Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,409
- 8,911
Kwanza nikupe heko mtoa mada. Mojawapo ya matatizo makubwa tuliyonayo Tanzania ni kutafuta njia rahisi kutatua matatizo magumu. Kiukweli wengi wetu lugha hizi zote mbili hatuzifahamu ipasavyo, yaani tunababia babia tu iwe kisw au kiing. Na matokeo yake ndio kuchanganya lugha kusiko na maana. Tutatue kwanza tatizo hili jamani. Kiingereza hatuwezi kukiepuka hata kidogo kama tunataka kasi ya maendeleo yetu iwe ya maana. na hatuwezi kufikia huko kama tunaridhika tu kukariri misamiati michache ya kiingereza na kuitupia tupia tu kwenye mazungumzo ili kuwatisha watu! Na kwa vile lugha zote hatuzijui kikamilifu, ndio maana tunatafuta nafuu katika kuondoa moja au sijui kufanya nini. Tufikirie vizuri, turekebishe mitaala yetu na hapo ndio tutakuwa kwenye mstari safi wa kutatua tatizo hili.
Na wewe pia unajaribu kutoa suluhisho kwa kuendelea kufanya makosa yale yale, kubadilisha mtaala kutasaidia nini? nani kakwambia tatizo ni mitaala? kwa taarifa yako miaka ambayo Watanzania tanajifunza kiingereza ni mingi sana hivyo kwa hali ya kawaida ilipaswa itoshe kabisa na zaidi, katika hali ya kawaida unaweza kujifunza lugha ya kigeni na kuweza kuitumia kwa ufasaha kabisa ndani ya miaka miwili tu, ushahidi upo wazi wapo Watanzania wengi ambao wanakwenda kusoma nje ya nchi na hawajawahi kusoma lugha za nchi wanazokwendwa hata siku moja, lakini ndani ya mwaka wanakuwa wanauwezo wakuitumia vyuoni na kusoma na kumaliza vizuri, wazee wetu wote waliosoma kama ni urusi au Uchina au Brazili. mimi rafiki yangu kaenda Japani na katumia mwaka mmoja kujifunza Kijapani sasa hivi ana shahada ya uhandisi ya Japani, hivyo tatizo la nchi yetu sio sijui kuanza kusomesha watoto kiingereza tangu chekechea kwani kiingereza tunaweza tukawafundisha kwa Kiswahili na bado tukatilia mkazo katika soma la kiingereza na bado wakaweza kukielewa, ndivyo nchi zote za watu wenye akili wanavyofanya, hata siku moja hawajaribu kujadili nafasi au umuhimu wa lugha yao katika nchi yao, bali wanabakiza ya kwao halafu hizo nyingine wunajifunza tu, miaka miwili inatosha kabisa!