Tanzania-Nchi iliyopoteza matumaini!!

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Kinachosikitisha sana ni pale ambapo mambo yanafanyika hovyo hovyo tu na watawala wanakaa kimya kama vile wanawaongoza vipofu au viziwi.Hata wanapotokea watu wakasema au kulalamika basi wao huchukuliwa kama maadui wa dola au amani ya nchi.Hivi kweli nchi hii itaendelea kwa mtindo huu??mbona hawa viongozi hawaoni hata angalau uchungu kwa hawa maskini ambao wanawapa kura kila wakati?hivi kweli we kiongozi unajisikiaje unapokuwa unaishi kwenye nyumba nzuri Dar es salaam wakati kule wilayani ulikotoka watu wako wanakula majani alafu we unaenda kuwaomba kura na kuwasahau?zile barabara za kuingilia kijijini kwako hazipitiki na wala umeme na maji hamna,we waona sawa kula raha dar es salaam kweli?ifike mahali watu wamwogope mungu jamani!!!hivi anapotokea mtu akayazungumzia haya matatizo ya jamii hadharani(hata kama wa chama pinzani)hivi huyu anawezaje kuwa adui wa amani au maendeleo?
  • Hii ni nchi pekee ambapo raia wake wamefikia hatua ya kuishi kwa kufuata upepo wa matukio(yawe ya kisiasa au kijamii)ili mradi lililojadiliwa jana hata kama halijapatiwa ufumbuzi basi litafutwa kwa lililojitokeza leo(mfano jamii sasa imejikita kujadili swala la babu wa loliondo na kusahau kuwa nchi iko gizani)
  • Hii ni nchi pekee ambapo raia wake wanaishi kwa woga wa ajabu na kushindwa kujikita kutatua matatizo yao kwa kuwa tu wanaishi kwa fikra ya kuendeleza amani wakati kuna wananchi ambao mlo wa siku hawapati na wengine wanasaza na kutupa(unawezaje kuwa na jamii yenye amani wakati wengi wanashinda na njaa wakati wachache wameshiba na kusaza?
  • Hii ni nchi ambayo viongozi wangependa waheshimiwe kwa kutowatendea haki raia wao.Heshima itoke wapi wakati raia wanapoteza maisha kwa makosa ya serikali(mfano vifo vya mabomu mbagala na g'mboto na vifo vya Arusha)
  • Hii ni nchi pekee ambapo haki haipatikani mahakamani,mwizi wa kuku anahukumiwa kifungo lakini anayeua na kuibia taifa anaachiwa huru
  • Wafanyakazi,waalimu,madaktari na wanafunzi hawapati haki yao ya msingi mfano mishahara mizuri na mikopo ya masomo kwa madai ya ukosefu wa fedha lakini fedha zinaweza kupatikana za kuwalipa matapeli wa nishati
  • Nchi ina kila aina ya raslimali lakini raia wake wengi ni maskini wa kutupwa,nchi inazidiwa kimaendeleo na nchi ambazo hazina raslimali na tumezikomboa kutokana na migogoro ya kivita,angalia majirani zetu wote wametuzidi kwa kila kitu
  • Nchi haina cha kujivunia zaidi ya woga wa amani,hamna shirika la ndege la kujivunia,hamna reli ya kujivunia,hamna bandari ya kujivunia hamna chochote cha kujivunia,hata mlima wetu wa kili ulishajulikana hauko kwetu,mbuga zetu nzuri zinawanufaisha wachache,hata madini yetu hatuyaoni(wameuziwa wageni)
  • Watanzania walio wengi hawajui kinachoendelea nchini mwao,angalau wa mijini wameanza kuamka
  • Nchi hii watu wake wamebaki kushabikia maendeleo ya wenzetu,utakuta watanzania wanashabikia mipira ya nje au vitu vizuri vya wenzetu maana sisi vya kwetu hatuna(hata vingozi wetu wako radhi waende kutibiwa au kutembea nje maana kwetu tuna nini?)
  • Nchi imejaa jamii inayoamini ushirikina kwenye ngazi zote kuanzia viongozi hadi jamii(angalia maalbino walivyo uawa,pia fika bagamoyo uambiwe ambavyo viongozi wetu wanahudhuria kwa waganga wa kienyeji
  • Siasa za nchi zimebaki kuwa za kishabiki zisizo na tija kwa mtanzania,hata akitokea kiongozi makini anaonekana adui au tishio kwa wenzake hata wakubwa zake
  • Mtanzania wa chini ameachwa kujijua mwenyewe na matokeo yake watu wamekuwa desperate kutatua matatizo yao kwa njia yoyote ndio maana hata akitokea mtu akasema anaweza kuwaondolea matatizo yao basi wanaamini,yawe matatizo ya kifedha au maradhi(mfano DECI ya matapeli au sasa babu wa loliondo na tiba yake),haya yote yanatokea wakati nchi ina uongozi uliochaguliwa na hawa hawa maskini(wameachwa wajitatulie matatizo yao)
  • Inapofika mbwa mwoga akafukuzwa sana ili auwawe mwishoni huwa anabadilika ghafla na kumshambulia anayemfukuza.Hili ni angalizo kwa watawala kwani jamii hii itakapochoka(na imeshachoka),itaigeukia mamlaka husika na kudai haki yake kwa nguvu zote
  • Maangalizo kama haya yamejaa kwenye vyombo vya habari makini lakini hayasikilizwi au kufanyiwa kazi,hata vyombo vya dini vimeongea sana
  • Ikumbukwe kuwa maskini akinyanyasika sana mwishoni huwa anamwachia mungu amtatulie matatizo yake na hii ndipo ilipofikia nchi hii(tukumbuke mungu huwa anamjibu mja wake kwa njia za ajabu na za ukweli hivyo iko siku)
  • Iko siku maskini watatoka kudai kilicho chao kwa matajiri
 
Back
Top Bottom