cabhatica
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 1,081
- 480
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, kila chama cha siasa kinaparamia jukwaa kunadi sera za chama husika.
Huwa napata shida nikifikiria tutakapofika mahali kama uingereza au marekani ambapo kila baada ya kipindi kifupi nchi inakamatwa na chama tofauti.
Sera za vyama jinsi ambavyo hazishabihiani, itakuwa hivi kwa Tanzania: leo elimu na afya bure, kesho wananchi wachangie elimu na afya, kesho kutwa bure, mtondo kuchangia . Leo tunajenga kiwanda cha silaha, kesho ujenzi haujakamilika unasitishwa na chama kingine. Leo magari ya serikali ni hardtop kesho mashangingi. Kesho kutwa hardtop. Leo tuna mikoa na wakuu wa mikoa, kesho majimbo na magavana, keshokutwa mikoa . Leo tuna wizara ishirini, kesho wizara kumi, keshokutwa wizara thelathini . Leo kipaumbele ni elimu, kabla hilo halijafanikiwa kesho kipaumbele ni kilimo, keshokutwa ni utalii hata kama kilimo hakijafanikiwa, mtondogoo ni uwekezaji, au nishati au maji nk ..Huu ni wendawazimu!!!!!
Jambo ninalotaka wana-jamiiforum wachangie ni hili: Kwanini kama taifa tusiwe na SERA ZA TAIFA halafu kila chama cha siasa kikaratibu mikakati yake ya kutekeleza sera hizo badala ya kila chama kuwa na sera zake?
Hili litatufanya watanzania kuwa na malengo ya pamoja (common goals) na hivyo kuwafanya wapiga kura kuweza kulinganisha mikakati ya vyama mbalimbali kuona ni ipi inatekelezeka ili kufikia malengo yetu kwa haraka na kwa urahisi zaidi hivyo kukipa ridhaa ya kuongoza ..?
Naomba kutoa hoja!