Tanzania yathibitisha uwepo wa wagonjwa wapya 5 wa COVID-19. Waathirika wafikia 32, watatu wafariki dunia

Kesaboso,
Mkuu makonda alizungumza kama mkuu wa mkoa, Kama kiongozi kwenye jamii alipaswa kujua wajibu wake na kufanya yanayopaswa kufanya.

Watu kumsikikiza Makonda walikuwa sahihi. Ukisema tusiwasikilize viongozi wetu maana yake unatuambia tuasi na kwa maana hiyo nchi haitaweza kutawalika
 
FabulousRegularGadwall-size_restricted-1.gif

Tumeingia kwenye wakati wa Kujuta na kusaga meno
 
Kulingana na taarifa ya Wizara ya afya kuhusu Ugonjwa wa virusi vya corona nchini Tanzania wanaume hao wote wawili waliokufa ni raia wa Tanzania.

Wagonjwa hao ni miongoni mwa wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya covid-19.

Waliothibitishwa kupoteza maisha ni Mwanaume mwenye miaka 51, mtanzania mkazi wa Dar es Salaam na mwanaume wa miaka 57

Halikadhalika wizara ya afya imethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wapya watano wa virusi vya corona.

Wagonjwa hao ni wote ni watanzania wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Wagonjwa hao ni wanaume wanne wa miaka 68,54,57 na 41 na mwingine ni mwanamke mwenye miaka 35.

Katika hatua nyingine Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuwepo kwa wagonjwa wengine wawili na kufanya idadi ya walioambukizwa nchini Tanzania kufikia 32, miongoni mwao watano wamepona kabisa.

[https://ichef]Image captionWaziri wa Afya Tanzania Ummy Mwalimu amekua akiwataka wananchi kujihadhari

Waliokutwa na maambukizi baada ya kupokea majibu ya watu waliokuwa wakishukiwa kuwa na maambukizi ni mtanzania mwenye miaka 33 aliyeripotiwa tarehe 7 mwezi Aprili.

Mgonjwa huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali, mafua na kifua na hivi sasa yuko katika kituo kwa ajili ya uangalizi

Mgonjwa wa pili ni Mtanzania mwenye miaka 24, naye aliripotiwa kuwa na mafua na kikohozi naye alichukuliwa sampuli ambayo imeonesha kuwa ameambukizwa na tayari anaendelea na matibabu.

Wagonjwa hawa wote hawana historia ya kusafiri nje ya nchi kwa siku za hivi karibuni.

Wizara ya afya Zanzibar inaendelea kuwafuatilia watu wa karibu wa wagonjwa hao na wale waliokutana nao ili kudhibiti maambukizi zaidi.

Idadi ya watu walioambukizwa visiwani humo hivi sasa imefikia tisa baada ya ongezeko la wagonjwa hao wawili.

Hatua zilizochukuliwa na Tanzania kudhibiti maambukizi zaidi ya corona:

kufungwa kwa shule zote kuanzia za awali mpaka kidato cha sita kwa siku 30 zikiwa ni jitihada za kudhibiti maambukizi.

[https://ichef]Image captionKama njia moja ya tahadhari, ndoo za maji ya kunawa zimetawanywa katika maeneo mbali mbali ya Tanzania.

Serikali imekua ikiwahamasisha watu kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono ili kuepuka kuambukizwa au kusambaza virusi vya corona.

Wizara ilifanya marekebisho ya ratiba kwa wale wanaotarajiwa kufanya mitihani tarehe 4 Mei, itasogezwa mbele kadiri ya matokeo yatakavyojitokeza ili nao wapate kusoma kwa kipindi kilekile kilichokubalika na ratiba hiyo.

Serikali pia ilisitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile ligi kuu ya Tanzania, Ligi daraja la pili, ligi daraja la kwanza lakini pia michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA), michezo ya shule za sekondari(UMISETA) pamoja na michezo ya mashirika ya umma.

Kuzuwiwa kwa mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.

_111750131_efd287aa-479d-46f6-9329-a6f263145e2d.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi:Jamani tumsikilize Profesa Janabi

Makonda: Profesa Janaba ndio nani
 
Sijui Kama wanahitaji kura ya mtu ili kubakia madarakani
Kuruhusu Pandemic kuingia nchini kizembe na kusababisha vifo WHO inaweza kuongea na Fatou Bensouda ili Magufuli na kundi lake wafikishe mbele ya Mahakama
 
Kuruhusu Pandemic kuingia nchini kizembe na kusababisha vifo WHO inaweza kuongea na Fatou Bensouda ili Magufuli ma kundi lake wafikishe mbele ya Mahakama
Mkuu watanzania tunakosea hapa,kwamba mtu aliyefanya uzembe uliogharimu maisha yetu naya watoto wetu hatuwezi kumuadabisha wenye bali tunasibiria WHO au mzungu ndo aje amwadabishe,sina hakika Kama tupo serious
 
Kunawa mikono ...kutofanya Safari zisizo za lazima...kuzuia mikutano na mikusanyiko...kuweka karantini wanaoingia nchini kutoka nje...kutoa elimu ya Corona na kadhalika na kadhalika...
Mkuu umewahi kufika nchi yoyote huko first world countries? Kama huko kunawa mikono hakujasaidie,unadhani huku kajamba nani itafanyakazi?
 
Hilo halina uasi ni kwa ajili ya maisha yako na ndo maana huyo makonda alisema kama huna chakufanya ukae nyumbani ila kama una hitaji unatoka, sasa nyie mnataka mpaka iwe sheria? Kwani kukaa nyumbani hakusema?

Ona uzito wa tatizo mbele yako mwenyewe, na kama mejaaliwa kipato kaa nyumbani, waache wenye shida nao wakatafute cha kwao maana bila kutoka hawali kwa siku moja.
 
Back
Top Bottom