Uchaguzi 2020 Tanzania ya baada ya Uchaguzi: Taifa lililogawanyika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,522
51,194
Uchaguzi umekwisha,na kwa nguvu za kidola tumerudishwa katika mfumo wa chama kimoja huku kukiwa na vyama vingi vya kuzugia na kudanganyia dunia.

Haya mambo si kwa faida ya Taifa zima, bali ni ego tu ya mtu mmoja na genge lake dogo la watu wanafiki wanaowaza matumbo yao badala ya Taifa zima na hivyo kujitoa ufahamu kwa kuangalia shibe yao ya leo badala ya mustakbali mpana wa Taifa la kesho!

Kutokana na yaliyotokea nchini, kuna mambo nayaona yanaweza kutokea nchini katika awamu hii ya pili ya utawala wa awamu ya tano

1. Kutakuwa na nguvu kubwa ya kuzima moto unaofukuta
Kama ulidhani biashara ya kununua watu waunge mkono juhudi imekwisha, tegemea hii inayokuja kuwa fungakazi, watu wenye ushawishi mkubwa watapewa option chukua mpunga ukae kimya au leta kidomodomo tukikate!. tegemea blackmails za kiwango cha Kimafia!. Sasa watu wana familia zao, wanaogopa hatma ya maisha yao, wapo ambao kwa hofu kubwa watanyamaza, wapo wachache ambao sauti zao zitaendelea kulia kutokea nyikani

2. Kutatokea kibinyo cha wahisani, na hivyo ili tuwe na unafuu tutajikuta tunajikurubisha zaidi kwa wachina
Wahisani wetu kwa miaka mingi ni nchi za Ulaya na Marekani, nchi za Nordic na Scandinavia wamekuwa ni wahisani wetu kwa miaka mingi tangu enzi za mwalimu, hawa wanaguswa na values za demokrasia na haki za binadamu huko wapelekapo misaada. Tegemea kuanza kuona wakipunguza misaada kwa sababu ya kilichotokea katika uchaguzi huu.

Marekani yenyewe inaona uchaguzi huu ulivyoendeshwa kama mpango mkakati wa Tanzania kufuata mfumo wa China wa chama kimoja huku kukiwepo vyama vya kuzugia (kwa wasiofahamu hata China vipo vyama vya kuzugia ila haviruhisiwi kushika dola!!), Kwa hiyo Marekani itatumia ushawishi wake ikiwemo Kupunguza misaada mbalimbali kama vile ya barabara, madawa na pia kuweka kibinyo kupitia mashirika ambayo ina ushawishi mkubwa kama World bank na IMF kuiweka Tanzania katika msitari inaotaka!. Tegemea kuanza kuona Tanzania ikisnza kulazimishwa kwa nguvu kubadili sheria ilizozitunga hivi karibuni ikiwa ni kstika mkakati wa kuminya upinzani wowote wa maana!

3. Kurudishwa kwa mchakato wa katiba mpya, lakini ile ya Chenge siyo ya Warioba
Kutatokea jitihada za serikali kutafuta legitimacy kwa umma, na kwa jumuia ya kimataifa. Wanajua, umma unataka katiba mpya, kwa hiyo kupoza hasira za umma baada ya uwendawazimu uliofanyika katika uchaguzi mkuu huu, wataurudisha mchakato wa katiba mpya pale ulipokuwa umefikia, yaani wataitisha kura ya maoni kupitisha rasimu ya Chenge. Na kwa kuwa katiba ya sasa ya mwaka 1977 inamzuia Magufuli kuendelea na uraisi baada ya mwaka 2025, hata hivyo katiba mpya ikipitishwa haimfungi mtu yeyote kuanza upya!. Kwa hiyo natabiri kuona Wapambe wa Jiwe wakipiga kampeni kali aendelee kwa hoja kuwa katiba hiyo mpya haimfungi mikono kuanza upya baada ya 2025

4. Kutakuwa na umasikini zaidi, hali ngumu ya maisha zaidi Ila kutakuwepo propaganda kali zaidi kuonyesha mambo yako shwari
Katika mazingira ya kisiasa ambayo bunge ni la chama kimoja na wabunge wana utiifu kwa Mwenyeiti tu mtu aliyewapa tonge kwa sababu kimsingi wao kama wao hawana uhalali mbele ya umma ambao haukuwachagua, Katika nchi ambayo wahisani wataacha kumwaga hela, nchi ambayo mifumo ya kisheria ipo compromised ili kuwa in favor ya regime(hata mahakimu na majaji nao wanaangalia bwana mkubwa angependa nini kwenye kuamua mashauri ya aina hii), usitegemee kuona wawekezaji wakileta mitaji kwa wingi, usitegemee kuona wafanyabiashara wakirisk kufungua biashara katika mazingira haya. Hali ya kiuchumi itakuwa ngumu na wimbi la ukosefu wa ajira litakuwa kubwa, na uchungu (bitterness) ya wananchi itakuwa kubwa zaidi na watajaribu kufanya reforms kadha wa kadha kutuliza hasira hiyo (angalia namba 5)

5. Kunaweza kutokea baadhi ya reforms za kutuliza hasira ya umma
Ili kutuliza watumishi wa umma wanaweza kuongezewa vijisenti viwili vitatu kwenye mishahara, Vitambulisho vya wamachinga vitarasimishwa, sasa vitakuwa na jina, picha, jinsia, anuani etc. Wakulima wanaweza kupewa uhuru kidogo wa kuuza mazao yao wanapotaka. Wanaweza kurejesha bunge live.

6. Umma kupoteza imani na dola na mifumo yake na kudharau chaguzi
Kutokana na jinsi uchaguzi huu ulivyofanywa, jinsi bunge lilivyobehave katika muhula wa kwanza wa awamu hii, na mahakama ilivyokuwa ikisimama na utawala katika mashauri yanayohusu demokrasia. Umma utapoteza imani na mambo ya chaguzi, umma kupoteza imani katika njia za kidemokrasia za kubadili serikali, hii ni hatari, kunaweza kutokea watu wakajaribu kuexploit dharau hii, Mwalimu alikutana na kadhia hii miaka ya 1980, na kwa experience ya tukio hilo na mengine yaliyotokea Afrika ni sababu mojawapo iliyomfanya baadae kutaka vyama vingi ili kuwepo na channel tofauti ya mawazo katika nchi (rejea aliposhauri kuwa tusingoje wanaotaka vyama vingi wawe wengi ndo tushtuke kuvileta, alisema hayo akitolea mfano wa rais wa Romania aliyeangushwa na wananchi kwa maandamano)

Kwa hiyo all in all, kuna njia ngumu iliyoko mbele yetu, siyo Wapinzani au CCM wote muda si mrefu tutaanza kuona consequences za uchaguzi huu. Yeyote anayeshangilia uwezo wa mtu kuwa mbunge, au diwani au cheo chochote bila ridhaa ya wananchi basi anashangilia yeye mwenyewe kupokwa nguvu na mamlaka ya kuweka madarakani serikali yake mwenyewe itakayomtumikia, Kiufupi anashangilia yeye kuwa mtumwa wa watawala badala ya yeye kuwa ndiye bosi wa watawala!. Mtawala hatokuogopa kwa sababu anajua kuwa wewe umeplay role ndogo sana ya yeye kuwa pale, mchango uliotuoa kwake ni Ujinga wako tu wa kuunga mkono magumashi yake

Na wale waliowezesha, kama ni wajumbe wa NEC, wakurugenzi, watu wa TISS, wa vyombo vya usalama laiti wangalijua ubaya wa waliyoyatenda kwa mama Tanzania kwa hakika wasingaliyafanya!. Wamelitendea Taifa kosa kubwa na dhulma kubwa ajabu ambalo naamini mpaka siku wanaingia katika makaburi yao kamwe Taifa halitowasamehe!. Wameangalia pafupi sana, badala ya mbele sana kwa mustakbali wa Taifa hili

WHY SHOULD YOU HELP ONE MAN IN HIS EVIL ENDEAVOR, AT THE EXPENSE OF THE WHOLE NATION, ARE YOU THAT SHORT SIGHTED AND CHEAP?
 
Wanatuharibia sana taifa umoja na ustawi. Japo ukweli wanauona dawa machungu yameanza Polepole jana media kasema hawana haja kujipongeza,kushangilia....hadi 2025
 
Watanzania ni MAKONDOO tu wala hawajali. Unawatawala unavyotaka wao alimradi kumekucha.

Elimu duni wanayopewa, siasa ya ujamaa zimewafanya wasitambue haki zao ni zipi. Wamebakia ni watu wa kuburuzwa tu
 
Nchi iko float, kila mtu hana raha, mpaka waliopitishwa bado hawana amani ya kweli, kila mtu anashangaa mpaka mshindi anajiuliza mbona kura zimekuwa nyingi hivi, na kila mtu kwa sasa, hasa mwenye akili haoni hatima yake mbele maana hajui kesho wakiamka watasema nini.
 
Mbona watu mnabashiri mambo mabaya kutoka kwa Rais na serikali yake,kwanini msiwe na matumaini?

Rais JPM alikataa kuwafungia ndani wananchi wake kwasababu ya Covid-19.

Rais JPM kapigania ardhi yawanyonge iliyoporwa na wawekezaji uchwara zirudishwe kwa wananchi na imewezekana.

Rais JPM kawarasimisha wafanyabiashara ndogondogo wafanye biashara zao kwa uhuru bila bughdha.

Moja kati ya kero kubwa kwetu sisi wananchi ilikua ni ufisadi,ubadhilifu na ucheleweshaji wa maendeleo kwa utendaji mbovu wa viongozi wa serikali,JPM kadhibiti hili kwa kiasi kikubwa.

Miaka yote tunajua sera kuu za upinzani huwa ni elimu,afya,ufisadi n.k.
lakini mwaka huu wamekacha kabisa hizi sera na kuzifumbia macho,kwasababu kunakitu Magufuli amefanya.

sera kuu ya mwaka huu kwa upinzani ilikua ni "haki,wajibu na uhuru wa kutoa maoni"
 
Mbona watu mnabashiri mambo mabaya kutoka kwa Rais na serikali yake,kwanini msiwe na matumaini?

Rais JPM alikataa kuwafungia ndani wananchi wake kwasababu ya Covid-19.

Rais JPM kapigania ardhi yawanyonge iliyoporwa na wawekezaji uchwara zirudishwe kwa wananchi na imewezekana.

Rais JPM kawarasimisha wafanyabiashara ndogondogo wafanye biashara zao kwa uhuru bila bughdha.

Moja kati ya kero kubwa kwetu sisi wananchi ilikua ni ufisadi,ubadhilifu na ucheleweshaji wa maendeleo kwa utendaji mbovu wa viongozi wa serikali,JPM kadhibiti hili kwa kiasi kikubwa.

Miaka yote tunajua sera kuu za upinzani huwa ni elimu,afya,ufisadi n.k.
lakini mwaka huu wamekacha kabisa hizi sera na kuzifumbia macho,kwasababu kunakitu Magufuli amefanya.

sera kuu ya mwaka huu kwa upinzani ilikua ni "haki,wajibu na uhuru wa kutoa maoni"
Ardhi ya wanyonge ipi wakati yeye kajimiikisha maelfu ya Ekari huko Karagwe?
 
Kujipendekeza itakuwa kazi kuu Kwa wateule WA raisi kuna wengine watamlamba magufuli miguu na wengine wataenda mbali zaidi watamlamba mwili mzima ilimradi wapate vyeo!!
Kwenye miaka hii mitano kutakuwa na kila Aina ya kituko na vibweka ilimradi mfalme magufuli afurahi
 
Back
Top Bottom