Tanzania and Kenya the last Victim of Kivu Republic plan

kibarango

Senior Member
Sep 6, 2014
146
308
Kinachoendelea katika majimbo ya Kivu na Ituri huko DRC ni mpango wa muda mrefu wa kuanzisha Jamhuri ya Kivu ambapo maslahi ya Tusti yatalindwa.

Mpango mkuu unatajwa ni kuwa na sauti kuu ya kutawala na kuamrisha mataifa yote ya maziwa makuu.

Rwanda ndiyo Moyo wa Tusti kingdom. Kagame anajiona ndiye mbeba maono haya ya kutawala maziwa makuu. Akiwa na Godfather wake Mseveni

Mpango wenyewe.
Kuanzisha Kivu Republic ikikamilika basi kwa ushawishi wa mataifa manne. Uganda, Rwanda Burundi na Kivu basi Tz na Kenya zitakua mateka wa kisera na umoja huu wenye nguvu.

Umoja huu utaweza kuingilia Sera za Tz na kuvuruga kiasi cha kuweka watawala ambapo ni pandikizi na mateka wao. Ikifika wakati huo Tz itakua yatima na haitakua na uwezo wa kubishia muungano huo. Maana watakua na nguvu kubwa kijeshi na uchumi.

Mtu atasema mbona Burundi kuna Hutu dominance, nakujibu hiyo ni kwa muda tu. Burundi haita tulia kamwe, Kwa sasa ni kwa kua frontline ni Kivu hivyo Burundi imewekwa kiporo. Ndayishimiye pia ameamua kutoingilia maslahi ya Tusti huko DRC hiyo haonekani kama threat.

M23 hawana sababu ya msingi kuanzisha vita. Lengo kuu ni kuleta taharuki na kuhujumu Serikali ya DRC. Utaona wakati wote wakitulia hua na Amani maeneo hayo. Wakirudi vurugu na mauji kwa watusti huibuka.

Wanataka kutuma vita na mazungumzo ya Amani kipata makubaliano ya kuingizwa katika jeshi ili baadae wapange vita ingine, wale walio ndani ya jeshi la DRC ndiyo hua asset ya kuhujumu jeshi la DRC frontline.

That's why Tchisekedi hataki mazungumzo kwani kwenye mazungumzo demand yao huwa wapewe vyeo jeshini. Ni wakipewa huanza plan ya wimbi njingine la uasi na mara zote hua kubwa zaidi ya la kwanza.

Hutumia vyeo vikubwa wanavyovipata kwenye mazungumzo kujiposition zaidi Kwa wimbi linguine la vita.

Watusti wataendelea na vita hizi huko Kivu mpaka pale watakapoona wasaa Bora wa kusema dhima yao kuu ya kutaka nchi huru ya Jamhuri ya Kivu.

Note. Watusti ni chini ya asilimi moja ya watu wote wa Kivu na Ituri. Sasa watu hawa wachache hivyo wanapata ndoto ya kutawala wengine.

Wakilegezewa wataweza.

Wazungu 500 walitawala Nigerian Million 30. Mwaka 1900. Bye
 
 
Hizi stori tu mara Bahima empire mara Kivu republic ni story kama story nyingine tu,eti itakuwa na na nguvu kisera,kiuchumi na kijeshi kwa nini hao magodfather wa mpango huo hizo nguvu zisionekane kwenye nchi zao wanazozitawala sasa..wewe unafikiri Kagame hapendi Rwanda kuwa na nguvu ya kiuchumi,kijeshi na kisera!?
 
Story za kufikirika sana,hao Kivu republic nguvu za kiuchumi na kijeshi watazitoa wapi?
Hv Kagame na Mseveni wakifa kesho,huo Mpango utakuwepo?
Kwanza Kagame na RPF/A kuitawala Rwanda,ilikuwa kibahati bahati tu,Habyarimana asingeuawa,history ingekuwa tofauti sana
 
Story za kufikirika sana,hao Kivu republic nguvu za kiuchumi na kijeshi watazitoa wapi?
Hv Kagame na Mseveni wakifa kesho,huo Mpango utakuwepo?
Kwanza Kagame na RPF/A kuitawala Rwanda,ilikuwa kibahati bahati tu,Habyarimana asingeuawa,history ingekuwa tofauti sana
Unajua Nani alihusika kumuhua??!
 
Haka kaukanda tupo weak sana kweny fitna za kiintelligensia. Kagame hatakiwi kuendelea kuwepo madarakani. And i wonder nan aliruhusu rwanda kuingia kwenye jumuiya ya afrika mashariki. Ilipendeza tubaki watatu vile vile, yn kenya, uganda na tanzania.
Ukweli ndiyo huo.
 
Habari kama hii iliwahi kuwa Makala katika gazeti la RAI mwanzoni mwa miaka ya 2000. Tena iliandikwa kiuchunguzi kwelikweli ikiwahusisha hao wababe wawili.
Kama nina kumbukumbu nzuri, hata ramani ya hako ka-nchi kalioneshwa.
 
Back
Top Bottom