Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 205 58.4%
  • Ni Mbaya

    Votes: 147 41.9%

  • Total voters
    351
JK alitwambia miezi michache iliyopita ili kurudisha maadili mema ya Watendaji ndani ya serikali, watendaji watatakiwa wachague siasa au biashara. Sasa kulikoni tena mbona wanapigana vikumbo kufanya ufisadi mwingine? Ile kauli ya JK ilikuwa ni usanii tu?

Vikumbo vya vigogo tenda ya vitambulisho

Mwandishi Wetu Juni 25, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

HOFU imetanda mchakato wa mradi tata wa Vitambulisho vya Taifa unaokadiriwa kugharimu karibu shilingi bilioni 200 unaanza tena leo kwa makampuni mbalimbali ya ndani na nje kuugombea huku baadhi yakihofia mchezo mchafu kutokea.

Hofu hiyo inagubikwa zaidi na kutajwa tajwa kwa watun mashuhuri ndani ya serikali kuhusika na mradi huo kwa namna moja ama nyingine kwa kuwa na uhusiano ama mawasiliano na baadhi ya makampuni yanayowania zabuni hiyo.

Taarifa ambazo Raia Mwema imepata wiki hii zinasema kiasi cha kampuni 104 zimejitokeza kuwania mradi huo mkubwa. Hizo ni pamoja na tatu za Malaysia za Iris, Data Sonic na Malaysia Microelectronics Solutions.

Mengine ni Infotech (T) Limited, Raha.com, Simba Technology, Business Connection, Softnet, Digisec, Etcon na NEC.

Kampuni nyingine ni Agumba, Transnational, Tata, Rubianes, Technobrain, GI, Necordata, IBM (South Africa), Copycat (Tz), BT Connect, SXmart, ZECGroup Computor Mart, Otiglobal na Jaba Trading.

Mradi huu wa Vitambulisho vya Taifa una historia ndefu ukiwa umebuniwa mwaka 1972, kiasi cha miaka 35 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya 1972.

31.jpg

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha

Tangu wakati huo mawaziri wengi waliopita katika Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali, za karibuni zaidi zikiwa ni mgongano wa kimaslahi, ya umma na ya binafsi.

Sasa ni mara ya nne kwa mradi huo kutangazwa kuanza. Oktoba 1995 ulitangazwa na kampuni zipapatazo 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za kifisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyanganyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.

Mwaka 1998 zabuni zilitangazwa tena, waombaji wakajitokeza, lakini Serikali ikaifuta zabuni hiyo na kuahidi kuitangaza upya huku ikiacha kiwingu cha utata.

Mwaka 2007, Serikali ilikaribisha tena wazabuni kadhaa kupitia utaratibu wa Request for Proposal (RFP) ili wawasilishe maombi yao. Kampuni kutoka Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Afrika Kusini na Malaysia zilijitokeza, nyingi zikiwa na ushirikiano na kampuni za kizalendo za nchini.

Mchakato wa kupitia maombi uliashiria matumaini kuwa safari hii Serikali ilidhamiria kwa dhati kukamilisha zoezi hili. Katika hatua ya kushangaza na kwa sababu ambazo hazikuwahi kutajwa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo, Joseph Mungai ghafla alisitisha zoezi zima la mradi huo.

Tangu mwanzo maamuzi yaliyohusu mradi huu yaligubikwa na usiri mkubwa. Kwa mfano, uteuzi wa mshauri wa mradi uliendeshwa kwa upendeleo ambao wafuatiliaji wa mambo wanasema umekiuka sheria za nchi.

Serikali iliipa kazi hiyo ngumu kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na afisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia mchanganuo wa mradi huo.

Katika utangulizi wa mchanganuo wao, Gothan na Kyaruzi, ambao wote wakati wanabuni mradi huo walikuwa watumishi serikalini walitaja washirika wao katika ubunifu huo kuwa ni Profesa Damas Muna, Jaffar Buyogera, Dickson Maimu, Salum Mpugusi, Donald Carriere, Coen Kleihans, Kenneth Roko, Robert Alexander, Richard Butler, Anthony Githua, Rama Mwikalo na Robert Stewart.

Japokuwa mambo hayakuwekwa wazi sana, baadhi ya wanaotajwa katika safu hii ya wabunifu wa mradi wana mahusiano ya karibu na kampuni ya Business Connection iliyomo katika mchakato na Facet Technologies ya Afrika Kusini ambayo inaweza kuingia katika hatua za baadaye.

Lakini pengine utata mkubwa katika mchakato mzima ni unaowakilishwa na kuteuliwa kwa Maimu kuwa kwanza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Vitambulisho, japo sasa anatajwa kuwa Mratibu Mradi.

Kingine kinachoshangaza ni hatua ya Serikali kukubali kwamba baada ya kumaliza mchanganuo wa mradi kundi hili la kina Gotham ndilo liwe linasimamia mradi.

Ukiacha kundi hilo la Gotham, utata mwingine unaogubika mradi huo ni nafasi ya sasa ya Laurence Masha. Miaka kiasi 10 iliyopita Masha alikuwa wakili wa kampuni moja ya Malaysia, ambayo ilishinda zabuni kabla ya mradi kufutwa.

Kampuni hiyo, kimsingi ilishinda kesi na Raia Mwema haikuweza kupata kwa hakika kama ililipwa. Sasa inaaminika kwamba nayo imo katika kinyanganyiro hicho na Masha ndiye Waziri mhusika.

Huko nyuma mradi huo ulipotangazwa tena, kampuni hiyo ilikuwa inajipitishapitisha ikidai kwamba yenyewe ndiyo iliyostahili kupata zabuni kwa kuwa, na kweli, ilishinda wakati ule kabla ya mradi kufutwa.

Kwa upande mwingine, kuna mvutano ambao umedumu kwa muda mrefu sasa ukihusu aina ya teknolojia muafaka kwa mazingira ya Tanzania.

Mojawapo ni ile ya Micro Chip Smart Card ambayo wataalamu wanasema ni ghali mno na kwa kuwa Tanzania haina mtandao wa miundombinu ya mawasiliano ya kisasa, basi itakuwa ni kazi bure kuchagua teknolojia hiyo. Ushauri mzuri uliotolewa ni kuwa na aina ya Smart Card ya kawaida ambayo si ya kiwango cha juu na ambayo itakidhi matarajio ya mradi ili nchi iweze kumudu gharama zake.

Aidha, wachambuzi wa mambo wanashangazwa na mwelekeo wa Serikali kutaka kuendesha mradi huo nchi nzima kwa wakati mmoja jambo ambalo ni gumu.

Wanasema kitaalamu mradi wa ukubwa kama huo unaohusisha teknolojia ya kisasa hauwezi kutekelezwa bila ya majaribio au pilot project ambayo itawezesha marekebisho ya hitilafu na ufanisi kabla ya kueneza nchi nzima.

Wanasema ni dhahiri kuwa kwa mwenendo wanaotaka Wizara, wa nchi nzima mara moja, mradi huu lazima utakwama na kusababisha hasara kubwa kwa nchi.

Wataalamu pia wamekuwa wakihoji dhamira ya kuwa na vitambulisho vingi tofauti, kwa mfano, vitambulisho vya uchaguzi vinavyotolewa na Tume ya Uchaguzi, leseni za udereva zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA), pasi itolewayo na Idara ya Uhamiaji na sasa hivi vitambulisho vya uraia vya Wizara ya Mambo ya Ndani. Hii inadhihirisha namna idara za Serikali zinavyokosa ushirikiano na mipango endelevu kiasi cha kusababisha ubadhirifu usio wa lazima wa fedha za umma.

Vilevile Serikali hadi hivi sasa haijaamua kama mradi huu utajiendesha wenyewe au utagharamiwa na Serikali. Kuna habari kuwa kila raia atalipia kitambulisho chake, na kama hivyo ndivyo basi iko haja ya kuchukua tahadhari kubwa ili wananchi wasije kukamuliwa gharama kubwa zitakazosababishwa na maamuzi mabaya.

Lakini wachambuzi wanasema katika macho ya wanasiasa mradi huu ni bingo ya mwisho na ambayo haifai kuikosa. Ni vigumu kujua idadi kamili ya viongozi wenye tamaa wanaohusika na maslahi binafsi na Mradi huu wa Vitambulisho lakini jambo la uhakika ni kuwa kwa kasi hii umma ujiandae kmwenendo ambao Mhe. Wawa mradi mwingine wenye mauzauza.

Wachambuzi wanasema kwamba kwa kutoonyesha umakini wa mambo, kwa mfano, katika mahitaji ya mradi, kwenye kipengele cha mkataba ama Specific Contract Requirements; Type of Contract kumeandikwa TBD (To be Determined-mkataba utafahamika baadaye) ikiwa na maana kwamba kuna wazo la mradi na hesabu ya fedha inafahamika, lakini haijulikani ni aina gani ya mkataba utaingiwa. Kwamba seriali inategemes mzabuni ndiye aseme aina ya mkataba atakaoingia nayo.

Kwingine ni kwenye Method of Payment: Prices TBD. Kwamba haijulikani malipo yatafanyika kwa mfumo upi.

Kwingine ni kwenye General Supply Expeience, yaani huyo mshindi atatakiwa kuwa na kiasi gani cha fedha ili aweze kuruhusiwa kuendesha mradi huo nako kumean dikwa TBD, maana yake kwamba itamhuhitaji mzabuni ndiye ataje ana fedha kiasi gani za mradi na Serikali umuamini.
 
Kwakua kila mtanzania aliefikisha miaka 18 ana kadi ya mpiga kura ambayo ina picha na maelezo muhimu,na kwakua kadi hii inatumika hivi sasa kama kitambulisho sehemu nyingi,na pia wanaofikisha umri wa miaka 18 wanaandikishwa nchi nzima wakati huu.Sioni umuhimu wa serikali kutumia mabilioni kwenye mradi wa vitambulisho vya kitaifa kwa sasa huku nchi ikikabiliwa na matatizo mengi yanayohitaji utatuzi.Nionavyo mimi mabilioni haya yanaweza kutumika vizuri zaidi kwenye elimu,afya au barabara
 
Last edited by a moderator:
Gee that will surely save us alot of money but you should understand that people pushing this project will be getting a percentage and will make sure it goes through and may have already made plans on what to do with the windfall when it comes.
 
Washahili wanasema "mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake"

hivi unafikiri agenda ya vitambulisho vya taifa ni agenda muhimu hivi sasa? serikali inajua kuwa kuna vitu vya maana zaidi ya vitambulisho vya taifa lakini kwa kuwa huo ni mradi wa pesa nyingi, na kwa kuwa kuna watu wanayo 20 percent zao hapo, na kwa kuwa kwa njia moja au nyingine utawasaidia marafiki zao wa karibu kukuza vipato vyao,,

serikali itaendelea na mkakati huo bila kujali maoni ya wananchi, kama walivyonunua rada kwa lazima. hii ndiyo ya muuza sura wetu kikwete. atleast angesikiliza maoni yetu wananchi basi na kuyanyia kazi
 
Kamuulize Mhe. Mungai, alipofika wizara ya mambo ya ndani aliuona huo mradi wa vitambulisho kama ulaji wake. Taratibu zote zilizokuwa zimefikiwa akazipiga chini na kuanza kufanya zake ikiwemo kuteua members wa board ya vitambulisho. Akiwepo huyo Mungai fedha nyingi zilitumika karibu 200m kabla hata kitambulisho kimoja hakijatoka. Aliposhitukiwa akaomba kujiuzuru na akakubaliwa.

Ninachoona ni ka-mradi ka wazee na tutashuhudia ufisadi mwingine hapo. Walioajiriwa nao inasemekana ni kwa mizengwe. Jamani mwenye taarifa sahhihi kuhusu mradi huo atufahamishe ili tuzidi kuwapigia kelele wenye huo ulaji.
 
Muheshimiwa Rais Kikwete atalihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania siku ya alhamisi. Katika hotuba yake hiyo mojawapo ya mambo atakayozungumzia ni tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali yake.

Sehemu mojawapo ya hotuba hiyo itazungumzia mapambano dhidi ya ufisadi, sehemu hii ya hotuba nimepewa na mmoja wa wanyeti wangu wa siku nyingi ambaye yuko Ikulu. Alisikitika kuwa iwapo hii hotuba ikisomwa kama ilivyo itawanyamizisha wabunge wapiga kelele kwani itaisafisha TAKUKURU na uongozi wake. Mnyeti huyo amenithibitishia kuwa wao kama Ikulu wanajua kuhusu uozo uliopo TAKUKURU na anakiri kuwa kuna mapungufu mengi sana ya kiutawala na kimaadili katika taasisi hiyo nyeti.

sehemu ya hotuba hiyo ambayo ikulu wamepata takwimu kutoka TAKUKURU inajumuhisha uongo na taarifa zilizotengenezwa kuwadanganya watanzania zikionyesha kwamba tangu Hoseah aingie madarakani utendaji wa kazi umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano ripoti hiyo inaonyesha ongezeko la asilimia 292% katika kesi zilizopelekwa mahakamani. Ripoti hiyo inaendelea kudanganya kwa kuwaambia wabunge na watanzania waendelee kuwa na subira eti kesi za grand corruption zinachukua muda mrefu kufanyiwa kazi. Ukweli ni kuwa taarifa hii imelenga kuwanyamazisha wabunge wanaohoji kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya kamati ya tume ya mwakyembe yaliyotolewa bungeni.

Sitakuwa na muda wa kuichambua hotuba nzima hapa, Kwa mfano kuna kipengele kinachosema kuwa mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 2006 TAKUKURU imefungua ofisi za wilaya. Huu ni uongo na upotoshaji kwani kwa taarifa nilizonazo toka ndani ya TAKUKURU ni kuwa tokea uongozi mpya wa TAKUKURU uingie madarakani mwaka 2006 hakuna ofisi zozote mpya za wilaya zilizofunguliwa na TAKUKURU imefunga ofisi za wilaya zipatazo 20 kwa kisingizio cha kubana matumizi wakati bado wilaya hizo zinapigiwa hesabu kwenye budget.

Taarifa za kwamba ndani ya TAKUKURU hali ni mbaya, morari ya wafanyakazi ipo chini sana na mgawanyiko wa viongozi ni mkubwa tayari zimeshafika ikulu siku nyingi.

Katika taarifa hiyo wanaongelea mafanikio waliyoyapata katika mapambano dhidi ya rushwa tangu 2006 na wametaja kuhusu uchunguzi wa manunuzi ya rada. Hivi kweli kama kesi moja tu ya rada inawachukua miaka zaidi ya minne kuimaliza, hawa TAKUKURU wako serious? Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba uchunguzi wa radar haufanywi na takukuru bali unafanywa na SFO ya uingereza, TAKUKURU wao ni bendera fata upepo tu.

Hii ni sehemu ya takwimu za mafanikio ya mapambano dhidi ya ufisadi zilizoingizwa kwenye hotuba itakayosomwa kesho.

TAKWIMU ZA KESI ZA RUSHWA (2005-2008)
Takwimu za: (A)kesi zilizopokelewa, (B)Kesi ambazo uchunguzi wake ulikamilika, (C)Watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu, (D)Kesi zilizofunguliwa Mahakamani, (E)Kesi zilizoendelea kuendeshwa katika Mahakama mbalimbali, (F)Kesi zilizoshinda na watuhumiwa kuhukumiwa vifungo mbalimbali

Mwaka A B C D E F
2005 3,121 540 111 50 202 6
2006 6,320 1,688 209 71 205 18
2007 8,235 2,015 280 196 272 35
07/2008 3,840 615 36 80 288 24

ONGEZEKO LA UTENDAJI KAZI KWA ASILIMIA
(A)Taarifa ambazo zilipokelewa (B) Kesi ambazo uchunguzi wake ulikamilika (C) Watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu (D) Kesi zilizofunguliwa Mahakamani (E) Kesi zilizoendelea kuendeshwa katika Mahakama mbalimbali (F) Kesi zilizoshinda na watuhumiwa kuhukumiwa vifungo mbalimbali

Mwaka A B C D E F
2005 - - - - - -
2006 102% 213% 88% 42% 2% 200%
2007 164% 273% 152% 292% 35% 483%

Muheshimiwa Rais jiridhishe kabla hujasoma hotuba hiyo bungeni ama sivyo utakuja kuumbuka mambo mengine yakifumuka.
 
Kama ndiyo hayo, kweli kazi ipo!!!!! Na afadhali asihutubie kwa sababu hii itakuwa sawa na kung'ang'ania kuzoa maji yaliyomwagika! Nchi inayumba kama washauri ndio wanamshauri rais hivi! Labda anahotuba yake ataitoa mfukoni, siyo hiyo rasmi
 
Mimi umeniacha maana yake hotuba nzima atazungumzia utendaji wa TAKUKURU tu?? ama vipi ????

kama ni hivyo basi hamna la maana.
Mbona kuna mambo mengi ya kuhutubia, ukizingatia watanzania tuna katabia ka kuappretiate kiongozi mkubwa anapoongea.
 
Sasa hii source yako ya habari mbona ime-base kwenye sehemu moja tuu, nashindwa kushawishika kwamba muungwana ataongelea swala moja tuu, halafu kama nitakuwa sikosei hotuba hiyo source wako amekupa kwenye copy iwe soft au hard kwa kuwa haiwezekani katika chit-chat ukawa na uwezo wa kukumbuka takwimu zote hizo, sasa kama ni hivyo basi imwage hiyo hotuba janvini, waungwana waione na waijadili........kama tarehe imekosewa wasiliana na Mwanakijiji.
 
muheshimiwa rais kikwete atalihutubia bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania siku ya alhamisi. Katika hotuba yake hiyo mojawapo ya mambo atakayozungumzia ni tuhuma za ufisadi zinazowakabili baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali yake.

Sehemu mojawapo ya hotuba hiyo itazungumzia mapambano dhidi ya ufisadi, sehemu hii ya hotuba nimepewa na mmoja wa wanyeti wangu wa siku nyingi ambaye yuko ikulu. Alisikitika kuwa iwapo hii hotuba ikisomwa kama ilivyo itawanyamizisha wabunge wapiga kelele kwani itaisafisha takukuru na uongozi wake. Mnyeti huyo amenithibitishia kuwa wao kama ikulu wanajua kuhusu uozo uliopo takukuru na anakiri kuwa kuna mapungufu mengi sana ya kiutawala na kimaadili katika taasisi hiyo nyeti.

Sehemu ya hotuba hiyo ambayo ikulu wamepata takwimu kutoka takukuru inajumuhisha uongo na taarifa zilizotengenezwa kuwadanganya watanzania zikionyesha kwamba tangu hoseah aingie madarakani utendaji wa kazi umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano ripoti hiyo inaonyesha ongezeko la asilimia 292% katika kesi zilizopelekwa mahakamani. Ripoti hiyo inaendelea kudanganya kwa kuwaambia wabunge na watanzania waendelee kuwa na subira eti kesi za grand corruption zinachukua muda mrefu kufanyiwa kazi. Ukweli ni kuwa taarifa hii imelenga kuwanyamazisha wabunge wanaohoji kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya kamati ya tume ya mwakyembe yaliyotolewa bungeni.

Sitakuwa na muda wa kuichambua hotuba nzima hapa, kwa mfano kuna kipengele kinachosema kuwa mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 2006 takukuru imefungua ofisi za wilaya. Huu ni uongo na upotoshaji kwani kwa taarifa nilizonazo toka ndani ya takukuru ni kuwa tokea uongozi mpya wa takukuru uingie madarakani mwaka 2006 hakuna ofisi zozote mpya za wilaya zilizofunguliwa na takukuru imefunga ofisi za wilaya zipatazo 20 kwa kisingizio cha kubana matumizi wakati bado wilaya hizo zinapigiwa hesabu kwenye budget.

Taarifa za kwamba ndani ya takukuru hali ni mbaya, morari ya wafanyakazi ipo chini sana na mgawanyiko wa viongozi ni mkubwa tayari zimeshafika ikulu siku nyingi.

Katika taarifa hiyo wanaongelea mafanikio waliyoyapata katika mapambano dhidi ya rushwa tangu 2006 na wametaja kuhusu uchunguzi wa manunuzi ya rada. Hivi kweli kama kesi moja tu ya rada inawachukua miaka zaidi ya minne kuimaliza, hawa takukuru wako serious? Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba uchunguzi wa radar haufanywi na takukuru bali unafanywa na sfo ya uingereza, takukuru wao ni bendera fata upepo tu.

Hii ni sehemu ya takwimu za mafanikio ya mapambano dhidi ya ufisadi zilizoingizwa kwenye hotuba itakayosomwa kesho.

Takwimu za kesi za rushwa (2005-2008)
takwimu za: (a)kesi zilizopokelewa, (b)kesi ambazo uchunguzi wake ulikamilika, (c)watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu, (d)kesi zilizofunguliwa mahakamani, (e)kesi zilizoendelea kuendeshwa katika mahakama mbalimbali, (f)kesi zilizoshinda na watuhumiwa kuhukumiwa vifungo mbalimbali

mwaka a b c d e f
2005 3,121 540 111 50 202 6
2006 6,320 1,688 209 71 205 18
2007 8,235 2,015 280 196 272 35
07/2008 3,840 615 36 80 288 24

ongezeko la utendaji kazi kwa asilimia
(a)taarifa ambazo zilipokelewa (b) kesi ambazo uchunguzi wake ulikamilika (c) watumishi waliochukuliwa hatua za kinidhamu (d) kesi zilizofunguliwa mahakamani (e) kesi zilizoendelea kuendeshwa katika mahakama mbalimbali (f) kesi zilizoshinda na watuhumiwa kuhukumiwa vifungo mbalimbali

mwaka a b c d e f
2005 - - - - - -
2006 102% 213% 88% 42% 2% 200%
2007 164% 273% 152% 292% 35% 483%

muheshimiwa rais jiridhishe kabla hujasoma hotuba hiyo bungeni ama sivyo utakuja kuumbuka mambo mengine yakifumuka.

unamwaga issue nzito kama hii, halafu unaingia mitini....hainiingii akilini...
 
Mimi umeniacha maana yake hotuba nzima atazungumzia utendaji wa TAKUKURU tu?? ama vipi ????

kama ni hivyo basi hamna la maana.
Mbona kuna mambo mengi ya kuhutubia, ukizingatia watanzania tuna katabia ka kuappretiate kiongozi mkubwa anapoongea.

......kwa mtazamo wa haraka, nadhani source yake iko katika mchango waliopeleka TAKUKURU Ikulu kwa ajili ya hotuba. Haingii kichwani hotuba yote ikajaa taasisi moja tu.

...pili sitaki kuamini kuwa JK hatakuwa makini kiasi hicho cha kwenda kuhutumbia bunge na Taifa kwa ujumla juu ya TAKUKURU tu.
 
Tumpe moyo mleta taarifa, nadhani ameandika paragraph ya pili kuwa sehemu ya hotuba hiyo itaongelea mambo hayo

Waberoya
 
Hotuba itakuwa JF live. I will take that serious mkuu Yebo Yebo!

Jamani hebu semeni muda na sisi tuliko mbali tusikilize. JK ni smart tunaweza tukasikia anatoka bungeni na kuitisha press conference na kutangaza nusu ya wana JF wameula ili nchi inyooke, Mwanakijiji (Mkurugenzi TAKUKURU) Gembe..., Bubu msemaovyo.... teheteheteh
 
Hapo mungwana anaingia kwenye usanii kichwa kichwa mwache ajilengeshe kisha aone reaction ya wananchi watu wameiba kuwapeleka mahakamani mpaka ukunje sarawili yako miaka 7 ijayo????
 
Kuweni macho. Hakuna hotuba ambayo inazungumzia Takukuru tu.

Kuweni macho acheni kusinzia JF!
 
Back
Top Bottom