kukicha na hao manyan'gau wa nje wakishirikiana na mafisadi wachache kwenye wizara mbali mbali.
 
Wanaruhusu wanafunzi chini ya uangalizi maalum kuitembela hiyo lodge. Kuna nyingine inaitwa Lobo iko huko machakani nayo ni nzuri sana.

Pia kuna rates za mtz mweusi, bt still ni expensive. I am somehow proud kuwa wawekezaji wanavumisha jina la tz vizuri.
 
Kwa kweli hii lodge ni master piece. Ila kwa mtazamo wangu hii siyo property ambayo mtanzania anaweza kujivunia nayo. Tunaweza kusema nchi inanufaika kwa mapato kutokana na park fees (kuna wakati huko nyuma kulikuwa na mpango wa kuwatoza wageni wanaokaa kwenye lodge hiyo extra park fees kama USD 500 kwa mtu kwa siku baadala ya USD 50 kwa mtu kwa siku), vinginevyo mimi nakerwa sana kuona mbuga zetu mashuhuri zimetekwa na hao wawekezaji kutoka nje. Kwa mfano, hakuna hata lodge moja ambayo iko kwenye National Park zetu inayomilikiwa na mzawa. Zote ni za hao wazungu, wahindi kupitia Agakhan Foundation na wahindi wengine kutoka Kenya. Kuna zile ambazo serikali ilishindwa kuziendesha nazo ni Lake Manyara National Park, Ngorongoro Wildlife Lodge, Seronera Wildlife Lodge na Lobo WildlifeLodge. Hizi zote ziliuzwa kwa mhindi mmoja anaeitwa Kotak wa GAPCO.! Tatizo kubwa la kiuchumi hapa kwetu ni hiki kisingizio cha Globalization (Ukoloni Mamboleo). Tanzania kuna watu serious ambao wangeweza kuzi run hizo hoteli kama wangewezeshwa kifedha, lakini umasikini wetu unatuhukumu na hizi Funding Institutions au mabenki yaliyozagaa hapa nchini hayana shughuli na watanzania hasa wazawa. Mikopo watapewa watu wenye pesa tu, sisi tutabakia kuwa washangiliaji siku zote tukiona hivi hivi urithi wa maliasili yetu ukibakwa kila kukicha na hao manyan'gau wa nje wakishirikiana na mafisadi wachache kwenye wizara mbali mbali.
Inasikitisha sana matunda ya taifa letu wanakula wageni, tena kwa msaada wa Watanzania wenzetu viongozi
 
Cha kusikitisha zaidi, siku hizi ukitaka kufanya booking katika baadhi ya hizo lodge inabidi utume booking kwenye ofisi zao zilizopo nje ya nchi! Na pia hizo hoteli au lodges hua zinapokea bookings kutoka nje ya nchi! Tour Operators wa nje huwa wanalipa kwenye benki zilizoko kwao kabla watalii hawajaja kwetu, hivyo basi hatutaweza kamwe kujua idadi ya wageni waliolala kwenye hizo properties au nchi imefaidika na nini kiuchumi, tumekwisha!
 
Back
Top Bottom