Tanzania kila eneo wakazi wake wana kilio tofauti, wa Upanga wanalia na popo

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Nimeona story ITV wakazi wa Upanga wanalia na popo.

Wakazi wa Mtaa wa Sea View Upanga, Jijini Dar es Salaam, wamesema kumekuwa na ongezeko la popo katika eneo hilo hali ambayo wamedai inasababisha adha kwa wakazi wanaoishi kwenye eneo hilo.
.
Wakizungumza na ITV wakazi wa eneo hilo, wamesema licha ya watu wa maliasili kuja na kupuliza dawa lakini popo hawajaondoka.

Pale maeneo ya Palm Beach hadi Makao Makuu ya CRDB pamejaa popo. Unaweza kuhisi mti umekauka kumbe popo. Hii Nchi ina kila eneo wakazi wake wana kilio chao tofauti!
 
Wakati hao wakilia kwa popo wengine wanalia na wanyama pori kuharibu mazao yao. Tembo wamekuwa wengi tangu ujangili udhibitiwe. Tembo wamekuwa wakivamia vijiji na kuvuruga mashamba ya wakulima. Kwa uchache simba nao wapo kutishia wanavijiji kuwala, pia kuna fisi, chui na mbweha hawaachi kuleta rabsha vijijini. Kuna wanyama wengine kama tumbili, nyani, digidigi hawaachi mashamba ya wakulima salama. Vicheche nao ni wasumbufu kwa kula kuku bila kuwasaha ndege kwelea kwelea ni taabu tupu. Mwewe, vipanga hawajaacha kuku salama. Tumalize na kunguru wa mijini nao ni kero kwa udokozi wa vitu nyumbani
 
Dawa ya kufukuza popo nyumbani ni kupuliza manukato tu pale wanakopendelea kulala juu ya dari. Ukinyunyuzia hata sabuni za manukato hizi za unga wanahama. Kiboko ya yote uchome pilipili kisha we mwenyewe utoke ndani ya nyumba, hakuna mnyama wala mdudu atakayehimili moshi wa pilipili, mpaka panya na nyoka watatoka kwa kasi ya ajabu kuokoa uhai wao, Angalizo, hizi ni mbinu zangu tu nilizozijaribu kufukuza wanyama hao kwa lazima, haijapendekezwa kitaalamu
 
Mbolea ya popo ndio mbolea Bora kuliko zote
pale kisarawe karibu na kiwanda fulani kilashakufa siku nyingi inakopita reli ya mkoloni chini ya mlima kuna mapango wanaishi popo. Wananchi wa eneo hilo kijijini huwahiana kuzoa mbole ya popo kila siku na huja kuiza dar kwa viroba. Ni mbolea nzuri sana kustawisha bustani za mbogambogo, ni mbolea ya kinyesi cha popo isiyo na kemikali za viwandani
 
Kuna waumini wa dini fulani walichinjachinja mifugo mingi sana mijini. Cha ajabu wakawa si wasafi wa kutunza miji. Walichinja mifugo wakachuna, wakachukua nyama wakaacha ngozi zikitapakaa hovyo mijini ongeza na zile samadi za utumbo. Bora fisi wavamie miji ili kusafisha mitaa kwa kula ngozi zilzotelekezwa zikikaukiana na kuwa uchafu mijini. Fisi wana tabia ya ku sense iliko mizoga. Sasa kama waki sense kuna ngozi zinazagaa mijini na wakaamua kuvamia miji ili kuja kula ngozi zilizoachwa kizembe mtu asilalamike kuwa fisi wamekuwa kero kuvamia miji na kuwa tishio kwa usalama wa wananchi
 
Wakati hao wakilia kwa popo wengine wanalia na wanyama pori kuharibu mazao yao. Tembo wamekuwa wengi tangu ujangili udhibitiwe. Tembo wamekuwa wakivamia vijiji na kuvuruga mashamba ya wakulima. Kwa uchache simba nao wapo kutishia wanavijiji kuwala, pia kuna fisi, chui na mbweha hawaachi kuleta rabsha vijijini. Kuna wanyama wengine kama tumbili, nyani, digidigi hawaachi mashamba ya wakulima salama. Vicheche nao ni wasumbufu kwa kula kuku bila kuwasaha ndege kwelea kwelea ni taabu tupu. Mwewe, vipanga hawajaacha kuku salama. Tumalize na kunguru wa mijini nao ni kero kwa udokozi wa vitu nyumbani
Wana vijiji waondoke huko Temboni.
 
Back
Top Bottom