Tanzania iliwahi kuwa nchi ya tatu kwa upelelezi duniani

Mwanzo walisema waarabu wamekamatwa kwa taarifa za ambrose baadae wakasema wamekamatwa sababu walikua maeneo ya tukio na kama isingekua ubalozi wao kuwasaidia wangetolewa kafara bure maskini nawaskitikia FBI wao ni proffessional wameingizwa kweny mtego wa siasa hawatapata chochote!

Obama anakuja Tanzania....tafakari uwepo wa FBI nchini....!
 
hizi hekaya zinanikumbusha miaka ilee ya utotoni nilipokuwa natamani kuwa pilot kila mara ndege ilipokuwa ikikatiza ktk anga la kijijini kwetu.
 
Enzi hizo mazuzu walikuwa wengi wengi,hiyo tv tu alikuwa na sheikh yahaya na Nyerere! halafu wakawa wanawatabiria wenzao mambo ya ulimwengu kumbe wao wameona kupitia CNN,BBC!midingi ya wakati eti mtu yuko chumbani na wife anaogopa kutaja jina la Rais kwa ubaya anahisi panya aliyepo darini ni shu shu shu aliye jigeuza panya !
 
Polisi siku hizi kaka wanachukuliwa hadi form 4 leaver 2 ht km ana div 4 pnts 32 anaenda depo unategemea nn?

Kufaulu Mtihani tena mmoja siyo tija ya kumfanya mtu awe anafaa kuwa operative wa nchi yeyote ile... angalia maandishi yako kabla haujaandika..
 
Enzi hizo hatukuwa na vyombo vya habari hivyo tulidhani sisi ndio tuko juu maana wanasema motto asiyetembea kwa majirani na kuonja mapishi ya wengine huwa anadhani mama yake ndiye bora kwa mapishi kuliko wengine wote. Ukitafakari kwa kina jinsi ulimwengu unavyokwenda jiulize kwa Tanzania ni lipi lingetuweka nafasi ya tatu.
 
Labda sijui maana ya intelijensia!

  1. -Intelijensia zote duniani kipaumbele kikubwa ni kulinda rasilimali za nchi zilizopo, kulinda na kutafuta maslahi ya nchi hiyo ndani na nje. Kuhakikisha na kukagua mikataba ya nchi iliopo na itakayo sainiwa inakuwa ni kwa maslahi ya nchi na watu wake! Hii ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuitangaza kibiashara, kiutalii na kuwekezaji! Kuhakikisha raia wa nchi husika anapata kipaumbele kwa jambo lolote dhidi ya mgeni!
  2. -Ulinzi na usalama wa viongozi, raia na mali zao, mipaka ya nchi...hivi vyote ni kipaumbele cha kwanza kwa idara za kijasusi!

Tuangalie Tiss inafanyeje katika hayo ya hapo juu, ili tulinganishe na idara za nchi nyingine!
  • Inalindaje rasilimali za nchi kwa manufaa ya watu wote?
  • Inasimamia vipi mikataba ya nchi inayo sainiwa baina yetu na wawekezaji, kwa manufaa ya nchi?
  • Inafichua vipi fedha za umma zinazo toroshwa nje ya nchi na viongozi wakuu, na zile zilizomo nchini?
  • Inawalinda vipi wanachi wanaozulumiwa ardhi zao bila fidia na kupewa wawekezaji?
  • Inadhibiti vipi migogoro ya dini na ukabila inayo ibuka nchini, au ndio yenye kuiratibu?
  • Inadhibiti vipi ubora wa elimu na bidhaa duni zinazo ingizwa nchini?
  • Inasimamia vipi matumizi ya fedha za umma, safari za wakuu wa nchi, magari ya kifahari nk?

......na hata hiyo tiss ya zamani tunayo aminishwa ilikuwa kiboko...bado wananchi wetu walio wengi hawakuwa na elimu...vyombo vya habari vyote ni vya serikali......na kwa kipindi kile...adui mkubwa ni genge lenye kutaka kupindua nchi tu.....kuna taarifa kuwa mikakati yetu ya siri ya vita ilikutwa ikulu ya uganda....!

Badala yake sasa imekuwa ni idara ya kuhakikisha kundi la watu wachache (viongozi walio madarakani na wastaafu), linalindwa dhidi ya dhuluma kwa umma woote wa watanzania! Sasa idara hii imeaminishwa kuwa, yeyote anayehoji mikataba, anayehoji rasilimali za nchi, anayehoji fursa sawa kwa wote.....mtu au watu hao ni wahaini na wanatakiwa kung'olewa kucha, kung'olewa meno, kutobolewa macho na vitu vyenye ncha kali bila ganzi....ili kutishia wengine wasithubutu!

Kumbe basi, idara inawajibu kwa raia wote wa tanzania bila kujali vyama, dini kabila wala rangi!
 
Enzi hizo mazuzu walikuwa wengi wengi,hiyo tv tu alikuwa na sheikh yahaya na Nyerere! halafu wakawa wanawatabiria wenzao mambo ya ulimwengu kumbe wao wameona kupitia CNN,BBC!midingi ya wakati eti mtu yuko chumbani na wife anaogopa kutaja jina la Rais kwa ubaya anahisi panya aliyepo darini ni shu shu shu aliye jigeuza panya !
Hata sasa utakuta kuna kichaa amekwisha mbaya ameonekana mitaani miaka ishirini lakini wanaamini kwa moyo mmoja ni shushushu.any way kama ilshawahi kuwa ni miaka hiyo,siku hiz tecnologia ndio inaplay major rall siku hiz watu wanatumia bugs hadi vyooni,redio transmitars hadi kwenye miswaki baba.
 
Labda sijui maana ya intelijensia!

Kumbe basi, idara inawajibu kwa raia wote wa tanzania bila kujali vyama, dini kabila wala rangi!

Inaonesha kuwa Hujui maana ya Intelligence kwa ni vema utafute namna ya kujua kabla hauja hainisha vitu vya wongo
Any intelligence agency works for the ruler of that area(nation/state/kingdom) so they works for him and not for the people, if you don't believe, then you are free to ask anyone who knows such things..... Ndugu K.Msese haya mambo hayapo uchi kama mnavyoona.
Na kama unataka kulaumu mtu mlaumu RAISI WAKO WA JAMUHURI NA WATENDAJI KAZI WAKE.............
 
mkuu kamandawasua
Kama hiyo ndio only definition.....ya inteligence ulio mezeshwa...bora idara hiyo ivunjwa na iundwe yenye mitazamo nilioeleza hapo juu!

Naomba kukunukuu...."Any intelligence agency works for the ruler of that area(nation/state/kingdom) so they works for him and not for the people......" m.y a.s.s.

-Kwa taarifa yako...hii taasisi inatakiwa iwe huru na yenye meno......kwani hata rais wa hiyo nchi asipoendana na sera za hiyo nchi...idara hiyo humuondoa kwa kifo! Kama mashirika na idara za kijasusi za mataifa yaliyo endelea yanawapa definition uliyotoa ili mkariri...hali wao wanatuma majasusi wao katika nchi zetu za kimasikini ili watunyag'anye rasilimali zetu...na kuua viongozi waadilifu wanaotetea rasilimali za nchi zao kama kina Lumumba vs CIA, kumbe pole sasa sisi!

Idara yetu ya kijasusi tunayo itaka inatakiwa ifanye kazi kwa maslahi ya raia wake wote na sio kwa ajili ya viongozi ambao wao wamepewa tu dhamana ya kutuongoza na sio kutumiliki.......!

Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani.

Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.

Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.

Mimi naona haya ni masimulizi tu ya utotoni kama yale ya IDDI AMIN alikuwa anakula nyama za watu.
 
M
Ndugu wana bodi,wakati nikiwa mdogo enzi za mwalimu kuliwahi kuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata ikawa nchi ya Tatu kwa upelelezi duniani.

Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya ezi hizi,nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chafu ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori,lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.

Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.

Miaka ipi hiyo mkuu na kama ni kweli tatizo lilianzia wapi na miaka ipi mkuu mada inapendeza
 
Aaah CIA, MOSSAD, MI6 na FSB....kat ya hawa wanne cjaona nafas ya intelligenc agent yiyote ya africa
 
Back
Top Bottom