NakuliliaTanzania
JF-Expert Member
- Sep 24, 2007
- 555
- 7
- Thread starter
- #21
Mkuu, sababu ya mimi kuulizia hili ndo hiyo...nilipenda nijua..na possibly wengine wajue..je ni mkakati wa kuongeza mauzo? uhuru wa kupata habari huo....sidhani kama kuna ubaya walau tukajua kuwa sasa wamebadili mbinu..ili nijue kuwa nikitaka kusoma Tanzania Daima, nalipata muda gani kwenye mtandao!NI kwa sababu hiyo basi magazeti kama Tanzania Daima na Raia Mwema na MwanaHalisi ambayo yanategemea zaidi mauzo kuliko matangazo ya biashara yanajikuta yanabadili mkakati wa kupata fedha na siyo suala la uzembe.
Unazungumzia waliopo nchi zilizoendelea....well,, walioko huko hawana uwezo wa kupata hard copies otherwise sidhani kama ingekuwa tatizo kununua mkuu!
Hakuna kitu cha dezo na mambo ya ujamaa yalipita zamani. Tunaishi katika nchi ya kibepari na katika mfumo huu wa kibepari kinachopendwa na maximization of profit and individual success. Kama kuwahisha gazeti online kunapunguza mauzo ya magazeti mitaani what do you do? The answer is very clear.
Mkuu mi nadhani hapa tukiingiza suala la 'udezo' tutafika siko....kama nilivosema....I just want to know if that is the case..na sio suala la dezo...mfano hapa JF..watu wanakuja wanatoa mawazo maoni hoja etc...wanalipia? hawalipii..guess what? ni kwa namna gani JF imechangia kubadili hali ya mambo hususan ufisadi nyumbani? hata msomaji ambaye si mchangiaji, anabadilika kifikra kwa kusoma hapa JF...na nikikunukuu msemo wako mahiri wa 'mapambano ya kifikra....ndipo tunapotegemea ushindi zaidi..wa kifikra.
kwangu mimi gazeti kama Tanzania daima ni sehemu ya mapambano hayo! kama linasomwa na watu wengi, the better..manake ujumbe unakuwa unafika...sasa ukisema ni suala la kuzoea 'dezo' mkuu that sounds a bit offensive!
Ndipo hapo tunaingia sisi wengine ambao tunajaribu kutengeneza mtandao wa habari kuweza kuleta habari za leo leo hii, na habari za sasa sasa. Guess what?
Do we get support? no.. watu wanataka dezo. Tunajaribu kuweka mtandao wa kutuletea habari kwa kadiri zinavyotokea lakini hao waleta habari wafanye kwa dezo kama kutoa sadaka kanisani? Linapotokea tukio mahali waende kwa nauli ya nani na watakapopata mahali pa kutumia intaneti cafe walipie kwa fedha zipi?
anzisheni na nyie vyombo vyenu vitakavyoweza kufanya kazi kwa kujitolea kuleta habari 24 hours, no delay, no complains and see how easy it is.
Na suluhisho sio 'kuanzisha vyombo vyetu' vya kujitolea...ukweli ni kuwa unapoingia kwenye biashara, iwe ya habari au nini. lazima uangalie hali ya soko kama je, unaweza kuhimili mikikimikiki ya ushindani? kwa sababu sasa hivi vyombo vya habari ni vingi na kila kimoja kinatafuta nafasi kwneye soko....so kwa sisi hatuwezi kuingia huko...lakini wapo wanaoweza kuingia huko na kutupa habari!