Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 741
- 479
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini amekutana na Mhe. Dkt. Abdullah bin Abdulaziz Al-Rabeeah, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Huduma za Kibinadamu cha Mfalme Salman wa Saudi Arabia kujadili ushirikiano kwenye sekta za afya, elimu na miundombini baina ya Tanzania na Taasisi hiyo.
Dkt. Al-Rabeeah ameahidi kuendeleza mpango wa Kituo hicho kuwasaidia watoto wenye uhitaji wa matibabu ya magonjwa ya moyo na kufanyiwa upasuaji. Kituo kinatarajia kupokea watoto pacha waliogandana kutoka Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kutenganishwa.