Jamani hivi hii nchi yetu imekosea wapi? Tuna kila sababu ya nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi tajiri ukanda wa kusini wa jangwa la sahara. Kwanini? mito tunayo ya kutosha, maziwa,madini, bahari na aridhi safi kwa kilimo. Lakini mbona wengi ni masikini wa kutupwa. umeme shida, kilimo cha jembe la mkono na kutegemea mvua, uchumi unapanda lakini wananchi wanazidi kuwa malofa,kijana kijijini utamkuta kavaa t shirts yake chakavu ya kijani imeandikwa maisha bora kwa kila Mtanzania . Hivi tatizo ni nini au tumelogwa? Ni sasa wala siyo jana wala kesho ni wakati wa mabadiliko. Amka kijana usidanganyike na fulana na kitenge wakati wenzako na familia zao wanakula kuku.Au wote inabidi kwenda Loliondo kwa babu kutibiwa ugonjwahuu wa kuridhika kwa kila jambo hata kama lina affect kizazi hiki na kijacho!? Kama tuna watu, aridhi, siasa safi na uongozi bora sasa tatizo ni nini?. Tutafakari pamoja.:angry: