Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,534
- 8,619
...wapi ..kikwete yupo libya..anafundwa..hutaweza kumuondoa subirini 2010...
Mhh Ndoto hii huenda ikatimia; mwenzio yuko Libya kwa shughuli ya kikazi- eti walimu; eti wanafunzi kugoma; eti EAC kuandaa kombora; eti TRL; eti richmond; eti EPA ya nini; eti Buzwagi; eti raslimali na migodi kutonufaisha waTZ; eti OIC; eti kadhi; yote upepo mwenzio yuko Libya!!!! anakula kuku; sasa je nini zaidi ya hapo kusema huyu si mwenzetu
Kufuatia taarifa kwamba DIT wamegoma (Tz daima), wakidai wale wanafunzi waliofukuzwa warudishe, ni kitendo cha kishujaa kufanywa na wanafunzi. Natamani mlipuko huu wa mgomo uambukize vyuo vingine, halafu sekondari na walimu wao, tutamalizia na wanafunzi wa shule ya msingi. Mgomo utaendelea kwa wafanyakazi wa mashirika fulani wakiunga mkono waalimu,TRL, NMB... Hatimaye mgomo uwe nchi nzima, ikiwezekana mpaka wafanyakazi wa ikulu wenyewe. Usalama wa taifa na polisi nao watagoma, hakuna FFU wa kuzuia migomo na maandamano. Manesi na madaktari wataendelea na kazi yao kama kawaida huku wakiunga mkono hatua itakayofanywa na wenzao katika idara na taasisi zote.
Tutaona watu wakielekea ikulu, tutaona rais aliye waangusha watanzania kwa kujiangusha mwenyewe akitoka ikulu. Tutashuhudia nchi inapita kipindi cha mpito. Tutaona mabadiliko ya amani , hakutakuwa na vifo wala watu kuzimia, ambayo yatakuwa simulizi na fundisho kwa vizazi vijavyo.
Kutakuwa na mjadala wa taifa kuhusu mabadiliko ya katiba, yatakayotoa fursa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kuwa kila chama kitapata nafasi serikalini kulingana na kura walizopata.
Tutaona Tanzania mpya, ambayo siku zote ni nzuri inayoharibiwa na watu wachache kwa uroho wao, kisa kwa sababu ya upole na uungwana wa watanzania. Tutaona nchi iliyobarikiwa kwa mali asili ikifaidi matunda ya uumbaji wake, kwa kila raia kufaidikia na matunda yake.Tutajua vizazi vijavyo jinsi vitakavyokuja kuisifu tanzania ya sasa kwa maamuzi haya mazito. Huku wenyewe tukifanya kazi kwa bidii kila siku pasi kuwa na chembe ya ufisadi.
Nguvu kidogo tu inahitajika sasa, kama hali ni hii migomo nchini kila mahali wataalamu mko wapi, JF je?
wakatabahu!

Hivi yule 1st lady wetu si alikuwa teacher?
Au tuseme kwa vile anakula mikuku na misosi heavy amesahau matatizo ya walimu?
Kweli waTZ wasahaulifu sana huyu mama naye amekulia maisha magumu leo hii anashindwa hata kuwasaidia wenzie?Anashindwa kumbania pua mzee awasaidie walimu wenzie?
Be careful what you wish for, you may receive it.
Kikwete akitoka kuna mkakati gani wa kuhakikisha tunapiga hatua madhubuti mbele?
Kwa hali yoyote Kikwete ana kikomo cha mihula mwaka 2015, baada ya hapo kuna mkakati gani? Tutaenda na sera au ndio tutabaki na siasa za kufuata watu? Tunahakikishaje hatutompata Kikwete mwingine?

Thats right! Kikwete anaweza kuondoka easily tu lakini je nani ameandaliwa kuchukua nafasi yake? Kwa sasa waroho wote wapo gado wakitia ubani jamaa aondoke na majority ya hao hawafai bora ya JK. Kwenye msukosuko huu tusipokuwa waangalifu tutaishia kumtoa lesser devil na kuingiza bigger one
WENYEVITI wa vijiji na vitongoji wa Halmashauri ya Wilaya Tandahimba wamegoma kuanzia Novemba 10 mwaka huu wakidai malimbikizo ya posho za miaka miwili.
Katika risala yao ya utii kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Francis Miti iliyosomwa na Katibu wao, Ahmed Khalifa viongozi hao wa vijiji walisema hawatafanya kazi hizo mpaka halmashauri hiyo itakapowalipa madai yao ya kuanzia Juni, 2006.
"Kwa kipindi hiki cha miezi 28 kuanzia Juni, 2006 hadi Oktoba mwaka huu wenyeviti wa vijiji wote wa kata hizo tatu (za Tarafa ya Mahuta, Mkundi na Chingungwe), tulikuwa tunaidai Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Sh5,880,000."
"Na wenyeviti wa vitongoji ilikuwa halmashauri ya wilaya iwalipe Sh 9,380,000. Madai haya ni kwa wenyeviti wa vijiji 21 na wenyeviti wa vitongoji 67 wa kata hizo tatu," ilisema risala ya wenyeviti hao na kuongeza: "Na hali hii ni kwa Kata zote 22 za wilaya."
Madai hayo yanatokana na malimbikizo ya posho ya mwezi ya Sh 10,000 wanazostahili kulipwa wenyeviti wa vijiji na Sh5,000 kwa wenyeviti wa vitongoji.
Wenyeviti hao wanamshutumu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Gedra Msuya kwa kushindwa kuwatekelezea madai yao ambayo walisema kwamba ni madogo kulinganisha na malipo ya wilaya jirani ya Newala.
Viongozi hao wanadai kwamba Msuya amekataa kuwalipa posho zao na hata ruzuku ya asilimia 50 ya pato la vijiji ili halmashauri zao zijiendeshe.
Wanasema kwamba licha ya kukataa kufanya yote hayo ameshindwa pia kufikisha hoja zao katika baraza kuu la madiwani kama ilivyo sheria.
Akizungumzia madai hayo, Mkurugenzi Mtendaji huyo alikiri kuwa wenyeviti hao wanaidai ofisi yake na ameahidi kwamba suala lao linashughulikiwa.
"Ni kweli taarifa hizo zimenifikia na jana tulifanya kikao na madiwani wote wa Wilaya ya Tandahimba kujadili suala hilo," alisema Msuya.
Hata hivyo, alijitetea kwamba huenda malipo yao yamekwama mahali akidai kwamba amekuwa akiwalipa kwa kutumia utaratibu wa kuandika hawala moja... "Nadhani tatizo liko kwenye akaunti zao hasa kutokana na umbali kwani benki yetu iko Newala."
Msuya alisema kwamba baada ya kukutana na madiwani hao ameunda tume kufuatilia suala hilo.