Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 4,820
- 8,886
Masanja na Mkandara:
Mnaanza kuleta side shows sasa. Hili suala la kukua kwa elimu katika miaka ya 70 na kuboronga baadaye alikutokea Tanzania peke yake. Limetokea katika nchi nyingi ukiondoa za South East Asia ambazo zimejitahidi kuvuka threshold ya umasikini. Hivyo sio suala la Ujamaa.
Bila haya mna-compare China na Urusi. China ina continuous civilization kwa zaidi ya miaka 3000. Waligundua baruti, karatasi, matumizi ya noti, alphabet na mambo mengi. Mambo mengi waliyofanya miaka 1000 iliyopita bado hayajafikiwa katika jamii yetu leo hii.
Mnazungumzia Urusi nchi inayotoa Brilliant Mathematicians kwa zaidi ya miaka mia moja tena kwenye taasisi zilizojengwa na wafalme na sio comrades.
Z10, wala siyo side shows. Ni kueleweshana tuu kwa sababu tuna mitizamo tofauti.
Unasema kwamba tatizo si ujamaa wala Tanzania pekee yake. What can partly explain that ni deep rooted corruption, mismanagement, na sheer stupidity of its leaders in these African countries. Kwa hiyo bado hujaonyesha Nyerere anahusika vipi na ujinga uliofanywa na unaozidi kufanywa na viongozi wetu wa leo. Ofcourse we can not continue glorifying the past..but truth is...Elimu yetu inashuka kwa sababu hakuna anayeijali. Mfano Nyerere alijenga viwanda vingi think of Mwatex, Sunguratex....name them..je..leo tumlaumu kwa hivi viwanda kufa kifo cha mende? Perhaps Yes. Je tumlaumu kwa hivi viwanda kuuzwa kwa bei ya kutupwa na kugeuzwa kuwa magodown? Iam not sure.
Nikuulize..ni kiongozi gani mwenye pesa TANZANIA..ambaye watoto wake wanasoma shule za serikali, ambako watoto wanategemea uji wa WFP saa nne?? Majority wako nje na international schools. Why? You guessed right. Infact viongozi wengi wa Africa..watoto wao..wanasoma nje kwa sababu elimu za nchini mwao hawazithamini. I will be pleasantly surprised kama mtoto wa Kikwete anasoma Mbuyuni primary school au Muhimbili primary school (na hizi ni far far better by all standards-kulinganisha na sehemu nyingine TANZANIA).
Mkuu mimi narudia tena: kwa logic yako na hali ilivyo sasa hivi..hata hiyo miaka 1000 inaweza ikapita tukawa bado tunapiga marktime hapa hapa tulipo kwenye umasikini. Ukisema maendeleo yetu tangu mwanzo hayakuwa sustainable..I could partly agree. But again I wonder what you would say kwa wakorea, na Asian Tigers waliopokea hiyo hela ya IMF..mbona baada ya mda ile hela imekuwa na positive impact? Ok tutasema sisi hatukuwa na wawekezaji wakubwa kutokana na politics za cold war. LAKINI MKUU huoni kwamba baada ya cold war..tumepata wawekezaji kwenye mali asili zetu ..lakini tukashindwa kulinda maslahi yetu kwenye meza ya mikataba? So what can we do if we cant even negotiate what is rightfully ours? Mbona leo tunashuhudia mataifa yanapokea hela hiyo hiyo ya IMF na WB na masharti magumu..lakini bado wanaitumia vyema..wanalipa deni na kusonga mbele?
Maendeleo ya aina yoyote hayana short cut. Ukiiba you have to be called your rightful name and be taken to your rightful place. Haiwezekani tu dream maendeleo..wakati akina Chenge ambao wameingiza nchi yetu kwenye hasara ya millions of dollars..wakiwa bungeni na kusema "yaliyomkuta ni mitihani ya Mungu". Na guess what? anawahutubia watunga sheria!
Mkuu, naamini kabisa..tatizo letu ni planning na vipaumbele katika maendeleo yetu. Nyerere has got nothing to with this mess (though ni mengi sikubaliani naye-ila kwa hili anastahili credit)
Sasa sijui baada ya miaka ishirini takwimu za wanaojua kusoma zikishuka zikawa 30% Sijui tutamlaumu Nyerere au Kikwete au atakayeingia-God knws.