Tanzania YETU: Je, ni jamii ya vilaza na viongozi wa Kiimla na Ukurupukaji?

“Exploration estimates indicate the country has about 53.9 million pounds of uranium oxide (U3O8) deposits that, at current prices of $41 per pound, is worth $2.2 billion.
Mantra, which will mine uranium in the south of the country at Namtumbo district, Ruvuma region, expects to produce 3.7 million pounds per year worth $151.7 million, using a 1,500 strong workforce and an investment of about $400 million, according to its website.”
Source: THE EAST AFRICAN PAPER APRIL 2010
MY TAKE
Jana via TBC news hawa jamaa wa Mantrac wamesema huo mgodi ni wa 7 duniani na ni wa 3 Afrika.
Yaani kidunia tumeizidi USA na kiafrika ata South Afika iko nyuma yetu iyo inaonyesha ukumbwa wa Mgodi na wakaupamba kwa kusema ni world class.
Kama ayo madini yana thamani ya $ 2.2 billion gawio la serikali apo ni ngapi?
Je iyo uranium itatumika kufanya nini?Kudhalisha umeme,makombora au ndo export?
Katika malengo ya Mantrac suala la kuzalisha umeme kwa GRID ya taifa halipo see www.mantraresources.com.au/upload/documents “ ila watazalisha kwa matumizi ya maeneo husika.
Kama ni kuzalisha umeme mbona ata haimo kwenye projects ambazo TANESCO wanazo as per their website.Wakati am sure iyo URANIUM ingeweza cover SADC countries pia.
Katika hili ELIMU BURE(MSINGI NA SECONDARY ) NA AFYA BURE NA UMEME WA UHAKIKA TANZANIA VINAWEZEKANA.
Let us be carefull on this ili tusije boronga when it comes to MCHUCHUMA AND LIGANGA WITH IRON ORE AND COAL.
My plea to concerned parties: I know for Uranium some negotiations are still underway please serve the nation interest for the existing and future generations.
NB:ALAFU UDONGO WA TANI 20 UMEPELEKWA SOUTH KAMA SAMPLE KAAAAAAZI KWELI KWELI.
 
i hope watalipa ile 30% corporate tax +other taxes + royalty fee na kutoa kazi na mishahara mizuri,medical etc kwa hao watu 1500 watakaoajiriwa,to me wakifanya hivyo ni sawa almost half kinachotoka migodini kinabaki nchini,acha wachukue nusu nyingine maana wao ndo wanachukua risk yote na ukumbuke nao ni wafanyabiashara wapo pale to make something....swala nuclear power kwa TZ naomba usahau kwa sasa.
 
Kwa uelewa wangu...Uranium itachibwa mpaka kwenye kiwango cha sample..then baada ya hapo inakuwa transported kwenda kwa mmarekani..as wanaseme ikifika kwenye processs level...kuna mawili yanaweza toke either utumie kwa kutengeneza nyuklia ambayo inachavusha umeme au kwa ajili ya mabomu....So kama ni umeme bora wao watufanyie kila kitu kwa maelezo yao...Huo mkataba unasema hivyo.

Kufaidika kwa watanzania labda tuongelee kwa ujumla watanzania wote na hapo ni hoja ndefu sana...labda tufanye ni kiwango gani kiangia katika mzunguko wa pato la taifa...ambayo ni mrahaba...kama bwana koba alivyo sema ....30% Corporate tax.
Ila kwa mtizamo wangu...kama tanzania ingekuwa na hisa kwenye hii sector would have been benefic big time kwa kwa kweli.
 
serikali itachukua kodi ambayo ni dola mil 500 kwa muda wa miaka 12 kwa hiyo gawanya kwa 12 upate kwa mwaka ni dola milioni ngapi ndio serikali itaambulia kutokana na hiyo uranium kwa mwaka.
 
Jamani wana JF naombeni mawazo yenu....hii nchi yetu inaelekea wapi jamani?
Mafisadi wakutosha,maendeleo hakuna.......na sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua kiongozi atakayeongoza hii nchi,naona kama vile mwezi wa 10 kunaweza kukatokea machafuko(siombei),kwa sababu CCM wameshajihakikishia ushindi...this means that wakishindwa wanaweza wakatumia means ya aina yoyote ili waingie madarakani....!
mnaionaje hii kitu?!
 
Kwa mtu yeyote makini anayefuatilia mwenendo wa mambo yanavyoendelea katika ngazi mbali mbali za utawala wa nchi hii kuanzia serikali za mitaa mpaka Ikulu atakubaliana na mimi kuwa kwa miaka ya hivi karibuni kuna nyakati viongozi wamekuwa wakitoa matamko yanayotofautiana kana kwamba wanatoka serikali tofauti. Si jambo la kushangaza kumsikia Waziri akitoa tamko leo kuhusu jambo Fulani kIsha muda mfupi baadaye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hiyo akatoa tamko tofauti kwa suala hilo hilo. Si jambo la kushangaza pia kusikia Ikulu ikitoa tamko linalopingana kabisa kimtazamo na tamko lilitolewa na Wizara Fulani awali na wananchi wakaachwa hivi hivi bila kuelezwa tamko lipi ni sahihi.

Inavyoonekana sasa tatizo hili linaendelea kuhitimu vidato. Tumeshuhudia hivi karibuni Watawala wakijitapa mbele ya wananchi kwa juhudi zao za kupambana na ufisadi ukiwemo ule wa matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa rasilimali za umma. Watawala wametutaka tuamini kuwa safari hii wako makini na kwamba vyombo vinavyohusika vimepewa uwezo wa kuwashughulikia watuhumiwa ikiwemo kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Tumeona na kusikia matamko ya wanasiasa ambao pia ndio watawala wetu wakitueleza kuwa Fulani hatukumpitisha kugombea nafasi Fulani kwa kuwa tumeridhika kuwa alikiuka maadili ya chama chetu ikwemo kutoa rushwa kwa wapiga kura!!!!

Sinema inaanza kushangaza pale Watawala hao hao wanapopanda kwenye jukwaa la siasa na kumpigia debe mtuhumiwa aliyefikishwa mahakamani (na shauri lake bado liko mahakamani) na kututaka sisi wananchi tumchague kwa kuwa ati ni muadilifu na mchapa kazi hodari. Hebu tujaribu kumfikiria mpelelezi anayechunguza kesi kama hii na Hakimu anayesikiliza kesi hii!! Hivi kweli kwa hali ya kawaida (hasa ukizingatia kuwa aidha yeye au kiongozi wake ni Mteule wa Huyu Mtawala) atakuwa na ujasiri wa kuchimba undani wa shauri hili kwa maslahi ya umma ulioporwa kifisadi au ataandaa mashitaka ambayo yatamfanya Mtuhumiwa kushinda shauri lake hata kabla ya hukumu kutolewa? Akili ya kawaida kabisa itakuonyesha kuwa katika mazingira kama haya ni nadra sana kwa haki kutendeka. Katika hali ya kawaida, kama mahakama ikimtia hatiani mtuhumiwa ni sawa na kumuumbua Mtawala ambaye ndiye aliyewateua wao (Majaji na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Hatutaki kuamini kuwa Watawala wetu hawana washauri wanaofaa. Aidha hatutaki kuamini pia kwamba watawala wetu ni wakaidi na hawataki kusikiliza ushauri wa washauri wao kama wapo!!! Hatutaki kuamini pia kuwa Washauri wanafanya kazi ya kuwasifia watawala hata pale wanapokosea. Hali hii haikubaliki kwa vyovyote vile

Maswali ya kujiuliza sisi sote hapa ni haya –
· Tunaelekea wapi kama taifa?
· Hivi maadili ya uongozi bado yapo?
· Kama yapo, vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa maadili vinafanya nini?

Natoa rai kwa wale wote tuanoitakia mema nchi yetu kupaza sauti na kuwaambia Watawala Wetu ukweli ili wapone!!! Tukiendelea kuwashangilia, kuwatandikia khanga wanapopita kwenye maeneo yetu (ili wasikanyage vumbi) na kuwafurahisha ili kuimarisha tabasamu kwenye nyuso zao itakuwa sawa na kuandaa matanga yetu na ya watoto wetu tukingali hai. Kwa hali ilivyo sasa ni sawa na ile hadithi ya Mfalme aliyekuwa akitembea uchi na watu wakimsifia kuwa suti aliyovaa imempendeza kweli kweli. Tuchukue hatua na kusema Mfalme uko uchi ili afiche aibu ya uchi wake na kulinda hadhi ya Taifa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA IPONE!!!
 
hata slaa huwa anatofautiana na chadema. lakini pia alitofautiana na akina david kafulila akatumia manguvu kwa na fasi yake chadema na kuwafukuza washikaji. kidogo tu nadhani alikuwa amfukuze na zito lakini akaogopa chadema kupoteza mwelekeo kabisa kwa jamii.
 
Tumepewa Fursa, Tuikomboe Nchi Yetu

Mungu, atukuzwe leo na siku zote, ameiumba Dunia na kuipa asili endelevu ya kuwahukumu watu wasiozitumia fursa. Hata katika katika mpira ukiona unakosa magoli ya wazi, basi ujue hiyo mechi utafungwa na utajilaumu. Hata katika kilimo ukiona mvua zinanyesha halafu wewe unacheza bao ujue utaikumbuka fursa hiyo na kujutia. Mwingine ameajiriwa ana mshahara mkubwa, hiyo ni fursa ya kujijenga usipoitumia utakumbuka na kujutia. Kwa ujumla ni katika kila jambo usipoitumia fursa unajitengenezea laana. Ndivyo Mungu alivyoiumba Dunia.

Ukweli ni kwamba kinachotusumbua watanzania au kinachoisumbua Tanzania ni laana. Ni vigumu kuifafanua hoja hii. Lakini nitajitahidi kuweka wazi ili ieleweke. Ugonjwa hujulikana kwa dalili. Hata laana hujulikana kwa dalili. Kwa nchi yetu nitataja dalili chache zinazoweza kuthibitisha kuwa ni laana inayotusumbua.

Dalili ya Kwanza, tuna rasilimali nyingi za utajiri katika dunia hii, mfano madini ya tanzanite hayapatikani popote Duniani, Kuna mbuga za wanyama kama Serengeti ambazo ni za kipekee, utajiri wa Tanzania utajaza vitabu kuutaja, lakini sisi ni kati nchi maskini zaidi Duniani na wajanja wanavuna raslimali hizo huku wakituachia migogoro ya kisiasa na kijamii.

Dalili ya pili, tuna jiografia ya kutegemewa ukanda wa kati na nchi nyingi za kiafrika ukiacha Mito mikubwa na Maziwa, lakini pia tunapaka na bahari ya hindi, na hivyo kuwa na uwezo wa kuwa na bandari kubwa Afrika inayotegemewa na nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Congo drc, Zambia nk huku reli ikitoa mizigo bandarini, lakini cha ajabu ni kuwa Bandarini kutoa mzigo ni kero na usumbufu unaochukua muda mrefu na kukatisha tamaa, bandari ni ya kirasimu huku reli ikiwa imekufa kifo cha mende.

Dalili ya tatu, ni mbuga ya Serengeti, hii imewekwa kuwa ajabu ya saba ya Dunia kutokana na mfumo wa kuhama kwa wanyama wakiwa katika mamilioni, aina kwa aina, makundi kwa makundi, yenye kuvutia na kustaajabisha, isiyokuwepo sehemu yoyote Duniani, huku mfumo wa ecosystem ukionekana dhahiri. Serikali inataka kujenga barabara ya lami inayopita karibu na hoteli zinazomilikiwa na vigogo wa serikali katikati ya mbuga hii, kwenye njia zinazotumiwa na wanyama wanapohama, hili ni janga. Ni sehemu ngapi hazina barabara Tanzania. Kwanini hapa. Tena kama ni lazima serikali ingeweza kujenga barabara tena kwa gharama nafuu zaidi na umbali mfupi zaidi nje ya mbuga kwenda sehemu hizo hizo. Wazungu wanatushangaa sana.

Nenda kwenye
www.savetheserengeti.org utaona kwa undani. Ni wazi kuwa mbuga ya Serengeti itapotea katika ramani ya Dunia. Hii pia siyo hujuma, bali ni laana. Kuna dalili nyingi saana za kuthibitisha laana tuliyonayo kama nchi. Laana tuliyoitengeneza wenyewe miaka mitano iliyopita.


Tuone sasa chanzo cha laana hii. Mungu, atukuzwe leo na siku zote, alipoiumba Dunia aliibariki kila sehemu kwa namna yake, kuna wenye utajiri wa mafuta, kuna wenye utajiri wa mazao ya kilimo, maliasili, kuna wenye viwanda, teknolojia n.k, lakini ujue Baraka hizi zote ni fursa, usipozilinda unalaaniwa. Unaweza usiamini kuwa wanyama wa Tanzania wanasafirishwa na kwenda kuanzisha mbuga Ulaya. Sisi tulikuwa na fursa ya kuzilinda, miaka mitano iliyopita. Tumejutia. Fursa itakuja tena 31October2010.

Maana, kumbuka, na usipoitumia fursa kama tulivyoona unalaaniwa. Na mkishalaaniwa, kama nchi mnakuwa nchi isiyo na maendeleo, na utajiri mlionao unafaidiwa na mataifa ya nje, tena kila neema kwenu inakuwa ni kero ya kuongelewa na kuandikwa magazetini bila muafaka.

Viongozi wenu wanazidi kuwa vibaraka na ardhi yenu inaporwa na wageni, vibaraka hao wanaibadili sheria wanavyotaka na kwa manufaa yao na familia zao na rafiki zao, mnakuwa watu wa kulalamika siku zote, rasilimali kidogo mnazovuna viongozi wenu wanazitumia kwa mambo yasiyo na maana kama vile safari za nje, posho, anasa, fahari na hatimaye kampeni huku hospitali zikikosa madawa, mishahara duni na miundombinu mibovu, mnakamuliwa kodi katika kila nyanja, huku vibaraka na kampuni zao wakikwepa kodi hiyo.

Tena mkishakulaaniwa, Maliasili zenu zinaporwa na vibaraka mliowachagua wakihalalisha uporaji na kuwabariki waporaji, ambao ndio wamewaweka madarakani kwa gharama zao. Maana ujue Tanzania haina uwezo wa kugharamia kampeni ghali, za kifujaji, kama zinazofanywa na chama tawala. Fedha hizo zinatoka kwa wanaopora rasilimali zetu. Hoteli, viwanja vya ndege na barabara za lami zinajengwa kwenye mbuga za wanyama walizopewa wageni ili kuwarahisishia uporaji wakijua wana muda mchache kabla ya kuwaachia wenzao.

Laana hiyo inasababishwa na kushindwa kutumia fursa ya kuikomboa nchi yetu kupitia sanduku la kura. Ni laana tuliyoipata miaka mitano iliyopita. Ila Mungu, atukuzwe leo na siku zote, ametupa fursa nyingine tarehe 31October2010. Ni juu yetu kuchagua laana au Baraka.

Wafanyakazi, Wakulima, Wafanyabiashara na Wajasiriamali, Mafundi seremala, Walimu na Wanafunzi, Polisi na Wanajeshi, Wanausalama wa taifa, Mashehe na Wachungaji, soote tupige kura kwa lengo la kuikomboa nchi yetu, kwa faida yetu na vizazi vijavyo. Hata kama tunawajibika kwa utawala huo, basi siku ya kupiga kura, tuusaliti na kuutosa utawala dhalimu, utawala wa vibaraka. Hiyo ni kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

Tupige kura kwa nia ya kuwachagua watu wenye Wito, Sifa na Uwezo wa Kuongoza kwa lengo la kuikomboa nchi. Tupige kura kwa lengo la kuikomboa nchi. Tuepuke kuwachagua vibaraka wa wezi wanaopora utajiri wa nchi yetu, na kubadili sheria kwa manufaa yao na rafiki zao na familia zao.

Shida tunazopata leo ni laana tuliyoichagua miaka mitano iliyopita, maana hatukupiga kura kwa haki, hatukuitumia fursa kuikomboa nchi yetu, tulipiga kura kwa ushabiki, kwa kupewa rushwa ya ahadi za uwongo, fulana na kofia, tukawachagua mafisadi na vibaraka wao, tena kwa kishindo. Hiyo ndio laana tuanayopaswa kuiepuka safari hii.

Ni laana ambayo tuliichagua kwa kuwa hakuna binadamu mwenye haki ya kumtawala binadamu mwenzake bila ridhaa yake. Na ndio maana tunapiga kura. Tulifanya makosa. Laana imetufundisha. Tuiondoe nchi yetu kutoka kwenye laana hii ya kutawaliwa na kundi hatari la mafisadi. Kumpigia kura fisadi kwa vile tu umepatiwa Shati, Khanga, Umekula, umekunywa pombe ni uzuzu. Kumpigia kura mtu asiyefaa kutokana na ushawishi wa fedha na mabango, ni kujiongezea laana. Tupigie kura watu wanaofaa bila kujali vyama vyao

Uchaguzi 2010 ni fursa. Tuitumie kuikomboa nchi yetu!

Cell: 0686371076
 
UKISOMA HADITHI HII ILIYOKO KATIKA GAZETI LA RAIA MWEMA TOLEO LILILOPITA UTAGUNDUA KUWA TANZANIA TUNAHITAJI KUZIBUA MASIKIO NA KUPANGASA MACHO KWA DAWA MAAALUM.


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.

Mpenzi Frank,

HUJAMBO mpenzi wangu wa moyo? Wiki hii nimekuwaza kwelikweli. Uko mzima? Hakuna anayekughasighasi? Hebu chunga sana mpenzi maana naona hali ya hewa si nzuri hata kidogo.

Ndiyo. Kwa mara ya kwanza mimi Hidaya nimeanza kuogopa. Mwanzoni nilifikiri kwamba mwaka huu hali ya siasa kwetu ni nzuri sana. Watu wanabishana, watu wanaelezana, watu wamejaa moyo wa kupigania misimamo yao kwa nguvu. Na sisi mbumbumbu ambao hatupati nafasi ya kusikia mawazo mbalimbali kila siku tunafaidika na kuanza kutumia akilia zetu. Lakini wiki hii …. Mmmh, sijui.

Kweli mpenzi. Hebu nikuelezee kwa nini. Kwanza Binti Bosi alienda kwenye kongamano na wanafunzi wenzie. Sijui waliongelea nini huko lakini BB alirudi na moto wa ajabu. Kuingia kwa baba yake tu alianza.

‘Shikamoo baba.’

‘Marahaba mwanangu.’

‘Unajua baba tulikuwa na kongamano la wanafunzi leo juu ya nafasi ya vijana katika uchaguzi.’

Bosi hakushtuka bali aliendelea kujibwaga chini na kumngoja Hidaya amletee wiski kama kawaida. Ndiyo maana niliweza kusikia yote hayo.

‘Bila shaka uliwaambia jinsi tunavyowapenda vijana mwaka huu hadi tumewaondoa wazee wengi ili vijana wapate nafasi.’

BB alikaa kimya kidogo hadi bosi akashtuka.

‘Uliwaambia siyo! Sisi tunajali vijana sana, ndiyo maana sisi ni chama pekee chenye umoja wa vijana.’

BB alizidi kusita lakini hatimaye moto wa volkano ulizidi nguvu ubaridi wa woga.

‘Kwanza baba huu umoja wenu umeongelea masuala ya vijana mwaka gani? Nionavyo mimi wale ni jeshi la mamluki tu la wanasiasa fulanifulani dhidi ya wanasiasa wengine.’

Bosi hakuamini masikio yake.

‘Nini!’

‘Ndiyo. Na sikuwaambia hata kwamba baba yangu ni Bwana Mikiki wa Taifa. Nichekwe?’

Bosi presha ikampanda

‘Nini!!!!!’

‘Ulitaka nichekwe? Watu wamechoka baba! Unajua katika wanafunzi woooote tuliokuwa pale, hakuna anayeamini kwamba uchaguzi huu utakuwa huru na haki? Kwa sababu mkiona mambo yanawaendea vibaya mtatumia hila’

‘Upuuzi mtupu!!!! Wenye hila ni wale wapinzani tu. Kweli wanafunzi hawana akili.’

‘Kwani baba hakujawa na rushwa mwaka huu? Hongo kibao? Na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.’

‘Ndiyo maana inabidi tutumie vyombo vya dola. Nyie watoto mnadanganywa tu na maadui?’

‘Jamani baba, tuna macho, tuna masikio, tunaongea na watu. Na kila siku magazeti yamejaa mambo kama hayo.’

‘Nimekuambia magazeti yote ni ya udaku, isipokuwa magazeti yetu. Na vituo vya luninga na redio vyote ni vya udaku pia.’

‘Baba unatania. Yaani mambo yanaharibika hadi hata sisi wanafunzi tunaona bado unakataa tu.’

Ghafla baba akageuka.

‘Hebu njoo ukae hapa mwanangu. Lazima uelewe vitu vichache.’

BB alienda kukaa karibu na baba. Na mimi nikajifanya napolishi meza ya bosi ili nisikie.

‘Uchaguzi huu ni muhimu sana. Labda ndio muhimu kuliko uchaguzi wowote tangu uhuru. Nchi yetu inaandamwa na maadui wabaya sana.’

‘Maadui gani baba?’

‘Maadui walewale wa enzi za ukoloni. Hawakufurahia tuliposimama imara na kudai uhuru wetu lakini tuliwashinda. Sasa wamerudi na ngozi tofauti na kuwarubuni watu eti upinzani ndio wa maana. Hawa wapinzani ni maadui wa taifa.’

BB alionekana anataka kucheka lakini aliweza kujizuia.

‘Lakini baba nilifikiri upinzani ni muhimu katika demokrasia.’

‘Ndiyo lakini si hawa. Hawa wanapinga tu, wanapinga, wanaumbua, wanasema uongo, wanaua watu ….’

‘Wanaua watu?’

‘Ndiyo kwa kuwapa fikra hizi mbovu wanawashawishi watu waachane na baba zao na mama zao bila kujua wanakwenda wapi. Kisha wanapotea jangwani na kufa na njaa. Lakini wanaobaki kwetu wanakula na kushiba na viongozi wanaenda nje kila wakati kuwatafutia chakula zaidi.’

Hapo BB hakuweza kujizuia ingawa labda angejua mlipuko unaofuata angeondoka kimyakimya. Akacheka kwa nguvu. Lo! Bosi akakasirika.

‘Unacheka nini mpumbavu we!’

‘Baba wewe hujui watu wanavyotafsiri mambo kama hayo. Eti nyinyi ni baba na mama huku mnakula wenyewe.’

‘Unanitukana. Unanitukana.’

‘Hapana baba nakuambia wanavyosema watu. Nyinyi mkianza kusema kwamba nchi inaandamwa na maadui, wanasema ndiyo. Mafisadi ndio maadui wenyewe. Na kama mnataka kuleta mawazo ya maadui wa nje, watu wanazidi kucheka na kusema kweli maadui wa siku hizi ni wajanja sana. Hawana haja ya kutawala moja kwa moja. Wanatumia ufisi wa mafisadi kutawala kupitia kwao.’

‘Na wewe! Na wewe unasema nini?’

BB akanyamaza tena.

‘Nimekuuliza na wewe unasema nini?’

‘Nitajua nini mimi baba. Mimi ni mtoto kama unavyosema.’

‘Acha ujinga. Niambie wewe na wehu wenzako mnasema nini.’

‘Mimi napata shida sana baba. Kila siku nashambuliwa kwa sababu wewe ni Waziri. Watu hawana imani kabisa maana hawaoni kwamba mafisadi wanashughulikiwa. Hata kama haya masafari ya nje yanaleta chakula, mafisadi wanatafuna chakula chote na kutubakisha makombo tu.’

Bosi ni mnene Bwana lakini nilishangaa alivyoruka na kumpiga mwanaye teke tumboni.’

‘Msaliti wewe. Kenge kasoro mkia. Kumbe nimemzaa nyoka badala ya mtoto.’

BB alikuwa ameangua kilio kikubwa sana.

‘Waniua baba, waniua.’

‘Kufa, wewe. Laana tupu. Unathubutu kumwambia baba yako maneno kama hayo? Nakuambia tunatawala na tutaendelea kutawala kwa sababu hatuwezi kuruhusu maadui washike nchi.’

Kilio cha BB kilikuwa kimemwita MB aliyekuja akikimbia sana.

‘Jamani kuna nini?’

‘Huyu mtoto wako …’

‘Mtoto wetu.’

‘Hapana. Kwa maneno yake si mtoto wangu tena. Hebu umtoe huko. Baba anamjali mwanaye lakini si mwasi. MTOE.’

Alivyokasirika ilibidi MB na mimi tujaribu kumnyanyua BB ambaye bado alikuwa analia.

‘Baba … baba … unanifanyia hivyo’

Lakini bosi alikuwa hataki kusikia. Alikuwa anazunguka sebuleni akitamba.

‘Hawa wapinzani tutawakomesha. Ndiyo. Kutupinga sisi ni sawa na kumpinga Mungu. Ndiyo. Ndiyo. Wakumbuke yaliyompata Lucifer alipojiona amekuwa mkubwa kuliko Mungu mwenyewe. Sisi ni wenye nchi na maadui hawawezi kutuondoa. Tutawakomesha. Tutawakanyaga. Ndiyo. Hatuwezi kuanguka. Hata siku moja hatuwezi kuanguka.

Basi wakati anatamba hivyo, mguu wake ukashika kwenye zulia akaanguka puuuu! Ilibidi niache kumfukuza BB na kumkimbilia bosi na kumnyanyua huku akipiga kelele.

‘Hatuwezi kuanguka. Hatuwezi kuanguka. Hatuwezi kukubali nchi yetu ishikwe na maadui.’

Lakini mpenzi ukiangalia, kwani BB alikosea nini? Kwani nani adui, fisadi au anayewachukia mafisadi? Kwani kupiga kura kwa wapinzani ni uhaini? Na kwa nini wanataka kutuaminisha hivyo kama si kutumia manguvu kunyamazisha sauti na akili za watu waliochoka?

Kama hawana nguvu ya hoja wanataka kubaki na nguvu tu? Na watu watakubali kupokonywa kwa nguvu? Mbona tuliwasikitikia wenzetu majirani zetu na sisi tunataka kuelekea hukohuko. Naomba Mungu tu watu wenye akili timamu waweze kuwashinda hawa vichwa vibovu wanaotafuta vita bila sababu

Mwenye majonzi moyoni mpenzi. Nakuwazia sana. Najua hautakubali kushindwa kwa hila wala bunduki shujaa wangu.

Hidaya
 
1)kumchagua Jk ili amani na utulivu uendelee
2)Tumchague jk, ili uchumi ukue kwa kasi
3)tusitetereke. kura yako ni siri yako, mpe jk kwa mustkabali wa taifa letu



Hate messages from Rashid Shamte to Dr. Slaa: The Guardian on Sunday

"......Although none of the messages advised for the masses to take any action against the opposition, the rhetoric used was reminiscent of the genocidal propaganda spread in the run-up to the 1994 massacre in Rwanda.

At that time, there was another popular 'Ten Commandments' that was circulated by Hutu extremists in the few days before the genocide, when radio and newspapers were used to incite hate against the Tutsi minority. What followed was the murder of about 1 million Tutsi and moderate Hutus in a genocide that shocked the world......"

If that is amani na utulivu, then amani na utulivu have no meaning.
 
Hate messages from Rashid Shamte to Dr. Slaa: The Guardian on Sunday

If that is amani na utulivu, then amani na utulivu have no meaning.

Ong'wise'

The words Amani na Utulivu can be used in a very corrupted way,

Can be used in a way it supports the evil in all aspects and yet harness all supports from the public...
Can be used to blind and fool the wise, who are feeble and unintelligent,
can be used to intimidate and corrupts the weak and not matured characters,

Finaly the resulsts will be obtained:

A humanbeing who can`t protect his farmily against corrupted hooligans ...cause that is Amani na Utulivu,
A humnanbeing who can`t defend and offend against the evils of the nations... that is amani na utulivu,
A person, who will give in to all what President has asked cause that is ...a&u..
A person who can not question and lead any rational movement cause that is...
A pesron... cause...a&u...

Yes if that is what Amani na utulivu is all about... then it is Suicidal, Injustice and Crime!

AND .. these are not qualities the President of this country wishes to his people!!
 
1)kumchagua Jk ili amani na utulivu uendelee
2)Tumchague jk, ili uchumi ukue kwa kasi
3)tusitetereke. kura yako ni siri yako, mpe jk kwa mustkabali wa taifa letu

kama kura yangu ni siri kwa nini unaniambia nimpe JK? Acha iendelee kuwa siri. 31 oct nitajua la kufanya
 
1)kumchagua Jk ili amani na utulivu uendelee
2)Tumchague jk, ili uchumi ukue kwa kasi
3)tusitetereke. kura yako ni siri yako, mpe jk kwa mustkabali wa taifa letu
-tumchague ili aendelee kuheshimu mafisadi
-tumchague ili aendelee kupanda ndege kula raha majuu
-ili tutawaliwe na familia yake, ridhiwan akiwa mshauri wake mkuu
 
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wa bendera kutoka kwa Waingereza. Ingawa tulio wengi hatukuwepo muda huo, tunajua kuwa wazee wetu walidai uhuru kwa madhumuni ya kuhakikisha tunajitawala ili tujifanyie mambo yetu tunayoyataka bila kushinikizwa na nyingine na pia kuona wananchi wanapata mamlaka ya kuendesha nchi yao.
Kwa hali hiyo kila Mtanganyika alikuwa na matumaini makubwa sana. Kwa hali ya kawaida binadamu ana mahitaji muhumu matatu. Nayo ni chakula, malazi na mavazi. Hivyo mtu yoyote utakayemwona anashughulika ujue yuko katika mchakato wa kuhakikisha anapata hayo mambo matatu bila shida.
Mungu alipomwumba mtu alitaka kila mmoja afaidike na raslimali za pale alipozaliwa. Kwa maana hiyo Mungu alikusudia Watanzania wafaidike na mali zao zilizopo Tanzania.
Ubinafsi ulipoanza, ndipo historia ya dhuluma ilipoanza. Tunasikia mambo ya biashara yalianza kila mtu akitafuta faida kwa kufanya dhuluma kwa mwenzake na hivyo hiyo ikaonekana kwamba ndani kwa kila mtu kuna kitu fulani kinachomssukuma kukusanya mali nyingi kwa kufanya wizi fulani. Hii haikuwa kusudi la Mungu!
Tabia hiyo ni mbaya sana tena nafikiri kwamba ubinafsi ni dhambi. Pale unapofanya dhuluma na hasa kama mtu umekabidhiwa mali ya jumuia wewe unakuwa ni muuaji sawa tu na yule anayechukua panga na kumkata mtu mwingine kwa ajili ya kunyang'anya mali.
Ndugu Watanzania, nchi yetu imetumbukia katika dimbwi kubwa la ubinafsi na wizi mkubwa sana. Viongozi wetu tuliowaamini na kuwapa dhamana wamejisahau na wamefikiri mali yote ni yao na hivyo hakuna haja ya kuwatumikia wananchi ila ni kuhakikisha wanafanya jitihada yoyote kuhakikisha wanashinda na wanabaki madarakani waendelee kuiba na kujinufaisha wenyewe.
Kama vile imesemwa mwanzo kwamba lengo la kudai uhuru kutoka kwa wale waliotangulia kuwa wabinafsi na kuja kututawala na kuiba mali zetu ilikuwa ni kuona mali zetu zinatufaidisha wote. Kitu cha ajabu ni kuwa baada ya kupata uhuru watu wamesahau malengo hayo na wanachofanya ni kuviziana na kila mmoja kunyakua kile kilichopo mbele yake na kuondoka.
Mambo haya yanadhihirika tunapoona viongozi wetu wanalimbikiza mali kupindukia wakati huo Watanzania wengi wakiwa hata hawawezi kupata yale mahitaji muhimu hata kwa kiwango cha chini kabisa.
Serikali yetu ya muhula wa nne imefanya mambo ya ajabu ya ubinafsi pengine kuliko serikali zote zilizotangulia. Hapa ninasema hivyo kwa sababu tumeona viongozi wetu wakiwa mahakamani kwa kesi za kukwapua mali za wananchi. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi.
Eti jamani, katika hali ya kawaida imewezekanaje mtu kupatikana na wizi huo lakini bado akaendelea kuwa katika ofisi ya umma na baadaye kupigiwa chapua la kuchaguliwa tena ili arudi katika nafasi ile ile aliyotumia kuiba mwanzoni?
Hivi sisi Watanzania hatuwezi kuona, kuhisi, kusikia wala kunusa!
Pengine tuseme hivi hatuwezi kuona haya yanayotendeka wazi wazi. Mtu anakuibia halafu baadaye anaomba umchague tena arudi madarakani kwa kukuletea komedi ili usahau lile alofanya mwanzo. Je, sisi Watanzania ni watu wa aina hiyo?
Ndugu zanguni, bila kuwa wanafiki mnajisikiaje pale familia moja inapotumia jasho la mlipa kodi ili kufanya mambo ya kifamilia yasiyo ya msingi kwa ustawi wa taifa letu. Mume ndege, mke ndege, watoto magari ya bei kali. Hizi ni mali za nani hasa.
Watanzania, kwa pamoja tuinuke tukapige kura ili tuwatose hao wasiotufaa.
Tuanze na kuona mali zetu zinavyoliwa na watu wachache wasio na uchungu na nchi yetu.
Mambo ya msingi yanayotakiwa yafanyike ili sisi tujikomboe na umaskini tulio nao ni kuwekenza katika elimu. Hii ina maana elimu ni ufunguo wa maisha. Mtu aliyeenda shule akasoma na kuelewa anaweza kupata chakula bora, malazi na mavazi safi. Kwa maana hiyo kama elimu ndio msingi wa maisha kila mtoto wa Mtanzania anatakiwa apewe elimu bora. Ili kuweza kutimiza hili utoaji elimu hautakiwi kuwa na vikwazo vingi tunavyoona sasa. wengi ni mashahidi wa ukweli kwamba watoto wa walala hoi wameishia darasa la saba si kwa sababu hawana uwezo wa kuendelea juu hapana ila ni kwa sababu ya kutokupata fursa ya kusoma kwa kuwa wazazi wao hakuweza kuwalipia ada na michango mingine. Hii ina maana uwezo wa kifedha ndo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya elimu nchini kwetu. Je, nani atbisha hilo? Kama tunakubaliana hapo, basi kwetu kiongozi anayetangaza elimu bure ndiye huyo anayetufaa sisi na si mwingine.
Kama nyumba ni sehemu ya mahitaji muhimu ya binadamu, ni kiongozi gani atakayetuwezesha sisi tujenge nyumba tuishi ili tuwe tumepata hitaji hilo la binadamu? Mimi nafikiri ni yule anayekumbuka hata kutuambia tu kwamba ujenzi wa nyumba utawezekana kama vifaa vya ujenzi vitakuwa vya bei ya chini ili wengi wetu tununue na tujenge nyumba. Kuongelea tu ujenzi wa barabara haitoshi maana barabara zinakumbukwa zaidi kwa kuwa hao wanaoiba na kufaidika kibinafsi na mali za nchi yetu ndo wenye magari ya kupitisha hizo barabara. Mimi mlala hoi cha msingi nyumba, elimu, na chakula. Barabara sawa lakini twende kwa vipau mbele ili kinachofanyika kimguse mwananchi wa chini kabisa.
Ili wananchi tuwe na nguvu ya kuleta serikali tunayotaka madarakani tunayo silaha moja kubwa: "KUPIGA KURA". Tusidanganywe ili tupige kura kumpigia mtu eti aliyetoa t-shirt, kofia na mabango. Mabango hayo ni fedha yetu inayotumika vibaya. Tunasema inatumika vibaya maana tungeondoa ubinafsi hiyo fedha iliyotumika kutengeneza mabango ingetununulia vitabu ili tusome tupate elimu bora.
Kwa kweli amini msiamini ndugu zangu, Tanzania yetu kwa sasa inahitaji matengenezo makubwa la sivyo huko tunako enda siko tuliko kusudia kwenda.
 
Ndugu zangu Watanzania, inaonekana wengi wetu wamegundua kuwa nchi yetu ipo mikononi mwa mafisadi na hivyo tumeamua kuhakikisha kufanya jitihada ya kuikomboa nchi hii kutoka kwenye mikono michafu ya watu hawa wasio na huruma yoyote.
Kila kukicha wamekuwa wakipanda ndege kwenda nje ya nchi kunywa chai na bwana Obama. Wakiwa majukwaani watuambia wamepigiwa simu na Obama. Sisi simu za Obama hatuzihitaji ila tunachokitaka ni maendeleo. Wakiwa majukwaani wanaonyesha mbwembwe kwamba wanaweza sana kucheza na kunengua kumbe sisi hatuhitaji hayo ila maendeleo.
Ndugu zanguni, hatua hii si mbaya! Tumefika mahali na wala tusikate tamaa kabisa ukombozi umekaribia na tunaweza kurudisha nchi yetu mikononi mwetu. Sisi ni wapiganaji tusiochoka!
Katika historia hakuna mpiganaji yeyote aliyeungwa mkono kwa asilimia mia moja! HAPANA! cha msingi hapa ni kutokukata tamaa maana muda wa ukombozi umekaribia.
Hapa zamani walitudanganya kwa maneno matamu eti maisha bora kwa kila Mtanzania kumbe maana yake ni maisha bora kwa kila mwanafamilia ya bwana mkubwa. Ehee, jamani saa ya ukombozi imefika. Tusilale mpaka tuhakikishe nchi yetu ipo mikononi mwetu.
Kumbe mambo si haba! Mafisadi wanatetemeka na matumbo yao moto.
HATULALI MPAKA KIELEWEKE!!!
 
Uko sahihi.
Naumia kila kukicha ninapoona nchi yangu katika lindi la umaskini huku ikisheeni rasilimali lukuki. Eti Kilimo Kwanza, mbona hawatwambii Dhahabu kwanza? Wameuza kila kitu kwa kisingizio cha uwekezaji huku wakifaidika na mapato yake kupitia foreign accounts.
Kwanini Tz ni maskini? Chama gani kimetawala toka uhuru? Tumechoka!
 
Ndugu zangu Watanzania, inaonekana wengi wetu wamegundua kuwa nchi yetu ipo mikononi mwa mafisadi na hivyo tumeamua kuhakikisha kufanya jitihada ya kuikomboa nchi hii kutoka kwenye mikono michafu ya watu hawa wasio na huruma yoyote.
Kila kukicha wamekuwa wakipanda ndege kwenda nje ya nchi kunywa chai na bwana Obama. Wakiwa majukwaani watuambia wamepigiwa simu na Obama. Sisi simu za Obama hatuzihitaji ila tunachokitaka ni maendeleo. Wakiwa majukwaani wanaonyesha mbwembwe kwamba wanaweza sana kucheza na kunengua kumbe sisi hatuhitaji hayo ila maendeleo.
Ndugu zanguni, hatua hii si mbaya! Tumefika mahali na wala tusikate tamaa kabisa ukombozi umekaribia na tunaweza kurudisha nchi yetu mikononi mwetu. Sisi ni wapiganaji tusiochoka!
Katika historia hakuna mpiganaji yeyote aliyeungwa mkono kwa asilimia mia moja! HAPANA! cha msingi hapa ni kutokukata tamaa maana muda wa ukombozi umekaribia.
Hapa zamani walitudanganya kwa maneno matamu eti maisha bora kwa kila Mtanzania kumbe maana yake ni maisha bora kwa kila mwanafamilia ya bwana mkubwa. Ehee, jamani saa ya ukombozi imefika. Tusilale mpaka tuhakikishe nchi yetu ipo mikononi mwetu.
Kumbe mambo si haba! Mafisadi wanatetemeka na matumbo yao moto.
HATULALI MPAKA KIELEWEKE!!!
Maneno mazuri na yanayotia moyo. Natumai kesho ukweli utakuwa umejulikana na kwa hali yoyote ile siasa za Tanzania hazitakuwa tena kama zile za zamani.
 
Kama mlifuatilia matangazo ya awali ya kura za uraisi wakati yanatangazwa moja kwa moja toka vituoni Dr. Slaa alikuwa anaongoza sehemu nyingi sana,jana walipobadilisha utaratibu eti mpaka tume itangaze hayo ya rais hata kama ni ya awali na kweli vyomba vya habari vikatii, upepo ukabadilika tena hata kule ambako alikuwa amepata kura nyingi tayari tume imekuja kutangaza vituko.Pia angalia sehemu ambazo Chadema imeshinda ubunge utakuta mbunge kapata zaidi ya kura hata 20000 na madiwani wengi ni Chadema halafu et Dr anapata kura zisizozidi 2000 huu ni mpango mahususi kabisa wa uchakachuaji.Ni wazi kabisa hakuna uwiano kabisa wa matokeo.Cha kushangaza taarifa za tume ya uchaguzi mchana huu inaonyesha Dr ni wa tatu,Je inawezekana?
 
Back
Top Bottom