Tanzania: Why we pay Double VAT?

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,375
Wachumi hii imekaaje?
ukinunua airtime recharge voucher unalipia VAT
ukiitumia pia unalipia VAT per minute talktime
hizi caculation zikoje jamani,wenye upeo zaidi watujulishe.
 
Hii mbona simpo mkuu? Ile ya kwanza ni kwaajili ya serikali na ya pili ni kwaajili ya wenyenchi aka mafisadi!
 
Kwa hiyo,una maana hiyo ya pili ni kwa ajili ya kulipia madeni ya kanga/vitenge/kofia nk za uchaguzi na madeni ya Dowans sio !!!!!!!
 
INKOSKAZ....MWANA WA UMSOLOPAGAAZ.....NAKUSALIMU....!
hii ni mada iliyotulia yenye maaana halisi ya GREAT THINKER......haina ushabiki bali imekaa katika kutafuta ufumbuzi wa kweli kwa mtanzania (mlaji) NASEMA TENA NAKUPONGEZA EWE NDUGU WA ALLAN QUARTERMAN
 
Nimekusoma mkuu..Kwa hiyo ID yako najua halmashauri mkichwa ipo sawa..asante sana na umenikumbusha mbaali na macomrade wenzamgu akina bwana Henry na bwana Good..we acha tu!
hayo Mahesabuya VAT siyaelewi na simu ninatakiwa nitumie
 
Hakuna double tax, no.

VAT ni aina ya kodi inayokusanywa kutoka kwenye bidhaa kwa kila hatua ya uzalishaji kutokana na jinsi thamani inavyoongezeka kwenye bidhaa husika. Kwa hiyo utaona kwamba kununua airtime ni hatua moja na kutumia airtime ni hatua nyingine.

by the way si mnajua jinsi wa Tz hatuna forums za walaji kulalamikia mifumuko ya bei,hii siyo ktk simu tu,hata ewura ktk gas ya kupikia,luku tanesco na petroli ,na VAT ni miongoni mwa vyanzo vichache vya mapato ya TRA.kimsingi hakukutakiwa kuwa na VAT ktk kununua vocha na kuitumia vocha kwani sioni value addition ktk hilo,unanunua vocha ili upige simu kwa kutumia mtandao wa mwenye vocha,sasa hiyo value addtion Tax inatokea wapi.
Mtoa mada umeongea la msingi sana ktk hili.Now how do we tackle this VAT ili ipungue ktk cost za kutumia simu.
 
ni kweli kabisa mkuu kuna bidhaa tofauti na zinazostahiki kuwa na added value nyingine ni wizi wa mchana kweupe
 
Hivi TZ hakuna consumer rights board or anything similar in place ?? au ni responsibilities za tbs na tra??!?
 
Mkuu kama zipo basi wanakula mshahara na posho bure wakati wamelala

Wajua TZ kuna mambo mengi sana yanafichwafichwa, ukute hiyo board nayo ipo ila sababu ya kuzama ktk ufisadi vitu vingi sana wananchi wa kawaida haelimishwi. Sielewi mpaka kesho ktk mkoa mmoja kuna mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya, wabunge, maafisa biashara etc etc. ukiwauliza roles zao hawatokujibu na nadhani hawaelewi!! Hakuna sharing of information, inconsistency, ignorance among those leaders ambao wengo hawana uwezo kabisa wa nafasi zao. Safari bado ndefu sana.
 
tutafika? na nahodha mwenyewe keshaachia usukani
 
Kama mnakumbuka wakatia wa kusoma bajeti ya 2010/11, kulitokea mabadiliko ya utozaji kodi kwenye huduma za simu. Moja ya badiliko ilikuwa utozaji wa VAT kwenye vocha badala ya airtime. Hii maana yake ni kwamba, sasa VAT inatozwa moja kwa moja kwenye vocha na sio muda wa maongezi, kwa sababu hapo kabla ilikuwa inatozwa kwenye airtime.

Ikiwa makampuni ya simu yanatoza VAT kwenye vocha na pia kwenye airtime, ni wazi kutakuwa na double VAT payment, so huu ni wizi. Ni muhimu tuwaambie/tuwajulishe baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano ili walishughulikie au wabunge wamhoji waziri wa fedha kulikoni?
 
Hakuna double tax, no.

VAT ni aina ya kodi inayokusanywa kutoka kwenye bidhaa kwa kila hatua ya uzalishaji kutokana na jinsi thamani inavyoongezeka kwenye bidhaa husika. Kwa hiyo utaona kwamba kununua airtime ni hatua moja na kutumia airtime ni hatua nyingine.

okay....what you said is plausible lakini...value inayokuwa added kutoka mtu unaponunua airtime dukani hadi kutumia ni kiasi gani?
Je, unaponunua soda dukani hadi pale unapokunywa nyumbani, napo kunakuwa na value added?
Kwa nini hizi bidhaa mbili zinakuwa treated tofauti?
 
Kama mnakumbuka wakatia wa kusoma bajeti ya 2010/11, kulitokea mabadiliko ya utozaji kodi kwenye huduma za simu. Moja ya badiliko ilikuwa utozaji wa VAT kwenye vocha badala ya airtime. Hii maana yake ni kwamba, sasa VAT inatozwa moja kwa moja kwenye vocha na sio muda wa maongezi, kwa sababu hapo kabla ilikuwa inatozwa kwenye airtime.

Ikiwa makampuni ya simu yanatoza VAT kwenye vocha na pia kwenye airtime, ni wazi kutakuwa na double VAT payment, so huu ni wizi. Ni muhimu tuwaambie/tuwajulishe baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano ili walishughulikie au wabunge wamhoji waziri wa fedha kulikoni?

thank you
 
Hapo ndo tunawachanga akina rostam na vodacom zao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom