Hii hapa nukuu kutoka kwa mmojawapo aliyekuwepo kwenye sherehe hizo za kuwarudisha vifaru:iweje tuwakodishe wakati hawa wanyama ni adimu?huoni serikali ilikosa mapato kwa wanyama hao kukaa uk?nani aliidhinisha ukodishaji huo?je wanyama wangapi tumewakodisha nje ya nchi na kwa idhini/maslahi ya nani?
Waheshimiwa: jana tulikuwa Mkomazi National Park kupokea vifaru watatu kutoka Uingereza walikokuwa wamepelekwa kuzaliana kwenye mazingira salama. Hapo mtaona Balozi wa Grt Britain na Waziri wetu Balozi Kagasheki na baadhi yetu waalikwa. DHL walichangia Boeing 757 kuwaleta kwenye macontainer matatu hadi KIA. Kuna ujangiri wa kutisha sasa hivi juhudi zisipofanyika tutajikuta hatuna wanyama wote wameuliwa. Tunaomba mchango wenu wa hali na mali, yakiwamo mawazo.
Nadhani hiyo itakupa jibu kwa swali lako.