Tanzania Premier League 'TPL' JKT Tanzania Vs Simba SC Uwanja wa Mkwakwani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya ligi kuu Tanzania (TPL), kuendelea tena leo Jumamosi, Novemba 3, 2018 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti nchini ambapo mechi kali na ya kusisimua itakayovuta hisia za wadau wa soka ni uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, kwa wenyeji JKT Tanzania walio na nafasi ya sita kwenye msimamo (TPL) kupapatuana vilivyo na mabingwa wa nchi Simba SC.

Je..JKT Tanzania wataweza kuzuia makali ya Simba Sports Club? Usikose Ukaambiwa. Kumbuka mechi ni saa 10:00 jioni na itakuwa mubashara Azam Sports 2.

Kikosi kinachoanza leo kwa upande wa Simba SC;

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga, John Bocco Meddie Kagere, Emmanuel Okwi.

Subs;

Deogratias Munish, Juuko Murshid, Said Ndemla, Cleoutus Chama, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Adam Salamba

FB_IMG_15412451406425081.jpeg



Naaaaaaaam mpira umeanza uwanja wa Mkwakwani

JKT Tanzania 0-0 Simba SC

01' Hasan Dilunga anapiga shuti kali lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick.

07' JKT wanakwenda sasa...Hassan Matelema anapiga shuti kali na Aishi anapangua na kukuta Kotei na kuokoa hatari ile

Ilikuwa hatari mno

11' Gooooooooooaaal Gooooooaaal..Mfumba Jicho MK 14 Meddie Kagere anawatangulia Simba bao la kwanza

JKT Tanzania 0-1 Simba SC

15' mashambulizi makali kwa pande zote..JKT wakitaka kukomboa kadhalika Simba wakitaka kuongeza

22' mchezaji Aziz Gilla anapiga shuti kali lakini mpira unagonga mwamba katika lango la Simba SC.

30' Kelvin anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezo mbaya kumchezea Tshabalala

JKT Tanzania 0-2 Simba SC

37' Gooooooooooaaal goooooaal MK 14 Mfumba Jicho Meddie Kagere anaandika bao la pili baada ya kumalizia shuti la Okwi lililogonga mwamba

JKT Tanzania 0-2 Simba SC

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Mkwakwani

Naaaaaaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wako mbele ya mabao mawili bila majibu dhidi ya JKT Tanzania


45' Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga JKT Tanzania Vs Simba SC

48' Goo laaaaaaa MK14 anakosa bao la wazi, ilitokea piga nikupige lango la JKT Tanzania na mpira kuokolewa na mabeki

57' Ali Shiboli anaingia upande wa JKT Tanzania na Mussa anakwenda kwenye benchi

60' Aishi Manula anapata matibabu baada ya kuchezewa vibaya

69' Meddie Kagere anaonyeshwa kadi ya njano

JKT Tanzania 0-2 Simba SC

69' Mabadilko upande wa Simba, anakwenda kwenye benchi Dilunga na anaingia Kichuya

72' JKT Tanzania wanafanya mabadilko, anatoka Kilemile anaingia Bilali

Mpira unachezwa kwa kutegeana hasa kipindi hiki cha lala salama, rafu za hapa na pale

82' Meddie Kagere anakwenda kwenye benchi anaingia Mzamiru upande wa Simba

Wanakwenda JKT, lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Simba

89' Ali Shiboli aliyeingia kipindi cha pili anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi wa kati

90+3 Wakati wowote mpira unamalizika

Naaaaaaaam mpira umekwisha hapa uwanja wa Mkwakwani ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao mawili bila majibu bila majibu

Mabao ya MK 14, Meddie Kagere Mfumba Jicho kunako dakika ya 11' 37 za mchezo huu wa TPL

Timu mzima ya JF imekuletea mtanange huu

Asanteni sana....Ghazwat
 
Kocha wa simba ameshaanza kutoa sababu baada ya kuona atapoteza point leo.mashabiki tujiandae kisaikolojia tu
12877d18ba32721d774e332cd36fcb97.jpg
 
Kaeleza hali halisi...Kuwa maendeleo ya mpira nchini inawezekana tu kukiwa na miundo mbinu bora

Ulitaka asifie kuwa uwanja ni mzuri ilhali mwenye macho haambiwi tazama?

SimbaNguvuMoja acha kuongopa This Is Simba SC
Kocha wa simba ameshaanza kutoa sababu baada ya kuona atapoteza point leo.mashabiki tujiandae kisaikolojia tuView attachment 920127
 
07' Wanakwenda JKT....Hassan Matelema anapiga shuti lakini Aishi manula anapangua na kukuta Kotei na akiokoa naye anakoa..ilikiwa hatari lango la Simba
 
11' Gooooooooooaaal Goooooaaal Mfumba Jicho MK 14.. Meddie Kagere anawatanguliza Simba bao la Kwanza baada ya kufumua shuti kali na kwenda moja kwa moja na kumuacha golikipa wa JKT alichumpa bila mafanikio

JKT Tanzania 0-1 Simba SC
 
Back
Top Bottom