Tanzania hatuwezi kuendelea kwa utaratibu huu.

mikati

Member
Jan 27, 2011
9
0
Waziri wa Uchukuzi Bw Omari Nundu ameunda kamati ya kuchunguza ni kwa nini hali ya usafiri wa anga inaendela kudororora. Hili ni jambo zuri ambalo Nundu ameamua kufanya. Kamati hii inaongozwa na Mama Magret Munyagi, aliyekuwa mkuu wa usafiri wa anga kwa takribani miaka 11 hivi. Mama huyu aliongoza na kusababisha usafiri wa anga kufikia kiwango ambacho hakikuridhishi na umeamua kuunda tume. NIA YAKO MH WAZIRI NI NINI HASA?

Je watanzania mwategemea kamati hii kuleta ufumbuzi wa tatizo? Inaeleweka kuwa Bw Nundu walipa fadhila kwa Mama kwa kuwa alikuwa boss wako hapo awali alipokusitiri..Lakini huoni kuwa waendelea kudidimiza shughuli za anga? Vyombo husika husika vya kudhibiti maovu mnafanya kazi gani? Au mchanga umeingia machoni?

Mama Munyagi alihakikisha anamuachia ofisi mtu ambaye (Fadhili) ni dhaifu kuongoza ili watu waseme kuwa yeye alikuwa ni kiongozi bora. Fadhili ana msaidizi/swaiba wake anaitwa Ruhongole. Huyu Ruhongole inasadikika kuwa ni chanzo cha matatizo mengi yanayojitokeza hivi sasa ndani ya chombo cha udhibiti wa mambo ya anga (TCAA). Huyu Ruhongole nae ana runner wake - home boy wake anaitwa Vyamana. Nae ni balaa kwa hivi sasa…ameota pembe kwani boss wake anataka afanye shughuli ikiwezekana zote ndani ya mamlaka (Cha juu/10%).

Mh Nundu tangu 10 feb 2011 kule TCAA makao makuu wamekatiwa umeme na tanesco (Ruhongole & Vyamana hao)….Sasa waunda kamati ya kufanya nini? Wategemea nini kutoka kwenye kamati hii?? Kuwa kiongozi na acha usanii…
 
Back
Top Bottom