Tanzania Tuivue Gamba tupate (Republic of People of Tanzania) Wana JF Mchango wenu.

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Wana JF

Munaonaje United Republic of Tanzania tukaivua gamba ! Badala ya kuwa na mfumo wa serikali mbili na wazanzibari kudai serikali tatu,na kwa vile kizazi cha sasa hawalitaki au wanalichulia neno Tanganyika,kutokana wengi ya watanganyika wamezaliwa wakati kuna Tanzania.

Sasa mimi pendokezo langu Munaonaje tukavua gamba Tanzania United tukawa na taifa la watu wa tanzania People' Republic of Tanzania ?
Na huku tukawa na muungano mpya na makubaliano mapya na Zanzibar tukawa na United Republic of Tanzania and Zanzibar ?

People's Repulic of Tanzania -Kuwa mwanachama wa United Nation- Sovereign state - Pia kuwa mwana chama wa EAC
People'S Republic of Zanzibar- Kuwa manachama kamili United Nation- Sovereign state- Pia kuwa mwanachama wa EAC
United Republic of Tanzania and Zanzibar- kuwa serikali ya shirikisho.

Nafikiri mfumo wa muungano wa TZ ukapitiwa umpya, ili kuondoa migongano na kupunguza gharama kubwa zinatumika kulinda muungano huu ambao umekuwa na mivutano ndani ya miaka 47,hadi sasa kufikia wazanzibari kuuchukia na kutokwa ndani ya nyoyo kabisa hata amani hauna tena.

Munaonaje wana JF Great Thinkers
 
Nani kakuambia kuwa vijana hatulitaki jina Tanganyika?Na je unafahamu ni jina Tanzania lina tokana na nini?Acha kukurupuka dogo....!
 
for your information there is no republic of people of tanzania....

Maybe to be called people's republic of tanzania

please make your changes first to go with what is correct then try again mwananchi!!!

* IF YOU WANTED TO KNOW WHY??? please READ...
 
Makubaliano Yalikuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kukazaliwa Tanzania yaani Upande wa Bara Ukaitwa Tanzania Bara au Tanzania Mainland
Upande wa Visiwani Ukaitwa Tanzania Visiwani Huku kwa pamoja Wanaitwa Watanzania .
United Republic Of Tanzania U.R.T.

Kukawa na Radio Tanzania Bara na Sauti ya Tanzania Visiwani sio Zanzibar
Haya Nakumbuka Sana Hili la Kurejesha Zanzibar Halipo kwenye Muungano
Sauti ya Tanzania Visiwani


Tanzania ikawa na Mikoa 26. Sasa Imeongezeka yaweza fika hata 30 Sukuma land Iligawanywa Kukawa na Shinyanga na Mwanza
Tabora na Mbeya Zikamegwa Ikazaliwa Rukwa Ikaendelea hadi leo watu wakijitengenezea ulaji.
Tuwe na Majimbo yetu wenyewe Tujiongoze kuliko sasa hivi viongozi hawabebeki wananuka uvundo.
 
Kuitwa Peoples' Republic au jina lingine lolote zuri bila uwajibikaji wa dhati wa viongozi ni bure. Kuna mambo mengi nchi hii yako vizuri kwenye makabrasha lakini utekelezaji hakuna. Oh! Mpaka inachosha kufikiri.
 
Kuitwa Peoples' Republic au jina lingine lolote zuri bila uwajibikaji wa dhati wa viongozi ni bure. Kuna mambo mengi nchi hii yako vizuri kwenye makabrasha lakini utekelezaji hakuna. Oh! Mpaka inachosha kufikiri.
<br />.
<br />
Mchawi wetu, ni CCM na Zanzibar, mpaka tutakapo achana na CCM na kufutilia mbali muungano ndio Tanganyika tutaweza anza fikiria misingi ya maendeleo ya Taifa letu la Tanganyika. Hapa tutapiga makelele kila siku, mara mafuta, mara gesi, mara dhahabu, mara karafuu, mara TRA, mara hatuna uwino. wa mabalozi wanaotuwakilisha, mambo mengimengi tu yasiyokuwa ya maendeleo ndio tunakaa kipiga domo.Waacheni Zanzibar waende zao Tanganyika tujenge nchi yetu
 
kapambane na akina Nguruvi na Mkandara kule kwenye hoja nzito. Hii ilipaswa kuwa post ktk thread ile. Sioni kwa nini uwe uzi mpya!
 
Back
Top Bottom