Tanzania Taifa la watu wenye akili Barani Afrika

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,485
11,037
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio chimbuko la Taifa la Tanzania hapo mwaka 1964.Hivyo basi Tanzania ni muungano wa nchi mbili,lakini cha kushangaza nchi moja ipo yaani SMZ lakini Tanganyika imemezwa na muungano.

Tanzania ndio taifa ambalo ukihoji na kushauri mambo ya msingi una kuwa adui wa watawala na kuitwa mchochezi na usiye litakia mema taifa.Lakini ukiwa chawa wa watawala basi tambua hiyo ni fursa hadhimu ya kupata teuzi.

Tanzania kuna mihimili mitatu yaani Bunge,Utawala na mahakama kikatiba ya 1977,Lakini Kuna muhimili ulio chimbimbia zaidi(Hayati JPM aliwahi sema),hivyo kufanya viongozi wa mihimili mingine kuwa chawa wa muhimili huo ni kosa kubwa sana kutenda au kuamua au kutoa ushauri kuhusu muhimili mama.kwa jambo hili bwana Job Ndugai ni muhanga.

Vyombo vya usalama ndani ya Tanzania viliwahi tembezwa nchi nzima kuzuia maandamano yaliyo ratibiwa katika mtandao wa IG na mdada aliye USA.

Kiongozi aliyepata madaraka kupitia katiba na kula kiapo cha kuilinda katiba ndio anaye idharau katiba na kuiita "kijitabu" na wakati huo huo urais kaupata kupitia katiba.

Tanzania ni haki kwa kiongozi kusema uongo na wala hawajibiki kwa uongo alio sema mfano nikwa PM.Majaliwa "JPM ni mzima na anaendelea kuchapa Kazi" kumbe nyuma ya pazia Shujaa kasha tuacha.Waziri wa afya Ummy Mwalimu anaumbuliwa kwa uongo wake kwenye mtandao wa X.

Tanzania kiongozi mkuu wa taifa anawalinda wezi na kuwapa fursa ya kuiba pesa ya umma"kula kwa urefu wa kamba"Dr.Samia.

Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali yaani CAG ni Sawa na toilet paper,maana watu hupiga kelele na kuhoji kwa muda mfupi na kusahau.wahenga waliwahi sema" kelele za Chura.............."

Tanzania kila baada ya miaka 5 hufanya uchaguzi wa madiwani,Wabunge na Rais,hutumi mabilioni kuandaa uchaguzi,Lakini mshindi hategemea Kura za wananchi kushinda nafasi yoyote.Maana Rais ambaye nae huwa mgombea humteua refa wa mchezo.


Tanzania kupata huduma za kijamii ni hisani na Wala sio haki na ili upate huduma kwa haraka ni vema utangulize pesa (Rushwa).

Umma unalipa Kodi lakini kwenye utekelezaji wa miradi ya umma,pesa huonekani niya Rais na Wala sio ya umma,ndio maana tuna kauli ya "Rais Katoa pesa kutekeleza................."

Taaluma sio kigezo cha kupewa nafasi serikali bali kuwa mfuasi wa chama ndio silaha ya pekee.

Ndani ya Tanzania watawala Wanampaka PhD,lakini matokeo yao ya nyuma hayupo kwenye mfumo.

Kutokana na Kazi nzuri ambayo anafanya rais.Waalimu wakuu wa shule za sekondari kwa pamoja wamemchangia pesa Dr.Samia kwa ajili ya kuchukua form ya ugombea wa urais.

Tanzania kiongozi akiharibu sehemu A anahamishiwa sehemu B ili akale kwa juhudi na kulinda maslahi ya wakubwa.

Watanzania sio watu wa kujipigania bali wameweka imani kwa kundi la wachache hilo jukumu.

Nitarudi.
 
Siga okwamba mwana wa mai nikale ku kitebhe nitegelesye amasango ku chalo kunu!
 
Muungano wa Tanganyika & Zanzibar umewafanya watanganyika wamekuwa wapumbavu na wajinga kupita kiasi,uenda tulitupiwa majini yanayoleta Ujinga Vichwani!
 
Muungano wa Tanganyika & Zanzibar umewafanya watanganyika wamekuwa wapumbavu na wajinga kupita kiasi,uenda tulitupiwa majini yanayoleta Ujinga Vichwani!
Muungano unalindwa kwa mtutu wa bunduki na Wala sio hoja.

Wazanzibar wanauza vitu vya Watanganyika kwa wajomba hivi hivi

RIP mchungaji Christopher Mtikila.
 
Back
Top Bottom