Tanzania: Kila mahali unakoenda ni kero tu

Observer2010

Senior Member
Oct 29, 2010
195
44
Naishangaa sana hii nchi yangu iliyobarikiwa kwa mali nyingi sana za asili, lakini badala ya hizo mali za asili kuwa ni furaha na utajiri kwa wananchi wanaozizunguka, zimegeuka kero kubwa na hatari katika ustawi wa maisha yao.
Binafsi ninashangaa sana hii nchi yangu tajiri wa asili ila wananchi wake tumezungukwa na kero kila mahali na umaskini wa kupindukia. Hebu angalia kero zilizopo na nyingine nyingi sana, nikianzia na mambo ya msingi:
1. Afya: Huko mahospitalini kwetu kunakera sana, kila mtu anajua ujinga mkubwa unaotendeka katika hospitali zetu, yaani maisha ya Mtanzania hayann thamani kabisa mbele ya Mtanzania mwenzake
2. Elimu: Elimu ya sas ni kero kubwa kuanzia kindergarten mpaka vyuo vikuu, hapa tumeona hali inayoendelea hivi sasa, kila mahali ni migomo, sasa migomo imefika mpaka kwenye vyuo vya kidini, hii ni hatari sana
3. Maji: Kila mahali unapokwenda maji ni kero kubwa sana, achilia mbali maeneo machache sana ya nchi hii ambayo sidhani kama yanafikia asilimia 10. Hapa jijini Dar ndio balaa, maji yamekuwa ni tatizo sugu, yaani maji kero kubwa sana kwa Watanzania. Hii nchi imezungukwa na maziwa makubwa na bahari wakati mito mingi ikitirirka katikati ya nchi, lakini bado maji na tatizo na kero kubwa.
4. Miundombinu: Barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege kote huko kumejaa kero nyingi sana . Hapa ndio chanzo cha mafoleni yasiyoisha hapa jijini Dar.
5. Usalama: Hawa jamaa wa naoitwa polisi wa aina zote, kuanzia FFU mpaka trafiki, ni kero kubwa sana kwa watanzania, wao kila kitu wanachofanya wameweka mbele rushwa. Yaani hawa jamaa wanakera sana.
6. Siasa: Hizi siasa za watawala zetu aisee zinaboa sana, siku hizi ndio wamejua kamtindo ka kuhonga waandishi wa habari ili wawaandike vizuri, na wengine ndio wameamua kumiliki kabisa vyombo vya habari. Jamani hawa watu wanakera.
7. Mabenki: Huku nako japo asilimia kubwa ni private ila jamani kunakera, ukienda benki kama NMB yaan unashangaa, hela zako mwenyewe ila ni kero kubwa kuzifanyia transaction.
8. Makazini: Sehemu kubwa ya sehemu za kazi kumejaa kero kubwa.
9. Wizarani/ofisi za serikali: Kama una shida katika wizara au ofisi yoyote ya serikali ndio utakapojua ujinga unaofanyika huko, hawa jamaa wanaboa vibaya sana.
10. TRA: Huku kuna kero za kipumbavu sana, jamaa hawapo serious kabisa, rushwa imetawala mioyo yao. Wanaudhi sana hawa watu.
11. Umeme: Hapa ndio sina hata cha kusema.
Najua wadau mnazo kero nyingine nyingi sana, hapa tuchangie mawazo haya makero yaliyojaa Tanzania hii tunayaondoa vp ?? Mi naaimini tunahitaji system overhaul, wadau mnasemaje ?
:bump2::bump2::bump2::bump2::bump2::bump2::bump2::bump2:
 
Sasa kama matatizo yote hayo yanatupata sisi na tunayajua vizuri kwanini tusiwaambie watawala wetu sasa imetosha watupishe!!!!
 
Observer,

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Nakumbuka kulikua na thread moja hapa iliwahi kujadili "kuna faida gani ya kuwa mtanzania" manake kwa kweli kila kitu kwetu ni nongwa na ni matatizo tu...! Kila mahali ni kero, hospitali, mashuleni, makazini, TRA, umeme ni shida, maji hakuna pamoja na kwamba tuna maziwa na mito mikubwa kabisa duniani etc...!

Kweli kabisa kila mahali ni kero kero kabisa...! natamani siku nikiikimbi ehio nchi kabisa na nisirudi tena...!
 
Back
Top Bottom