Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,254
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imethibitisha kwamba nchi hiyo inatarajiwa kukumbwa na El Nino ambayo huambatana na mvua kubwa kutokana na ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki katika bahari ya Pasifiki.

Meneja utabiri wa Mamlaka hiyo, Dr. Mafuru Kantamla amesema : "Mifumo yetu ya hali ya hewa baada ya kuipitia tumejiridhisha na kuona kwamba El Nino hii ambayo tuliiona kupindi cha mwezi wa tano, ni kweli imeshaanza kujitengeneza na inavyoonekana ni kwamba ina asilimia 90 ya El Nino hii kuendelea kuwepo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, 2023".

Kantamla amesema kunapokuwepo El nino " tunategemea ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya nchi" lakini ongezeko hilo linategemea na msimu, na kwamba limetokea katika msimu upi ili kubainisha athari zake.

'Kwa sasa hatuwezi kusema moja moja kwamba msimu huu wa vuli wa mwaka 2023 kwamba tunataraji kwamba mvua itakua kubwa sana, ni mpaka pale wataalam tutakapoenda kukaa mwishoni mwa mwezi wa nane na kujiridhisha kwamba El nino hii ambayo inayotarajiwa itakuwa na athari gani katika msimu huu unaotarajiwa', alisema Kantamla katika taarifa yake.

Meneja huyo ameyataja maeneo ambayo yanaweza kuathirika na mvua hizo kuwa ni pamoja na maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki ikihusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara pamoja na maeneo ya Pwani yanayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
 
Watabiri uchwara mmeanza.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imethibitisha kwamba nchi hiyo inatarajiwa kukumbwa na El Nino ambayo huambatana na mvua kubwa kutokana na ongezeko la joto la bahari katika eneo la kati la Kitropiki katika bahari ya Pasifiki.

Meneja utabiri wa Mamlaka hiyo, Dr. Mafuru Kantamla amesema : "Mifumo yetu ya hali ya hewa baada ya kuipitia
 
Back
Top Bottom