nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Saturday, July 20, 2013
http://www.letsgokenya.com/upload/images/lake-jipe-2.png
IMEELEZWA kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa madini ya uraniamu katika ziwa Jipe lililopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Kutokana na kuwepo kwa dalili za kuwepo kwa madini hayo katika ziwa hilo kwa sasa wataalamu wa kuchunguza madini wapo katika mchakato wa kufanya uchunguzi ili kubaini kiasi cha madini kilichopo katika ziwa hilo.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa mipango na utafiti wa madini wa ofisi ya wakala wa ukaguzi wa madini nchini Julius Mushi, wakati wa mafunzo maalumu kwa vyombo vya usalama na wadau wa madini juu ya kudhibiti magendo ya utoroshaji wa madini kwenda nje, yaliyo fanyika wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.