Tanzania hatuna Viongozi tuna Wanasiasa; Maisha ya Kujitakia!

Sasa wewe unataka kutuaminisha tuendelee kuwapa kura majambazi wa ccm? au unataka tufanyeje? kikubwa unachotakiwa kuelewa ni kuwa kitumike kihalali wala si kikundi cha watu wachache. ndio maana CDM inapigania huu usawa hatusemi tutakaa vijiweni tu bali maendeleo yatakuja kwa kufanya kazi tukisaidiana na serikali kupitia raslimali tulizonazo

Kama hii nchi watakao kuwa wanapata madaraka ni binadamu basi hakuta kuja kuwa na usawa leo hii mpeleke mke wako CHADEMA wakashndane na mke wa Slaa ktk post yoyote afu ndo utajua kama kutakuja kuwa na usawa au la
 
Kwa hii thread nakuunga mkono kama si mguu.
:coffee:
wanasiasa wote wanatafuta kula tu na kuiba raslimali za nchi kwa maslahi yao. Ila CCM nao wamezidisha mno kuibia wananchi lo!
 
wewe ni miongoni mwa watanzania wengi waliokata tamaaa" hawathubutu kujaribu, hawapigi kura, ukweli ni kwamba wanafanana na aliye jeruiwa na nyoka, wakiona hata mjusi wanaogopa. thread yako haitufundishi chochote!

we kweli ndo mtakamiwa, kama umeni-quote kuna sehem nimesema '' labda kikubwa ni mabadiliko kwamba CDM wanaeza wasiwe wezi SANA kama hawa wenzetu wa CCM''
 
kumbe cdm inapigania usawa na si kuchukua madaraka...hata hivyo bado sijajua usawa upi unaoongelea...kama ni mgawanyo wa rasilimali basi tuanzie ndani ya cdm.....chama mapato ni kiasi gani kwa mwezi??.mwenyekiti anapata ngapi?? muhudumu wa ofisi anapata ngapi?..kuna usawa gani??......ni usawa huu mnaopigania??

pengne hajui nini maana ya usawa ila anatumia tu hilo neno
 
systm ime corrupt lazma kutakuwa na ugumu ata kama kuna jtihada bnafc..
 
wewe ni miongoni mwa watanzania wengi waliokata tamaaa" hawathubutu kujaribu, hawapigi kura, ukweli ni kwamba wanafanana na aliye jeruiwa na nyoka, wakiona hata mjusi wanaogopa. thread yako haitufundishi chochote!

we mtakamiwa, tafuta sifa za mwanasiasa kisha pengne utakuja na wazo jipya.
 
Wewe ni gamba uliyekosa jinsi ya kutuingia ukaamua kuja kiivyo ili tuone kuwa cdm ni nothing tukiipa madaraka.Hata hivyo it show that umesoma walau shule ya kata ila tuna hasara kuwa na mwananchi kama wewe uliyekata tamaa..nchini za wenzetu wewe uliyejikatia tamaa yabidi hata ufungiwe selo usijelipua halaiki.
 
Kwa hiyo unatushauri nini wananchi? Kweli unategemea tuishi bila kuwa na imani na chama chote? Nani alikwambia kuwa cdm ni malaika?Udhaifu wa ccm ndio unafanya tukubali sera za cdm maana tuna matumaini nazo!
 
Wewe ni gamba uliyekosa jinsi ya kutuingia ukaamua kuja kiivyo ili tuone kuwa cdm ni nothing tukiipa madaraka.Hata hivyo it show that umesoma walau shule ya kata ila tuna hasara kuwa na mwananchi kama wewe uliyekata tamaa..nchini za wenzetu wewe uliyejikatia tamaa yabidi hata ufungiwe selo usijelipua halaiki.

hili nililitegemea....jibu rahisi kwa hoja ngumu ni "gamba" au "gwanda"
 
we mtakamiwa, tafuta sifa za mwanasiasa kisha pengne utakuja na wazo jipya.

inaitaji moyo mkuu. ukweli ni kwambwa hatuitaji kukata tamaa kiasi hicho. naamini tanzania ina watu wakututoa tulipo na kurejeshewa tumaini la kuishi. tatizo ni mfumo but still i see the future.
 
Wewe ni gamba uliyekosa jinsi ya kutuingia ukaamua kuja kiivyo ili tuone kuwa cdm ni nothing tukiipa madaraka.Hata hivyo it show that umesoma walau shule ya kata ila tuna hasara kuwa na mwananchi kama wewe uliyekata tamaa..nchini za wenzetu wewe uliyejikatia tamaa yabidi hata ufungiwe selo usijelipua halaiki.

sijawah kuwa sisiem na pia ni mwanachama mfu wa CDM sijailipia kadi yangu toka 2008. Pili, elimu yangu haikuhusu "appeal to people''>> attack my arguement and not me.
 
Zingatia pia kuwa nchi haiendeshwi ki ramliramli, bali kwa mipango na sera zinazoelezeka,zinazosomeka,na zinazotafitika,huu mlolongo wa maneno ya 'watakuwa/itakuwa/bila utafiti wa kutosha unaonyesha ni jinsi gani watanzania tulivyo wavivu wa kusikiliza/kusoma na ama kuelewa, kila chama kina sera ambazo ni written, kina katiba, na kina ilani yake.

Hivyo ni rahisi kwa great thinker kuelewa nini akitegemee kutoka kwa chama fulani, badala ya ku conclude kama mganga wa kienyeji anayepima ugonjwa kwa pembe la n'gombe, na hiyo ya kusubiri maisha bora huku umekaa kijiweni sijui unamzungumzia nani!? Mtanzania mwenye uelewa? Ama mvuta bange?
 
Zingatia pia kuwa nchi haiendeshwi ki ramliramli,bali kwa mipango na sera zinazoelezeka,zinazosomeka,na zinazotafitika,huu mlolongo wa maneno ya !watakuwa/itakuwa/bila utafiti wa kutosha unaonyesha ni jinsi gani watanzania tulivyo wavivu wa kusikiliza/kusoma na ama kuelewa,kila chama kina sera ambazo ni written,kina katiba,na kina ilani yake,hivyo ni rahisi kwa great thinker kuelewa nini akitegemee kutoka kwa chama fulani,badala ya ku conclude kama mganga wa kienyeji anayepima ugonjwa kwa pembe la n'gombe,na hiyo ya kusubiri maisha bora huku umekaa kijiweni sijui unamzungumzia nani!!mtanzania mwenye uelewa? Ama mvuta bange?

we ni maskini wa akili, unadhan ubora wa sera zilizo kwny makaratas bila utekelezaji ndo 2tapata maendeleo. Ktk sera, kila chama kitakuja na sera ambazo wanadhan zitawavutia wananch wake lakn tatzo ni kwny kutekeleza. Yawezekana we ndo mvuta bangi
 
Watanzania wanafanya kazi kwa bidii sana sema utawala mbovu unakatisha tamaa.kama matajiri wengi wanakwepa kodi kwa mgongo wa ccm ctegemei nchi kuendelea labda kwa miujiza.lazima ccm waondoke kwanza madarakan
 
Ni ujinga kwa mtanzania kutegemea kuwa maisha bora yataletwa na mwanasiasa, watanzania wengi wanaamini CDM ikichukua nchi kutakuwa na maisha bora hata wakiwa wanakaa kijiweni, hayo ni mawazo ya mgando yasiyo na maana. Kama CCM walivyo hata CDM ndivyo walivyo hata mkipinga kwakuwa mna mapenzi na chama lakn huo ndo ukweli, kwani hao CDM wamezaliwa mbinguni.?

Kwamuujibu wa John Locke ''man is selfish and greedy'' ni binadamu yupi asiye na tamaa?? Ni binadamu yupi atakaye kufikiria wewe kabla ya kujifikiria yeye na familia yake??. Kitu kingine... wote tunafahamu tabia ya wazungu, mzungu si mpuuzi hawezi akakupa kitu bila kuwa na maslahi na wewe, sasa kwakutumia akili ya kawaida unategemea CDM watawalipa nini OCD wa ujerumani kama si madini kama walivyofanya CCM. We unadhani nchi ikichuliwa na CDM nafasi za kazi hazitatolewa kwa undugu??

Yani wewe uombe kazi ofisi ya raisi na mtoto wa Mbowe aombe kazi ofisi ya raisi unategemea watamuacha mtoto wa Mbowe wakuchukuwe wewe?? Labda kikubwa ni mabadiliko kwamba labda CDM watakuwa sio wezi sana kama hawa wenzetu wa CCM ila kitu ambacho nataka kuwakumbusha wenzangu matumaini yako ya kimaisha usiyaweke kwa wanasiasa, wanasiasa wengi hawana maana, wamejawa na tamaa pamoja na ubinafsi.


Mkuu Simplex umeongea mengi


kwa upande mmoja ukosahihi kwa mtazamo wangu lakini 50% yapili kwangu mimi haujatutendea haki.

1. Nikweli maendeleo ya kila mmoja huletwa na mtu mwenyewe, kwa kufanya kazi kwa bidii kutafuta akijituma kupitia njia halali za kujipatia maisha bora, hili sina ubishi nakubaliana na wewe

2. Ili mtu binafsi afanye maendeleo yake na kuwa na tija pia kwenye maendeleo ya taifa serikali inahusika sana.

Utafanya kazi kwa bidii na moyo safi endapo serikali itakujengea mazingira mazuri kimkakati

a) Utafanyaje biashara ukianza na mtataji mdogo usafili nafuu wa reli za kati na Tazara kwa mfano zimefisadiwa ilikuwezesha watawala na familia zao, na jamaa zao kufanya biashara za usafilishaji mizigo kwa malori. Wamefisadi hata shirika la ndege kiasi kwamba tunaendeshwa na precision as if wanafedha zaidi ya serikali, sinatatizo na precision kujiendesha tatizo ni kwa nini serikali ishindwe kiasi kwamba raia wanataabika? (matokeo mfumko wa bei mitaji midogo inatekea na waachia hasira raia kwa serikali yao)


b) Huwezi fanya kazi ukiwa na afya mgogoro, kumbuka tunaongelea watanzania masikini ambao ndo wapiga kura wengi na wanaoteseka na hizo siasa ulizofafanua hapo juu. Matibabu hakuna, madakitari hakuna .......watjajiendelezaje hawa?


c) Huwezi kufikiri vizuri na kwa mahesabu mazuri kufanya ushindani katika dunia hii ya utandawazi endapo hata elimu ya darasa la saba watoto wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika kwa asilimia kubwa tu. (Je hili tunalitatuwaje as individuals who own nothing)


d) Huwezia pia kufanya kazi kwa bidii ukiwa na njaa, wala hujui kesho itakuwaje kilasiku afadhali ya siku ya jana (unatambua kwamba siasa za kilimo kwanza, kilimo ni uhai, Jembe ni mali zinaishiga majukwaani ???) - tunahitaji watakaozifanya kwa vitendo ili watanzania mmoja mmoja aweze kupigana na maisha)


Mambo yote hapo juu yanahitaji uongozi bora kwa maana ya usimamizi wa miuondombinu kwa maana ya watanzania mmoj mmoja kuweza kufanikisha shughuli zao za uchumi.

Hatuhitaji serikali ituwekee manoti mifukoni mwetu, bali tunataka ijenge mazingira mazuri yatakayomfanya mtanzania anaejituma kuweza kufikia malengo ya maisha bora. Hapa ndipo tunapotaka kujaribu na wengine kama akina cdm nccr cuf nk


Serikali imejaa wezi, kwanza wanatukata kodi kubwa kupita kiasi na hasa pay as you earn nk, wanakwiba madin ovyo ovyo, huduma mbovu za afya watu wanakufa ovyo mahospitalini, barabara, reli na viwanja vya ndege ovyo kabisa, mishahara duni kwa walimu ambao nao wanatukomesha kwa kufanya mgomo baridi, tutaendelea kuwa taifa la wajinga aslan siku zote, unafukuza madakitari unategemea kitu gani wewe?

Hitimisho, 50% za kila mtanzania kujipigania maisha zitakuwa na maana endapo zile 50% za serikali zitakuwa zimekamiliak au walau 30% uwezeshaji na mazingira bora kwa watanzania kufanikisha hicho ulicho kiainisha as individuals.


TUNAHITAJI CHAMA KINGINGINE KUTUJENGEA MAZINGIRA BORA YA MIUNDOMBINU, ELIMU, AFYA NA UWAJIBIKAJI. TAFAKALI CHUKUA HATUA, HUJACHELEWA.
 
Mi na kubaliana na wewe ktk jambo moja kuwa maisha bora hayawezikuletwa kwa kukaa vijiweni.ninapingana na wewe kwa kuiweka ccm na cdm kwenye chungu kimoja.Eti kwa vile ccm wameshindwa kuleta maisha bora basi na cdm hawawezi.Huwezi ukawapima wanafunzi walioingia darasani wakafundishwa kwa kuwapa mtihani wa aina moja na wanafunzi wanaotarajia kuingia darasani ili wafundishwe halafu ukategemea kupata matokeo ya aina moja.ccm wamepewa madaraka wameshindwa kuwaletea maisha bora wtz.cdm bado hawajapewa madaraka.ili uweze kupata kitu bora au dhaifu lazima kilichopo kiondolewe.wtz watajiletea maendeleo wao wenyewe kwa kufanya kazi watakapo wapata viongozi bora ili zana za kilimo zipatikane waweze kulima,barabara zitengenezwe wasafirishe bidhaa zao,masoko yapatikane,kile kitakachopatikana kilindwe na si kukiiba n.k.
 
Kwa hiyo unatushauri nini wananchi? Kweli unategemea tuishi bila kuwa na imani na chama chote? Nani alikwambia kuwa cdm ni malaika?Udhaifu wa ccm ndio unafanya tukubali sera za cdm maana tuna matumaini nazo!

Mheshimiwa ruttashobolwa.....kazi ya mwanasiasa yoyote ni kutia matumaini. tulitiwa matumaini sana mwaka 2005.. lakini kwa sababu matumaini yalikuwa ni ya kisiasa hata majibu yake leo tunajibiwa kisiasa. Wanasiasa wote ni wamoja awe ametoka Lumumba au Mtaa watogo au Buguruni wote ni wamoja...WANASIASA...WATIA MATUMAINI
Labda kungekuwa na chombo fulani cha kuwadhibiti katika kutekeleza ahadi/sera/matumaini waliyoyatoa kwa wananchi. Sidhani kama ahadi ni neno zuri sana... nadhani MAJUKUMU lingefaa zaidi.
Na haya majukumu yawe ndio mkataba wa kazi kati ya mwanasiasa na mwananchi. Kwa mfano kama mwanasiasa ameahidi kujenga zahanati lazima tukubaliane ujenzi utachukua muda gani na fedha za ujenzi atazitoa wapi (yumkini hutoka kwenye kodi zetu) kwa hiyo ndani ya miaka 5 aigawe hiyo kazi katika vipindi vidogovidogo hadi tujue ndani ya mwezi mmoja wa kwanza kazi itakuwa imefikia kiwango gani.. na kama itakuwa haijafikia basi kwa kupitia hicho chombo cha kuwadhibiti wanasiasa tumfukuze kwenye nafasi yake na ili tusipoteze pesa za walipakodi basi aliyepata nafasi ya nyuma yake kwenye uchaguzi achukue nafasi yake.... naya akiboronga pia tumtimue na kisha tusiwaache bure tuwafungulie mashataka ya uhujumu uchumi..... tukifanya hivyo nadhani wengi watarudi kwenye fani zao za uzalishaji mali
Miaka 18 na kuwa na akili timamu pekee kuwa ndiyo kigezo cha kupiga kura nadhani hakitoshi labda kwasababu kupiga kura ni JAMBO MUHIMU maana ni kama unafanya maamuzi hatima yako ya maisha ya baadaye. Kungekuwa na namna ya kupima uelewa wa mtu kabla ya kupiga kura... uelewa ambao mtu akiambiwa kama ukituchagua sisi bei ya sukari itakuwa shilingi 300 haushangilii ila unajiuliza bei itashukaje? na utashangilia pale utakapo pewa maelezo ya kueleweka jinsi bei itakavyoshushwa hadi kiasi hicho...hakuna maana ya kushusha bei ya sementi kisha gharama yake ikahamishiwa kwenye mabati... bei ya mabati ikawa maradufu.. Cha msingi hapa ni kujua jinsi ya kudhibiti bidhaa za msingi kama nishati (umeme, mafuta, gesi nk.) .. uzalishaji wa ndani, ununuzi wa bidhaa za nje nk
Kama tukiendelea na mfumo huu ambao tunauita demokrasia...yaani wengi wape basi kukiwa na kundi kubwa la wasio na uelewa basi maamuzi mengi tutayafanya kama watu wasio na uelewa......
 
SIMPLE X
Kama CCM walivyo hata CDM ndivyo walivyo hata mkipinga kwakuwa mna mapenzi na chama lakn huo ndo ukweli, kwani hao CDM wamezaliwa mbinguni.?

Mkuu, hakuna mtu anafikiria kwamba CCM ama CDM itagawa fedha kwa wananchi wake. Sera za vyama vya siasa ndivyo zinaweza kuleta matumaini kwamba vinatoa fursa ya watu kujiletea maendeleo yao au hapana. Sasa CCM haitoi hizo fursa kwa sababu ya sera zao (wameacha zile za Nyerere za Ujamaa na kujitegemea) na wamekumbatia uwekezaji usiolipa kodi wala mgawanyo uliosawa wa rasilmali kati ya nchi na wawekezaji hao pamoja na ufisadi. Kuna mwanazuoni mmoja aliwahi kuandika kuhusu "Planned Poverty" yaani "ufukara wa kujipangia". Ufukara wa Mtanzania si kwamba yeye ni mvivu, hapana, ila anapangiwa na watawala awe fukara kwa makusudi kabisa. Unaweza kumfukarisha mtu na akakupenda na kukuamini (kama Nyerere alivyopendwa). Sharti kubwa usiwe fisadi. Lakini usitegemee kumfukarisha mtu na papo hapo ukawa fisadi (kama CCM ilivyo sasa baada ya kukiri u-gamba na kushindwa kujivua) na kulaani kama mtu unayemfukarisha akuchukia na kukuona muongo. Hili la amani na utulivu linatoka wapi? Kwa nini TANU ilidai uhuru wakati hakuna wakati Tanzania ilikuwa na amani na utulivu zaidi ya wakati wa mkoloni? Tunaanza kumkumbuka Nyerere tutake tusitake!
 
Back
Top Bottom