Tanzania yaporomoka tena katika viwango vya Fifa

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Tanzania yaporomoka tena katika viwango vya Fifa
NYON, Uswisi

TANZANIA inakwenda fainali za Afrika za wachezaji wa ndani, CHAN ikiwa imeporomoka nafasi mbili katika kiwango cha Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa.

Nchi hiyo ambayo ilikuwa jana ikicheza na Zimbabwe mchezo wa kirafiki inashika nafasi ya 103 ikilinganishwa na nafasi ya 101 mwezi jana.

Wapinzani wake, Zimbabwe, DRC, Zambia ambao wanashiriki pia fainali hizo, wapo juu ya Tanzania kwa kiwango, wakiwa ndani ya 100 bora, kulingana na takwimu hizo.

Kulingana na orodha hiyo ya Fifa, Tanzania imepoteza pointi mbili, kutokana na kupanda kwa baadhi ya nchi ambazo ama zilishinda mechi za kujipima nguvu au zile za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 ambazo zinaendelea katika mabara mbalimbali.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, timu 1o bora hazikuathirika na orodha hiyo ambayo ilitolewa jana na Fifa.

Katika orodha hiyo, mabingwa wa Ulaya, Hispania ambao walikuwa jana wakicheza na England katika mechi za kimataifa za kirafiki wanaongoza orodha hiyo.

Ujerumani wanafuata, Uholanzi, Italia, Brazil na Argentina zinakamilisha vinara watano. Lakini, katika orodha hiyo, timu 20 imeingia nchi ya Romania.

Miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki, Uganda ndiyo inashika nafasi ya 71 kwa ubora huku Kenya ikiwa katika nafasi ya 98 ya viwango hivyo vya ubora vya Fifa.

Wakati huo huo, Rais wa Chama cha Soka cha Zambia, Kalusha Bwalya amejitoa juzi katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambalo uchaguzi wake ulifanyika jana mjini Lagos, Nigeria.

Bwalya, alijitoa na kumwachia Seketu Patel wa Mauritius ambaye amekuwa mgombea pekee na mwakilishi wa Ukanda wa Kusini mwa Afrika wa baraza hilo.

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=3579&stc=1&d=1234421691
 
Attachments

  • fifa.jpg
    fifa.jpg
    43.5 KB · Views: 67
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom