Tanzania ni namba 2 Afrika kwa kuwa na mifugo mingi ila haichangii chochote kwenye uchumi. Serikali anzisheni tozo ya mifugo

Mjinga sana wewe! Uliwahi kujiuliza Nchi hii ina bucha ngapi na kila bucha inalipia leseni na mapato sh ngapi? A unajua ng’ombe mbuzi ngapi zinaenda kuuzwa nje? (Live Animal) achilia mbali exported packed meat?? Hapo bado hujasema ngozi na other products!!
Ama kweli Nchi hii bado ina wajinga wengi sana.
Bucha ni value addition,tunazungumzia kule shambani
 
Labda ungeishauri Serikali iwanyang'anye Wafugaji Mifugo iwe inafuga yenyewe.

Maana Matozo yote hayo na Ushuru bado hauoni mchango wa Mifugo kwenye Uchumi?
 
Kila kitu mnawaza tozo.

Kwanini serekali isianzishe kampuni Tuipe jina TANBEEF, Iwe chini ya wizara ya mifugo.
Wakuze, wasimamie, wazalishe na kuuza bidhaa zote za mifugo nchini.
Itakua na faida lukuki.
1 . Ajira zitazalishwa.
2 . Mapato yatakusanywa kupitia mauzo ya malighafi.
3 . Itasaidia wafugaji kupata soko lao la uhakika kama watakua wanafuga kwa kufuata kanuni za hii TANBEEF.
4 . Kudhibiti uuzaji holela wa malighafi za mifugo na hii itapelekea magonjwa kutokomezwa sababu ili uuze lazima ukachukue mzigo kwa TANBEEF ambao umeshathibitishwa ubora wake.
Wanayo Kongwa Runch, inayo zalisha Kongwa beef, sema ndo hivyo nayo choka mbaya
 
Kwa miaka Mingi tumekiwa tunatakiwa takwimu za Tanzania Kuongoza Kwa Wingi wa mifugo Afrika kuanzia Ng'ombe Hadi kuku.

Ila pamoja na Wingi huo wa mifugo ,Nchi hainufaiki kiasi Cha kutosha na mchango wake ni mdogo sana kwenye Mapato ya Serikali badala yake mifugo inaongoza Kwa kuharibu mazingira,vyanzo vya maji na.kuzakisha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Inashabgaza watu wa Serikali Kushindwa kufikiria vyanzo vipya vya Mapato wakati mifugo ipo na wafugaji hawalipii Kodi yeyote ya maana na Wala hawana leseni za ufugaji.

Sasa Ili kuongeza Mapato ya Serikali na kuongeza mchango wa sekta ya mifugo kwenye Pato la Nchi napendekeza Serikali ianzishe tozo au ushuru wa mifugo yaani kuweka kiasi Fulani ambacho Kila mfugajo kuanzia wa kuku atalipia kulingana na idadi ya mifugo yake Kila mwaka.

Kila Ng'ombe akilipiwa 1,000,mbuzi/kondoo ,nguruwe 500 na Wanyama wengine wadogo wakiwemo ndege mfano kuku walipiwe 200 Kila Moja.

Tukienda hivyo tutapata pesa za kuboresha ufugaji.Mapafo mengi yanapatea huko Kwa wafugaji badala yake watu wanwakaba machinga,hii sio sawa.
Bila shaka wewe ni mgeni ndani ya nchi hii,serikali hii hii iwaachie wazawa bila kuwakamua?hebu Rudi kafanye homework yako vizuri
 
Kodi wanazochukua serikali kupitia miradi/biashara mbali mbali sio kidogo, mpaka kwenye mastand ya mabus wanachukua. Sasa unavyoishauri serikali waanzishe tozo za wanyama sielewi, kama ni ushuru wa minadani wanachukua, sasa kodi ya nini tena!
 
Back
Top Bottom