HT
JF-Expert Member
- Jul 29, 2011
- 1,897
- 414
tujitoe tu kwenye hilo dudu CW. Kwani sisi bado tupo chini ya malkia?Mh Membe leo amekutana na waandishi wa habari kutujulisha yaliyojiri kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola uliofanyika huko Australia hivi karibuni. Mh Membe ametoa tamko dhidi ya kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Uingereza ya kutishia kusitisha misaada ya kiuchumi kwa nchi za Jumuiya ya Madola zinazopinga suala la mahusiano ya watu wa jinsia moja.
Mh Membe amesema Katiba ya nchi inatambua familia kwa maana ya mahusiano ya kijinsia kati ya mume na mke na si vinginevyo. Amesema pia jadi na utamaduni wa Watanzania unaruhusu uhusiano wa mwanaume na mwanamke tuu na si vinginevyo. Mh Membe amesema Tanzania haikubaliani kwa namna yoyote ile na kauli ya Cameron na kwamba tutakuwa tayari hata kujitoa kwenye Jumuiya ya Madola kama Uingereza itashinikiza Tanzania itambue mahusiano ya watu wa jinsia moja.