Tanzania ya umoja na mshikamano

kausha

Member
Aug 21, 2007
73
4
Wananchi- Nyongeza ya posho ya 200.000 wanayodai wabunge ni kubwa mno
Serikali - Posho hiyo ni ndogo sana ukilininganisha na tunavyojilipa sisi serikalini, madai ya wananchi hayanana msingi kwa sababu hayazingatii hali halisi Posho tunaikubali tunasikitika kwa sababu ni Token.

Wafanyakazi- Mshahara kima cha Chini 150,000 kwa mwezi mdogo haukidhi mahitaji na kukabaliana na mfumuko wa bei unaokua kila siku.
Serikali - Tusameheane mapato ya serikali hayatoshi kutuwezesha kupandisha kima cha chini.

MADAKTARI-Jamani tumepoteza muda mwingi shule tuongezeeni ka mshahara nyumba za kuishi na kaposho ka kufanya kazi katika mazingira hatarishi.

SERIKALI- impossible hizo ni TILIONI za Shilingi kafanyeni kazii kama hamtaki serikalini OUT

Chama Tawala - Kutokana na misukomsuko ya Uchumi wa Dunia sera yetu ya maisha bora kwa kila mtanzania imeishia kwetu viongozi wakuu serikalini na wabunge wenu mkituamini na kutupa kura 2015 maisha tuliyonayo sisi na nynyi mtapata lakini watanzania nyinyi mmeendekeza njaa hamuaminiki mnaweza kutunyima kura zenu ni lazima tujiandae kwa kujilipa vizuri ili tubaki na akiba ya kununua kura zenu kwa pesa kidogo nyinyi hamchelewi kusahau.

KIDUMU CHAMA TAWALA
 
Back
Top Bottom