Tanzania Tumelala??

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,495
2,252
Ahhh nimeandika lipost likubwa likagoma ku-post!

Anyway naona kuna Google Developer Day ya Uganda na ya Kenya zinakuja, TZ zero!

Pia kuna Apps4Africa competition naona kuna Rwanda event na Kenya Event, Bongo zero! Na hata ukiangalia kampuni zilizoanzisha hiyo competition TZ hatupo, sasa ningependa kujua what is going on jamani? TZ hatupo kabisa kwenye haya maswala ya IT au ni nini tatizo?
 
Kama unavyojua mkuu, watanzania wengi hatupendi challenges . watu wanafikiria njia za mkato ambazo wanaushahidi tosha kuwa kuna watu zimewatoa ( Some people have become because of the shortcuts ways of becoming succesful).

Sababu kubwa ndiyo hapo juu, kama tutaacha kujibeba beba kila sehemu, lazima watu wataacha kuogopa challenges and they think, tutakuwa kama hao ndugu zetu lakini kama tutakuwa kila siku matamasha bila kufanya kazi kwa njia za haki basi ndio tutaendelea kuwa warumwa wa uchumi, wateja wa IT, wateja wa bidhaa za kichina, wateja wa maofisini nk.

Lakini hii inatokana na nini basi? 1)Mfumo mbovu na mazingira mabovu ya upatikanaji wa Elimu. Mtu anapata elimu kwa shida mno toka Primary schools hadi Vyuo vikuu hakuna hata siku moja utakuta mtu anauhuru wa kufikiria. 2) Kuelndelea kwa short cut kwa sababu vinaruhusika, utakuta mtu leo anaanza biashara baada ya miezi miwili kesha win, that is too much. 3) Hizi professional work hatuzithamini watanzania, tunakimbilia kuwapa wachina, kila kitu hadi tenda ya kufunga nyaya, kuchimba mifereji bila kujenga internal human capacity kwa ajili ya baadae (kukechapu)/takeover lakini 10% zinatuua.
4) Wataalamu wa ndani hatuaminiki, tunaendesha mikampuni kwa kujuana siyo kwa kujua kazi. watu wanapeana kazi, kwa hiyo utakuta mwenye kampuni keshazoea kupata kazi bila hata kuisotea/kuandika proposal yenye ushindani, mtu anafanya kazi kwa mazoea na wala si kwa utaalamu. Hapa naamanisha we are not updating ourselves to the current situation.
 
Kang: RedDevil : and Others:

Nyie mmefanya nini katika eneo hilo: Somebody Somwhere has to take the lead!
 
Kwa nini unasema tanzania zero. Hizi issue ni za individual.Una uhakika hakuna watanzania wanaoshiriki? Je na wewe mwenyewe unashiriki?

Sijui nasoma kwenye website hiyo ya Google naona ni kama marketting na survey ya bidhaa zao.
 
Ahhh nimeandika lipost likubwa likagoma ku-post!

Anyway naona kuna Google Developer Day ya Uganda na ya Kenya zinakuja, TZ zero!

Pia kuna Apps4Africa competition naona kuna Rwanda event na Kenya Event, Bongo zero! Na hata ukiangalia kampuni zilizoanzisha hiyo competition TZ hatupo, sasa ningependa kujua what is going on jamani? TZ hatupo kabisa kwenye haya maswala ya IT au ni nini tatizo?

Kang,
Kwanini hii drive ya kufanya mambo kama haya isianzishwe na players walioko kwenye soko badala ya kutegemea drive ya serikali peke yake? I believe kuna makampuni mengi ya ndani yanayofanya kazi za IT ambayo yanaweza kabisa kuunganisha nguvu na kuonyesha njia maana si tu kwamba yanaweza kuongezea kukua kwa soko lao la IT, bali pia yanaweza kuchochea ubunifu na kutuwezesha kuwa more aggresive kwenye mambo ya technology.
Wale waliosoma soma naona sasa waanze kufikiria namna ya kutoa michango yao kwa ajiri ya kuliendeleza hili Taifa. Haiwezekani wote tukawa tunavutiwa na siasa tu tukaacha mambo mengine. Tukumbuke sababu nyingine kubwa ya kuanguka kwa dola ya kikomunist ni kushindwa ku match na maendeleo ya technology ya nchi za magharibi. Wakati watu wa magharibu walikuwa wanaendesha mambo yote simulteneously, wao walikuwa wamebobea kwenye suala la ulinzi tu na kusahau mchango mkubwa wa technologia katika ku balance mambo.
Hatubanwi na sheria kama independently and proactively tutaanza kutoa michango yetu ha hali na mali katika maendeleo ya technologia.
 
Kwa nini unasema tanzania zero. Hizi issue ni za individual.Una uhakika hakuna watanzania wanaoshiriki? Je na wewe mwenyewe unashiriki?

Sijui nasoma kwenye website hiyo ya Google naona ni kama marketting na survey ya bidhaa zao.

Hizi ni events za Google sio swala la kushiriki, kuna event Kenya na Uganda, Bongo zero. Sijui unasoma site gani, ila Dev Day inakuwaga kwa ajili ya programmers so inakuwa inahusisha system zote za google ambazo developers wanaweza kutumia Android, Maps API, App Engine etc.
 
Kang: RedDevil : and Others:

Nyie mmefanya nini katika eneo hilo: Somebody Somwhere has to take the lead!

Ni kweli, ila kwa sasa mimi niko chini sana kiuwezo maybe in a few years.
 
Back
Top Bottom