Tanzania haiwezi kuendelea kwa sababu Makanisa na Misikiti ni Mingi sana kuliko idadi ya Viwanda, Hospital na Shule

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Huu ni ukweli mchungu.

Hakuna Taifa lililoendelea kwa kuweka mbele dini kuliko viwanda.

Hata Saudi arabia wanaendelea sababu dini kwao ni biashara inayochangia pato lao la taifa matrilioni ya hela. Wanafurahi sana kuona watu wengi wanaenda kuhijj kwao. Hela za visa, hela za hotel kule, flight fees airports. Zinawapa mahela hivyo unaona Saudi wana haki kabisa ya kuipenda dini yao maana ina faida sana kwenye uchumi wa nchi yao.

Saudi Arabia kuna wizara ya Hijja kabisa kwenye serikali yao. Sababu wanapiga hela za wataliii wa kidini.

Vatican na wao hivyo hivyo.

Sisi Tanzania ili tuendelee lazima tupunguze idadi na nguvu ya kujenga nyumba za ibada.

Kama tunavyochangishana kujenga makanisa kwa kushikana mashati kwenye Jumuia. Tunapaswa tuchangishane kujenga viwanda.

Ardhi ipo kubwa haitumiki inafaa kujengwa viwanda vya kila aina..

Rasili mali watu ipo kibao haina ajira inashinda vijiweni kubishana Simba na Yanga , Diamond na Ali kiba, Hamissa Mobetto na mabwana zake.

Tukijenga viwanda ndio tutaendelea.

Ushauri wangu Makanisa na misikiti yote igeuzwe viwanda.

Kila kata kubaki na msikiti mmoja tu na kanisa moja tu la kuzugia
 
Attachments

  • Screenshot_20240113-154552_Gallery.jpg
    Screenshot_20240113-154552_Gallery.jpg
    67.6 KB · Views: 6
Sijasoma post yote lakini mkuu kumbuka watapata wapi hizo sadaka wasipo jenga masinagogi?

Dini yangu haina hizo mambo za majengo ya kitawala
 
Huu ni ukweli mchungu.

Hakuna Taifa lililoendelea kwa kuweka mbele dini kuliko viwanda.

Hata Saudi arabia wanaendelea sababu dini kwao ni biashara inayochangia pato lao la taifa matrilioni ya hela. Wanafurahi sana kuona watu wengi wanaenda kuhijj kwao. Hela za visa, hela za hotel kule, flight fees airports. Zinawapa mahela

Saudi Arabia kuna wizara ya Hijja kabisa kwenye serikali yao. Sababu wanapiga hela za wataliii wa kidini.

Vatican na wao hivyo hivyo.

Sisi Tanzania ili tuendelee lazima tupunguze idadi na nguvu ya kujenga nyumba za ibada.

Kama tunavyochangishana kujenga makanisa kwa kushikana mashati kwenye Jumuia. Tunapaswa tuchangishane kujenga viwanda.

Ardhi ipo kubwa haitumiki inafaa kujengwa viwanda vya kila aina..

Rasili mali watu ipo kibao haina ajira inashinda vijiweni kubishana Simba na Yanga , Diamond na Ali kiba, Hamissa Mobetto na mabwana zake.

Tukijenga viwanda ndio tutaendelea.

Ushauri wangu Makanisa na misikiti yote igeuzwe viwanda.

Kila kata kubaki na msikiti mmoja tu na kanisa moja tu la kuzugia
Misikiti na makanisa vinazuia nini kuwa na maendeleo??

Hizo shule nyingi zilizopo zina misaada gani kwa taifa zaidi ya kuwafundisha ujinga vijana (kukariri ujinga na utegemezi wa ajira)

Tatizo sio misikiti wala kanisa, ndio maana umetoa hoja ya Saudia ukajaribu kutolea maelezo ya uongo.

Shida ipo kwenye mindset zetu kuanzia raia hadi viongozi.
 
Maelezo yapi ya uongo kuhusu Saudi Arabia ?

Kwamba hija haina mchango kwenye uchumi wa saudi arabia
 
Attachments

  • PiFwUuQ-stzDOnFoEWcVG-zLy1EpolnuDEdTHbm2XRI(1).JPG
    PiFwUuQ-stzDOnFoEWcVG-zLy1EpolnuDEdTHbm2XRI(1).JPG
    63 KB · Views: 7
Misikiti na makanisa vinazuia nini kuwa na maendeleo??

Hizo shule nyingi zilizopo zina misaada gani kwa taifa zaidi ya kuwafundisha ujinga vijana (kukariri ujinga na utegemezi wa ajira)

Tatizo sio misikiti wala kanisa, ndio maana umetoa hoja ya Saudia ukajaribu kutolea maelezo ya uongo.

Shida ipo kwenye mindset zetu kuanzia raia hadi viongozi.

Wenzako wanafaidika kiuchumi kupitia dini. Wanapiga mapesa tu watu wanavyoenda kuhiji
 
Attachments

  • Screenshot_20240114-105716_Firefox.jpg
    Screenshot_20240114-105716_Firefox.jpg
    242.5 KB · Views: 6
kama misikiti ikigeuza kuwa viwanda hakika Zenji itakuwa na viwanda Kila baada ya nyumba kumi, na Mbeya kula nyumba itakuwa na kiwanda

Hapo ndipo maendeleo ya kweli yatapatikana.

Hakuna nchi iliyoendelea kwa kuweka maombi na ibada mbele.. maombi hayakuzi uchumi wala kuleta maendeleo
 
Tanazania imejaa wapumbavu wengi sana,

Hiyo misikiti na makanisa inazuia vipi viwanda visijengwe? imemaliza ardhi yote kiasi kwamba wawekezaji wamekosa maeneo?

Hivi hayo makanisa na misikiti yamejengwa na serikali? na kama watu wameamua kujenga majengo yao ya ibada unataka serikali iwakataze? then wakuabudu wewe?

tutoke huko tuje kwa hao waarabu na na hija.
unadhani na hao waarabu wa leo walikaa kikao na kusema tujenga hili kaaba kwa ajili ya watu waje kila mwaka ili tufanye biashara ama kivutio cha utalii.

Hiyo KAABA imejengwa na Ibrahim ambaye hakua mwarabu kabisa, alitoka huko Iraq, sasa hebu tujiulize hao wa Iraq wananufaika vipi na hiyo ibada.
 
Data zinabishwa kwa data. Sio stori za madrassa na sunday school.

Tunaongelea leo hii dini zinafaida kwa nchi zinazoingiza hela kwa kutumia dini.

Na nikatoa mfano saudi arabia... wewe unaleta stori za kufikirika ulizohadithiwa Madrassa

Facts hizo hapo attached
 
Attachments

  • PiFwUuQ-stzDOnFoEWcVG-zLy1EpolnuDEdTHbm2XRI(1).JPG
    PiFwUuQ-stzDOnFoEWcVG-zLy1EpolnuDEdTHbm2XRI(1).JPG
    63 KB · Views: 5
  • Screenshot_20240114-105716_Firefox.jpg
    Screenshot_20240114-105716_Firefox.jpg
    242.5 KB · Views: 5
Data zinabishwa kwa data. Sio stori za madrassa na sunday school.

Tunaongelea leo hii dini zinafaida kwa nchi zinazoingiza hela kwa kutumia dini.

Na nikatoa mfano saudi arabia... wewe unaleta stori za kufikirika ulizohadithiwa Madrassa

Facts hizo hapo attached
nishakwambia hiyo AL KAABA hao waarabu unaowaona leo hawakuijenga wao, wenyewe wamaeikuta, sijui unanielewa?

hivyo suala la kupiga hela kwa waarabu ni suala ambalo exceptional.
 
Huu ni ukweli mchungu.

Hakuna Taifa lililoendelea kwa kuweka mbele dini kuliko viwanda.

Hata Saudi arabia wanaendelea sababu dini kwao ni biashara inayochangia pato lao la taifa matrilioni ya hela. Wanafurahi sana kuona watu wengi wanaenda kuhijj kwao. Hela za visa, hela za hotel kule, flight fees airports. Zinawapa mahela

Saudi Arabia kuna wizara ya Hijja kabisa kwenye serikali yao. Sababu wanapiga hela za wataliii wa kidini.

Vatican na wao hivyo hivyo.

Sisi Tanzania ili tuendelee lazima tupunguze idadi na nguvu ya kujenga nyumba za ibada.

Kama tunavyochangishana kujenga makanisa kwa kushikana mashati kwenye Jumuia. Tunapaswa tuchangishane kujenga viwanda.

Ardhi ipo kubwa haitumiki inafaa kujengwa viwanda vya kila aina..

Rasili mali watu ipo kibao haina ajira inashinda vijiweni kubishana Simba na Yanga , Diamond na Ali kiba, Hamissa Mobetto na mabwana zake.

Tukijenga viwanda ndio tutaendelea.

Ushauri wangu Makanisa na misikiti yote igeuzwe viwanda.

Kila kata kubaki na msikiti mmoja tu na kanisa moja tu la kuzugia
Mkuu Freshman,the bittertruth you said itawaumiza wengi sana,ila kihualisia Africa inahotaji maendeleo ya technology zaidi ya theology.

Maana nchi nyingi ambazo hazina Ukristo wala Uislamu Zina maendeleo sana na mungu hawapi adhàbu yoyote,si kwamba mungu hayupo,mungu yupo ila si huyu wa Wakristo na WA Islam.

North Korea ukikutwa na bibilia au Quran adhàbu yake ni kifo,nchi kama Japan,China,laos,Bhutan, Armenia,North Korea etc. Hazina Uislamu Wala ukrisato na ndo matajiri,na asilimia 95% ya magari tunayotumia yanatokea nchi isiyokuwa na dini,Japan,kwann mungu asingetupa sisi tunaokesha misikitini na makanisani?
 
Wafia dini hawatakuelewa

Hapa mtaani kwangu nimezungukwa na misikiti miwili, yaani nikiamua kwenda wowote ule haitazidi dakika 10 nitakua nimefika lkn naona kuna msikiti mwingine mpya unajengwa.

Ile miwili iliyokuwepo haijai labda iwe siku ya swala ya Ijumaa au Sikukuu za Eid lkn bado tunachangishana kujenga msikiti mwingine wa tatu.

Inshort hizi nyumba za ibada ni kama biashara za watu, Mtu akishasoma elimu ya dini akaielewa anatamani awe na kanisa au msikiti wake. Ndo maana Kila siku yanaongezeka hata kama hakuna ulazima
 
Back
Top Bottom