Tanzania tuna medali ngapi olimpiki mpaka sasa?

...watalii ambao hawaendi kujifunza zaidi ya kushangaa!
...alietuloga kweli ni kiboko...hatuna hata sehemu moja ya kujidai!
...yawepo na mashindano ya kiduku labda tutakewepo.
 
hivi hatuwezi ku-lobby Mchezo wa BAO au KARATA ukaingizwa kwenye OLIMPIKI 2016?na sisis angalau tushinde medali jamani?
 
Tanzania tuna vipaji vingi sana hususani kwenye Riiadha (jamii za Wafugaji) ARUSHA,MANYARA &SINGIDA lakini hatuna viongozi wenye maono! tunakalia kufuja pesa kuna pesa ilitolewa na KAMATI YA KIMATAIFA YA OLIMPIKI USD 120,000 (Tsh. 192,000,000/= au 192millioni) BAI amekula yote halafu bado anapeta tu mtaani. KWELI SISI WATANZANIA NI WATU WA AJABU DUNIANI. inakuaje mambo yanakwenda shaghala bagala halafu tumetulia tu? hapo ETHIOPIA na njaa/dhiki walizonazo cheki wanavyowapelekesha hata wazungu/kenya leo hii ati TZ inarudi mikono mitupu olimpiki tunaweza lipi?
 
The runner infront of you is always a Kenyan(even when not winning)
 
Mkuu wangu andreakalima medali zinataka maandalizi ya muda mrefu bahati mbaya Tanzania hutuna maandalizi ya kutosha tunaweka kambi mwezi mmoja tunaingia katika mashindano makubwa ya Olympik tunakutana na mataifa yaliyojiandaa vyema kama Kenya unategemea nini ?.Ng'ombe hanenepi kwa siku mmoja mkuu wangu chama cha riadhaa na serekali kupitia wizara ya michezo lazima wawajibike kwa kutufikisha hapa.
 
Last edited by a moderator:
kwa namna tunavyoandaa wachezaji wetu hatutakaa hata siku moja kupata medali au tuwange!
 
na haya mambo tunajitakia wazara husika haioni umuhimu wa kuandaa wanamichezo kwa ajili ya kushinda. hatuna interest ya kushinda labda niseme hivyo. lakini sishangai nini sisi tumewahi kuwa serious kama sio kuteka watu, fitna, uonevu na kujichotea mali isivyo halali kwa kadri upatavyo chance. kwa kweli inakera
 
halafu tunaambiwa raisi anapenda michezo!!!!!!!!! mbona hatuoni au anapenda "mchezo" fulani specific?
inakera sana
 
hakuna tukifanyacho kwa ufanisi na dunia ikatambua tupotupo tu eti tunategemea kupata maendeleo tutayapata kweli? ifike wakati tuamue kutopeleka kabisa ikiwa hatujaamua kupeleka kwa ajili ya kushindana na kushinda. ona china waliamua wakafanya jitihada sasa wanashinda.
au ndio tutasingizia vifaa vya michezo hatuna?
 
Hv unadhani medali ni mchezo mchezo wanariadha wetu kambi yao ilikuwa ni nyumbani kwa mzee bayi kibaha just imagine from there
 
Salam!
Mwenye kujua chochote mpaka sasa Tanzania tumepata medali ngapi za Dhahabu, Fedha na Shaba? hapo jirani zetu kenya jana naona wameongeza nyingine ya Mwanariadha na kapteni wa Timu ya Olimipki David Rudisha, Hongereni Kenya

Tanzania imepeleka huko London wachezaji 6 na viongozi 12, na baadhi ya viongozi wamebeba na wake zao!!! Hadi kufikia mchana huu, Tanzania yenye wakazi milioni 46 haijapata medali hata moja. Waliojaribu wote katika vinyanganyiro vya awali wametolewa!!! Hapa chini nimebandika ramani kuonyesha nchi zilizopata medali angalau moja ya dhahabu (Njano), angalau moja ya fedha (Kijivu), angalau moja ya shaba (Brown) au haijapata kabisa (bluu); na vile vile rejea orodha ya nchi zilizopata medali niliyoambatanisha. Angalia mwenyewe uone nchi yako iko wapi.


2012_Summer_Olympics_medal_map.png
 

Attachments

  • List of medal_Olympic 2012.pdf
    233 KB · Views: 30
medali wakati kambi ilikuwwa kibaha kwa yule mzee anayependa kusifiwa kwa rekodi ya 1974......ooooweeeeh...ptuuu
 
siku wakianzisha mashindano ya kunywa pombe na no*ngo ndio utajua vipaji vya watz; tutalamba medali kibao tuu
 
We uliona wapi mkimbiaji akawa mrembo? hebu wacheki wakenya,wako kimazoezi zaidi,si tunapeleka mrembo eti kisa anamvutia bosi fulani! maajabu! kwanza huko vijijini umasaini na umang'atini kuna wakimbiaji wa ukweli kabisa ,wao wanang'ang'ania ma sister du! haya sasa!

Miminilifikiri yule dada alibeba bendera siku ya ufunguzi ni mfanyakazi wa ubalozini katoa company kuongeza number kumbe ni mshiriki??

Binafsi nimewaona watanzania siku ya ufunguzi tu .................... otherwise nimewaona Wakenya, Waganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia, Mozambique, Botswana, RSA off coures, Sudani......!!!

Hivi kweli kulikuwa na haja ya kupeleka tumu kule?? Kama ni kupeperusha bendera hiyo kazi ingefanya na ubalozi!!
 
Jaman sawa tusiponde sana bila kujiuliza maswali je mnajua David Rudisha ambae ndo nahodha wa kenya? Yule jamaa sio mchezo ana miaka 23 but anarecord zaidi ya 10 na ameanza training za riadha toka mtoto na amesoma shule ya michezo kamkunji high school ambapo amesoma mac donald mariga yule wa inter milan, denis oliech yule wa monaco na wengine kibao, yule ndo usain bolt wa mbio ndefu,

so bongo tusiponde tu maandalizi wakati hatuna wati dedicated na vipaji vya kutosha, inabid tujenge shule za michezo kama kamkunji high school then watu wajitume wakifundishwa kuwa michezo inaleta utajiri kuliko ajira za kusomea uone chini ya uangalizi mzuri uone balaa lake
 
Labda kama kuna medali ya mahudhurio,hiyo nina uhakika vijana watarudi nayo! IOC si wangekuwa hata wanatoa medali ya shaba kwa ajili ya kushiriki tu iwe kama asante kwa kufika!
 
Back
Top Bottom