Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
Mkuu Kevo heshima mbele,nimevutiwa na kufurahishwa na hiyo ya kukalia farasi watatu.

Afadhali kama tai ndiyo ingekuwa inagusa washikaji zake pengine sehemu kubwa ya kiwili wili chake ingekuwa iko kwa farasi huyu mwananchi.

Kwa hali ilivyo nitatafuta mahali pa kujificha kama 2010 jemedari huyu ataibuka tena kidedea. Japo sitashangaa hilo kutokea pia!
 
Kwa kweli ufisadi ni tairi lenye petroli lililo shingoni mwa rais yaani kuliwasha ni kujilipua mwenyewe. Hotuba ya kesho bado ninaamini itatisa ila ni kwa vidagaa wa ufisadi. Mapapa hawashikiki ni Tairi lilishingoni. Ila bado kuna nafasi ya kufanya surprise.
 
Hata akivunja bunge na uchaguzi kurudiwa bada atakuwa rais tu, mimi nitampigia kura. Hakuna rais mmbadala dhidi yake Tz.

Na hilo haliwezi kutokea!
 
Hata akivunja bunge na uchaguzi kurudiwa bada atakuwa rais tu, mimi nitampigia kura. Hakuna rais mmbadala dhidi yake Tz.

Na hilo haliwezi kutokea!

FP
Ni wewe huyo?

Kesho sidhani kama kuna jipya. Labda ataacha kumwaga tabasamu lake wakati wa hotuba! Kwi kwi kwi
 
kesho kisura,hatajaribu kujibu mashambulizi dhidi ya serikali yake kwa wale wote wanaoipaka matope juu ya ufisadi,na hivyo kuhitimisha mjadala yote ambayo iliundiwa tume.Hapo ndipo utakuwa mwisho wa mjadala ndani ya bunge na nje ya bunge.

Mwisho atawaomba watanzania wajishughulishe na mambo yanayo waletea maendeleo na kuachana na malumbano ambayo yanawapotezea muda.pia atalishukuru bunge kwa kuwa msitari wa mbele ktk kuikosoa serikali.
Wabunge watashangilia sana kisha baada ya hotuba kwisha watatoka wakisemezana pembeni.
Kisha CCM wataanda maandamano nchi nzima kuhunga mkono hotuba ya raisi.2008 ndio itakuwa imekwisha na watu wataanza kujiandaa na uchaguzi.

katibu tarafa nakuunga mkono. Umepatia 100% ndo itakuwa hivyo. Naumia roho kuona hiyo ndo itakuwa maudhui ya hotuba yake.Naona mwaka huu hatutakuwa na pa kukimbilia. May b tukapate likizo rwanda tuburudishe roho na kujifunza jinsi kagame anavyopambana na kuboresha nchi.
Mnaosubiri kusikia makubwa kesho mmeliwa.Alamsiki
 
Wapambe wapo hapa wameshaiona nyeti hii na hivyo kubadilisha hotuba hiyo lakini nasikia hiyo nyingine ndiyo iko tupu kabisa haina chochote cha maana ni blah blah nyingi tu na kujisifia yeye na serikali yake na chama cha mafisadi.

JK fukuza wanamtandao akiwamo na wote uanze upya maana hawakutakii mema kabisa, lakini una ubavu wa kufanya hivyo? Ukiingia madarakani kimizengwe mizengwe na ufisadi wa hali ya juu badala ya kuwatumikia wale waliokuchagua unawapigia wale waliofanya mizengwe na ufisadi hadi ukaingia Ikulu.

Kama yanakushinda achia ngazi! Hutakuwa Rais wa kwanza kujiuzulu duniani na labda utafungua ukurasa mpya Tanzania wa kuonyesha kwamba hata Rais kama nchi inamshinda basi inabidi akae pembeni na kuwaachia wenye ujasiri na mapenzi ya kweli na Tanzania kushika usukani ili kuiokoa nchi ambayo inaenda mrama
 
Date::8/20/2008
Rais Kikwete kutupa kete yake ya mwisho kwa kuhutubia Bunge
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

LEO ni siku muhimu kwa Rais Jakaya Kikwete kujimaliza kisiasa au kurejesha imani, mapenzi na matumaini ya Watanzania dhidi yake.

Rais anazungumza na Bunge leo wakati tayari, utafiti wa kitaalamu uliofanywa na Mpango wa Demokrasi Awa Chuo Kikuu cha Dar es Salam (Redet) ukionyesha kuwa umaarufu wake kiuntendaji umeporomoka ikilinganishwa na Benjamin Mkapa.

Miongoni mwa sababu za kuporomoka kwa umaarufu wa Rais Kikwete ni serikali anayoongoza kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei ambao huchangia ughali wa maisha.

Utafiti wa Redet umeonyesha pia kwamba, hadi sasa chini ya serikali ya Awamu ya Nne malalamiko na matukio ya umma kuhusu maandamano ya ukosefu wa uwajibakaji ni 34 ikilinganishwa na 18 katika kipindi chote cha uongozi wa Mkapa.

Matokeo haya mapya ya utafiti wa kitalaamu, yanaonyesha kazi kubwa iliyopo mbele ya Rais Kikwete kuweza kurejesha imani na matumaini, ambayo Watanzania zaidi ya asilimia 80 walikuwa wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Hivyo, leo itakuwa ni kete muhimu kwa Rais Kikwete kurejesha imani na matumaini ya umma kwa serikali yake, iwapo atazungumza kwa umakini na kuonyesha njia sahihi ambayo nchi inapaswa kwenda pasipo kutumbukiza siasa.

Ukiacha matatizo hayo, Rais atapaswa kuonyesha msimamo kama mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu ambaye amekula kiapo cha kulinda Katiba na Jamhuri ya Muungano, kwa kutoa maelezo sahihi kuhusu chokochoko za muungano zinazoendelea hivi sasa.

Katika hotuba hiyo, pamoja na mambo mengine ya ufisadi Mwalimu alionya kuhusu nyufa za muungano ambazo kama hazitazibwa kuna siku Jamhuri ya Muungano itasambaratika.

Hili la muungano linapaswa kuwa moja ya jambo kubwa na la msingi, ambalo Rais anapaswa kulitolea kauli nzito ya kimamlaka si kisiasa kwani nyufa alizoonya Mwalimu kuhusu muungano zinajitokeza kwa kwa kasi kubwa.

Kuna mambo mengine, kama ufisadi katika Akaunti ya Maedeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), ambayo ripoti ya uchunguzi amekwisha kabidhiwa, Rais pia atapaswa kueleza hatua za maamuzi.

Watanzania wanataka kuona watuhumiwa walioba fedha hizo zaidi ya Sh133 bilioni wanakamatwa na si kusikia maneno yasiyo na utekelezaji kivitendo.

Pia atapaswa kueleza utekelezaji wa kivitendo kwa mapendekezo 23 ya Bunge kuhusu mchakato wa zabuni ya kufua umeme kwa Kampuni ya Richmond.

Hadi sasa Rais anaonekana kumezwa na kuzidiwa nguvu na mafisadi, ambao baadhi yao ni watu walio karibu naye ndani ya chama na serikali yake.

Rais pia atatakiwa kueleza ni hatua gani zaidi za kivitendo ambazo zinachukuliwa dhidi ya watu wengine wachache wenye fedha chafu, ambao baadhi wamezificha katika akaunti za kigeni hivyo kutishia usalama wa taifa.

Iwapo, Rais atazungumzia mambo hayo mazito kwa umakini na maelezo kujitosheleza kwa Watanzania, atakuwa ameitumia vema kurejesha umaarufu wake na kujenga imani kwa wananchi dhidi yake na serikali anayoongoza na kinyume cha hayo Rais atakuwa anazidi kujimaliza kisiasa.
 
Date::8/20/2008
Watanzania watarajie nini kutoka kwa Kikwete leo?
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajia kulihutubia Bunge mjini Dodoma, ikiwa ni mara yake ya pili tangu aingie mdarakani, mara ya kwanza alifanya hivyo alipolifungua rasmi mara baada ya kuchaguliwa kuiongoza Tanzania mwishoni mwa mwaka 2005.

Kwa maana hiyo, inaonyesha kwamba Kikwete amebatilisha mazoea ya nyuma ya rais kuhutubia Bunge mara mbili tu katika kipindi chake cha miaka mitano (wakati wa kulizindua na kulivunja), ingawa si sheria, kwani ana uhuru wa kufanya hivyo wakati wowote, hasa kama kuna mambo mazito yanayoikabilia nchi.

Kutokana na mazoea hayo ya nyuma, kuna hisia kwamba huenda rais ana mambo mazito anayotaka kuwaambia wananchi kupitia Bunge lao na hatua ambazo serikali yake imeamua kuchukua kwa maslahi ya taifa.

Tangu aingie madarakani, Kikwete amekabiliana na changamoto mbalimbali, ambazo kwa njia moja au nyingine zimetikisa utendaji wa serikali yake, kama vile tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), migororo ya wafanyakazi wanaodai maslahi bora, kashfa ya Richmond na mtafaruku wa Muungano unaoonyesha mpasuko.

Ni kutokana na changamoto hizo na hasa kufuatia kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa watuhumiwa wa fedha za EPA na Timu maalumu iliyopewa kazi hiyo, baadhi ya watu wahahisi kwamba anakwenda kuliambia Bunge kilichomo ndani ya ripoti hiyo, pamoja na hatua zitakazochukuliwa kwa wanaodaiwa kuhusika katika kuhujumu fedha hizo.

Hata hivyo, tunaamini kwamba rais anakwenda bungeni kuwaambia wananchi kupitia wabunge wao mikakati yake ya kuboresha utendaji serikalini na hasa hatua anazaotarajia kuchukua ili kukabiliana na vitendo vyote vinavyoushushia hadhi utawala wake ukiwemo ufisadi, migomo ya wafanyakazi wanaodai maslahi bora na uzembe wa wafanyakazi wa umma ambao umeanza kurejea kwa kasi.

Ripoti ya Utafiti wa hali halisi ya kisiasa nchini, iliyotolewa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia nchini (Redet) na kuonyesha kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) na utawala wake kwa ujumla unapoteza umaarufu kutokana na utendaji hafifu, ni changamoto nyingine inayotakiwa kutolewa ufafanuzi na Rais Kikwete kutokana na ukweli kwamba, wakati anaingia madarakani Watanzania wengi walikuwa na imani kwamba ataleta mabadiliko na kuwafikisha kwenye maisha bora kama alivyowaahidi.
 
Wapenda nchi, lets give him benefit of doubt. Lakini kwa kweli uvumilivu una mwisho. Iwapo hakuna jambo 'tangible' hotuba tupu ni lazima ikemewe na wote wapenda nchi hii kwa ukali wote unaostahili. Ni vema wapambe wake kama wako humu, wamfikishie ujumbe huu mapema, bado ana masaa ya kufanyia hotuba yake modification, japo sina hakika kama anao tena masaa ya kuchukua hatua. Tired of empty words! Taarifa zote tulizonazo zinatosheleza kwa hatua hivyo, hakuna sababu ya kisingizio chochote kwa sababu yeyote ile. EPA, Twin Tower, Ufisadi ndani ya Debt Conversion Scheme ( na hapa siongelei madeni), ufisadi ndani ya CIS (Commodity Import Support), maswala yote ya TANGOLD, MWananchi Gold Company, Meremeta, Deep Green Finance Company Ltd na mengine mengi. Hatuwezi kuendelea kuwa na Serikali isiyo na meno, hata kama inauma, ukweli lazima usemwe, na uchukuliwe hatua. Dhamira njema itajulikana tu kwa hatua dhabiti. Nchi Sovereign, haiwezi kuachia Investigations zake kufanywa na SFO (ambao wanafanya upelelezi kwa mujibu wa Sheria za Uingereza)! This is mockery of democracy. Kama nilivyosema, ninampa Mhe. Rais Benefit of Doubt, lakini Expectations are very high, and ought to be met! It is the minimum I and all those who wish this country well expect.

You're a brilliant mind!
Atukuzwe Mungu milele!!
 
MKJJ,

Nashukuru kwa maoni mazuri.

1) Kesho JK anahutubia tu as a matter of formality. Hakuna maswali wala hakuna kumwuliza maswali. Utmost, tunachoweza kwa mujibu wa Kanuni ni kuomba kujadiliwa kwa Hotuba hiyo ya Rais, lakini si kuomba Repoti yeyote kama ya EPA etc.
2) IGP, TAKUKURU na Mwanyika wanaweza kuitwa iwapo Taarifa yao itawasilishwa Bungeni, na Kamati inayochambua Taarifa yao inayo mamlaka ya kuwaita, lakini si vinginevyo. Wanaweza kuitwa katika capacity zao lakini si kama Kamati ya Rais....The only opening ni pale Taarifa yao itakapokuwa "Tabled", na wakubwa hawa mara nyingi wametumia kisingizio kuwa aliyeunda Kamati ni Rais na hivyo Taarifa hiyo ni ya Rais siyo ya Bunge...

Frankly, sioni umuhimu wa kuwa na bunge! Pesa zote mnazolipwa za marupurupu zingetumika kufanya kitu kingine kulikoni kuwalipa ninyi. Sasa kama hii ripoti haitajadiliwa bungeni (na kwa maelezo yako inaelekea haitajadiliwa), Then, I don't know mnachokifanya huko Dodoma?

P.S. Mimi ningekushauri wewe Dr. Slaa, Zitto, na watu wengine ambao mna nafasi ya kutia vichwa ndani ya jengo la bunge, mtumie fursa hii kudai mabadiliko ya Katiba ili next time, muwe na nguvu ya kujadili ripoti kama hizi, na kuwaita walioandaa ripoti kama hii bungeni. It's time you guys get smarter and make the case to the public kuhusu umuhimu wa kuwa na mabadiliko ya kikatiba.
 
Nhe nhee nheeeeee
nasubiri kitini hapa nimwone rais wangu akilonga bure bungeni. Nhe nhee nheeeeeeeee!!!
 
Nhee Nheeeee Nheeeeeeeee!!!!!!!

Ngoja nikae kitini nimwone rais wangu akihutubia bure bunge la Jamhuri ya Muungano.

Nhee Nheeee Nheeeeeeeee!!!!!!!!!
 
Tunasubiri leo kuthibitisha ktk nchi hii kumgundua mchawi wetu rasmi ni rais au vp. Ye ndie mwenye rungu, akishindwa kulitumia leo sasa tutegemee nini tena 2010?
 
Ngoja ngoja inaumiza matumbo hasa ulichokingoja kisipotokea, kikaja kingine usichokitegemea. Sasa tutaona tusichokitegemea. Zaidi zaidi atasema haya:
+Ufisadi utazungumziwa kidogo tu,
+ muungano sana
+ atalaumu sana wanaokosoa serikali
+ takukuru watapewa sifa

Mwisho wa hotuba hakuna 'action' itakayochukuliwa -wote midomo wazi hahahahahahaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom