Tanzania yailalamikia Ugiriki

bagwell

Senior Member
Sep 19, 2012
113
25
Serikali kupitia Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imemwagiza Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela, kuiandikia barua serikali ya Ugiriki kuwa Tanzania imechukizwa na kitendo cha Watanzania waishio nchini humo kushambiliwa wiki iliyopita.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, alisema wamemwagiza Msekela kuiandikia barua Ugiriki kuwa Tanzania haijapendezwa na kitendo kilichofanya na kikundi cha wafuasi wa chama cha Xris Avgi wakiongozwa na wabunge wao dhidi ya Watanzania waishio nchini humo

Haule alisema katika barua hiyo, wamemwagiza Balozi Msekela kuiandikia Serikali ya Ugiriki kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa Watanzania wanapatiwa ulinzi.

Alisema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa balozi Msekela kama ameshaiandika barua hiyo.

“Tumemwagiza Balozi Nsekela katika barua atakayoiandika kwa Serikali ya Ugiriki aiombe kupitia jeshi la Polisi la nchi kuhakikisha ulinzi katika makazi wanayoishi Watanzani unapatikana,” alisema Haule.

Hata hivyo, alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa chama cha Xris Avgi au Golden Down (Neo Nazi) hakihusiani na tukio lililotokea Dar es Salaam la kuuawa kwa raia mmoja wa Ugiriki.

Septemba mwaka huu, wafuasi wa chama hicho walivamia katika ofisi za jumuiya ya Watanzania waishio nchini humo na kuwajeruhi pamoja na kuharibu mali zao.
 
Hata mimi sijafahamu sababu za kuvamiwa Watanzania wenzetu,Serikali yetu ikomae sasa kidiplomasia ili walau tuheshimike maana sijui kama tumeshaombwa hata radhi na serikali ya Ugiriki!
 
Kwani Tanzania ni nini?Nchi au jina la mtu naomba kufahamishwa maana nimeona wanaandika eti watanzania waishio ugiriki!Mimi ninachojua tanzania sio nchi ila ni koloni la CCM na CUF bado haina uhuru sasa balozi anayetumwa kuandika barua anaandika kwa niaba ya hao wa Tz au mkoloni CCM?
 
porojo tu hizi......mtaishia kuandika barua tuu .....

Balozi ameagizwa kuandika barua lakini inaonesha barua bado haijaandikwa.

Huyu balozi nadhani anaogopa bora waziri mwenyewe angeandika ipite kopi tu kwa balozi.
 
Hata mimi sijafahamu sababu za kuvamiwa Watanzania wenzetu,Serikali yetu ikomae sasa kidiplomasia ili walau tuheshimike maana sijui kama tumeshaombwa hata radhi na serikali ya Ugiriki!
Ni nationalists wanaochukia foreigners. Not specifically watanzania.
 
Balozi ameagizwa kuandika barua lakini inaonesha barua bado haijaandikwa.

Huyu balozi nadhani anaogopa bora waziri mwenyewe angeandika ipite kopi tu kwa balozi.

hapa kinacchochezwa ni mcheo wa kisiasa kuonekana serikali yetu imelaani vikali na imetoa tamko...mwisho wa siku ishu inawekwa kapuni....kwani ni mara ya kwanza watanzania wa nje ya nchi kufanyiwa unyama na hatua kutokuchukuliwa?? unakumbuka ile ishu ya URUSI JAMAA ALIVYOCHANACHANWA VISU usoni?? nini kilifanyika??
waache porojo na kutoa matamko hewa.........
 
Mmarekanki akipata shida ugenini lazima umsikie Obama akiunguruma na kuchukua hatua. Kwa Tz 'life as usual', inauma sana.
 
Mkuu serikali yetu ingeaza kukomaa hapa hapa nyumbani. Kuna watu wako hapa hapa nyumbani wanafanyiwa unyama mkubwa lakini serikali haijali, kwanini ijali walioko nje tu?

Even worse hata wageni wakiuawa hapa serikali haijali.
 
Yeah nilitembelea Greece kikazi Mwaka Juzi; yaani wana watreat waafrika VIBAYA kweli...

Kwasababu ya Matatizo ya UCHUMI wamebadilika na kuwa FASCISTS wakiwaona weusi wanawapiga wakiona weusi

Kwenye foleni ya SUPU au MAJACKET wanawapiga na kama wamepata hizo SUPU wanawanyang'anya

Na watanzania wapo wengi kweli... Wengi wao walikuwa wanaishi TURKEY wakaenda GREECE sababu GREECE

Ilikuwa rahisi kugawa Makaratasi na unajua GREECE ni MEMBER wa EUROPEAN Union na TURKEY sio kwahiyo

Ukipata Makaratasi ya GREECE unaanza kutafuta Makaratasi ya EURO; lakini wabongo wengi kweli wanaishi GREECE

na wengine sasa wanataka kurudi BONGO hakuna Msaada; nilisema Ubalozi wa karibu ni wa ITALY na ni mbali...

Inasikitisha kweli...
 
Nilikuwa Europe mwezi uliopita nilipita Greece siku mbili jamaa yangu kakwama hapo alikuwa baharia ameoa na anafamilia kuondoka hawezi ila maisha magumu sana nilimsadia dola 200 hakuamini alitoa machozi wengi hawajui nini cha kufanya wengi walikata mawasiliano na ndugu zao bongo; na wengine wanadiriki kusema ni bora ya kufa kwa ujumla wamekata tamaa ya maisha; afadhali ya bongo mara 100 kwa sasa hivi, msisahau tulikotoka

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Chama mimi nimeishi europe muda mrefu sana . Kwa hiyo naelewa unachokiongea
 
Chama mimi nimeishi europe muda mrefu sana . Kwa hiyo naelewa unachokiongea

Mkuu si mchezo rumba la ugiriki limenitisha; nadhani serikali zetu zinatakiwa kujifunza hili ni somo michezo ya olimpiki imeifanya Ugiriki iwe masikini; Tanzania watu wananafasi ya kufanya mageuzi ya kiuchumi; ikiwa kama watajituma nafasi ipo hii kukaa kulaumu serikali haisaidii; mkuu nawaonea huruma wabongo wa ugiriki na sijui kama serikali yetu inaweza kuwasaidia kuwarudisha nyumbani wale watakaoamua.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wagiriki ni Mafashist... Tungepeleka hii Issue Umoja wa Mataifa; Sababu Mwanamichezo wao alifukuzwa

Olympics
Sababu ya kuwa immitate waafrika wanaoishi UGIRIKI
 
Back
Top Bottom