PMNBuko
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 967
- 154
Nasikitika kusema kuwa nchi yetu, licha ya kupinga tamko la Uingereza na Marekani juu ya Haki za Mashoga, tayari Tanzania iliridhia haki za Mashoga tangu 2009.
Kwa Mjibu wa Mkakati wa Taifa la Tanzania wa Kinga Dhidi ya VV/UKIMWI wa 2009 - 2012, Mkakati Na.9 (b): Kuongeza Uelewa na Kupunguza Mienendo Hatarishi Miongozi mwa Watu wenye uwezekano wa ongezeko la uambukizi wa VVU, unabainisha kuwa wanaume wanaolawitiana wana haki zifuatazo (soma ukurasa wa 35 - Huduma muhimu kwa wanaolawitiana) - nimetaja baadhi tu:
1. Kupata ulinzi wa kisheria na sera za msaada na uraghabishi.
2. -
3. Usambazaji wa vilainishi vya maji na kondomu.
4. , n.k.
Maoni yangu: Kwa kuwa Mkakati huu ni serikali ya Tanzania, na tayari unaridhia uwepo wa Mashoga na kwamba wanastahili kupewa haki za msingi pamoja na huduma muhimu kama vilainishi vya maji (kwa maana ya wakati wa kulawitiana), ina maana kwamba Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, hakukuwa na haja ya kulumbana na Mataifa ya Magharibi yanayoshinikiza nchi za Afrika kuheshimu haki za Mashoga kwani tayari tulishaheshimu haki zao tokea kuandikwa kwa mkakati huu mwaka 2009.
Kwa lugha nyingine, Serikali yetu iliridhia haki za mashoga mwaka huo wa 2009 kupitia mkakati huu. Siamini kama Membe hajasoma mkakati huu na kama ndiyo, tuna viongozi wavivu wa kusoma.
WanaJF hili mnalichukuliaje? Nawasilisha.