TANZANIA PEKEE: Basi linachukua abiria 95!

Ajali basi la SABENA huko Tabora laua 17, yajeruhi 78. Hivi Tz kuna basi linaweza chukua watu 95? askari kwa nini wasiwajibike? Source ITV
IGP Upoo???? ningekuwa mimi hali kama hii ikitokea ningekuwa nashika shingo ya RPC na hao mabosi wa mikoa kama wanataka kuendelea na nyadhifa zao ingebidi wawe wakali sana kwa wala rushwa, wazembe nk. Tatizo kwa sasa ninasikia {sina uhakika] ni kuwa kuna syndicate ambapo migao ya rushwa inapanda juu hadi kufikia kwa mabosi mikoani na kama unataka upelekwe sehemu nzuri [hasa kwa traffic] inabidi uwe na uso wa chuma ili uendelee .
Mkitaka kuthibitisha kidogo tuu kuhusu haya jaribu kuangalia mali wanazomiliki huwezi kuamini kuwa wamepata kupitia vijishahara wanavyolalamikia. Kwa dar ndiyo usiseme jaribu kuangali hizi dala dala na teksi huwezi amini/
 
Aiseee baba yangu hata lile basi la meridian,dar express,saibaba na rombo express zinazotoka mkuu mashati rombo kwenda dar hazina uwezo kubeba watu 95 imekuwa ndege
 
elimu finyu na tamaa ya pesa ndio chanzo cha ajali. Sasa itabidi tuanze kuwahold accountable wenye mabasi waajari madereva wenye akili. Kila ajali mwenye basi alipe fidia kwa abiria wote ...kuanzia milioni moja na kugaramia matitabu . Wajinga wanatumaliza kila kukicha twafa ..Khaa!
 
Ajali basi la SABENA huko Tabora laua 17, yajeruhi 78. Hivi Tz kuna basi linaweza chukua watu 95? askari kwa nini wasiwajibike? Source ITV

Kwa kweli inasikitisha. Ila si tanzania pekee ni tanzania na INdia. Hujaangalia ajali za India?
 
Kuna mwaka nilikuwa natoka Kondoa nilikuwa nimepanda gari la cNew Central line kiukweli lilikuwa limejaa hasa mpaka kutapika. Mimi nika mueleza konda kuwa naomba kuanzia siti yangu mpaka ya pili naomba kuwa na uwazi yeye akagoma kabisa basi nikamueleza kuwa ntalipoti polisi basi akaniambia fanya ufanyavyo. Niliona isiwe tabu nikapiga kwa Vehicle inspector Dodoma mjini naye akaanza kususa sua nikamtumia meseji kwa lolote litakalotokea atawajibika. Basi unaambiwa tunaondoka tu tukakutana na matrafiki wanawaeleza makonda mmebeba wanaoko humo so punguzeni abiria hilo nikamshukuru Mungu kwa kuwa walitekeleza tuabaki abiria 60 tu mpaka Dom

So tuchukue hatua!!
nilipanda basi la kampuni ya Ally's mwaka jana wkati naenda Kigoma, basi lilikua limejaza kupita maelezo na barabara ilikua ni rough road tulipofika junction ya Burundi na Kigoma kuna kituo cha Polisi hapo Kondakta alishuka akaenda kumpa trafic pesa na safari ikaendelea, yaani tungepata ajali naaamini wangekufa wale wote waliosimama kwanza tukafuatiwa na sisi, naamini ilikua na watu zaidi ya mia moja achilia mbali mizigo na spidi ni zaidi ya mia pia!!!!
 
Kwani kiwango cha Hiace kubeba abiria ni kiasi gani? Au ndo wale tangu kuzaliwa hajaenda vijijini kwenu? Aah ndiyo wale wajukuu wa mafisimaji wasioelewa tabu wapatazo watanganyika.
what????? 200? au ni macho yangu. kwa hiyo unadhani deki mbili 200 sijawahi ona au sikia hiyo.
kwa kawaida hata mia namba haifiki. around 80, yes.
 
Back
Top Bottom