Tanroad mnafeli wapi? Daraja siku 3 bado halipitiki?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Tuseme ukweli wizara ya ujenzi imepwaya sana pamoja na tanroad.

Pia sidhani kama tuna engineers wenye uwezo wa kutoa solution za haraka na zenye mashiko maana kazi ya engineer sio kupiga chepe bali ni kutoa solution za kihandisi na kisayansi kutatua matatizo kwa muda muaafaka.

Kama anavyo sema waziri mkuu ni aibu ya nchi siku 3 hakuna suluhu ya magari kupita kati ya dodoma na morogoro.

Kwanini baada ya daraja kuvunjika kusitafutwe njia mchepuko magari yapite wakati mnaendelea kutengeneza daraja?

Daraja hilo halihitaji kutengenezwa kama la muda inabidi litengenezwe la kudumu penhine bora kuliko lililokuwepo.

Mmeng'ang'ania kufukia kifusi na mawe ambayo mvua ikinyesha tena vitaobdolewa au daraja kutitia.

Inaonekana tanroad na wizara ya ujenzi hawaja jipanga kwenye majanga kama haya au kwa vile kamanda wenu JPM kapata kazi nyingine.

Nakumbuka kuna mwaka alillala site hapo morogoro hadi daraja likakamilika kwa wakati huku magari yakiendelea kupita.



Mapendekezo

1. Kwa mkoa wa morogoro Tanroad wabadilishe calvert za kutoka pipe culvert na kuweka box culvert au bridge culvert kwa madaraja yote ya mkoa wa morogoro.


2. Regional engineers wasimamiwe vizuri maana wengi hawayembelei barabara. Unakuta barabara ina shimo kubwa na lipo hata kwa miezi 6 wakati fedha za ukarabati zimekaliwa na engineers.


3. Kiundwe kikosi cha emergence kwa ajili ya majanga kama haya.


Nimekuhurumia sana eng kamwele unafanya kazi na watu wazito kuchukua maamuzi na wasio na ubunifu kwenye kazi zao.

IMG-20200302-WA0059.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea point, na kitu kizuri zaidi, ume kosoa na kutuoa mapendekezo yako, tofauti na watu wengi, hii ni aibu kwa wahandisi wetu na wahusika wore, hii barabara ni muhimu sana kwani inaunganisha kanda mashariki na kanda za kati, ziwa, magharibi na nchi za mipaka ya magharibi/kasikazini magharibu.
 
Mimi bado sielewi kuwa liliporomokaje?. Hakuna gari lililotumbukia ndani?. Je ilikuwa muda gani lilipoporomoka?.
 
Ni kwamba culvert lilijaa tope maji yakaanza kupita juu. Kumbuka haya maculvert yamejengwa zamani sana. Pia inawezekana eneo lilisha anza kubomoka ila wakwa wanachukulia poa.

Kuna kitu ambacho hakipo sawa kwa engineers wa tanroad.

Nchi za wenzetu barabara muhimu kama hizi wanashika private contractors ili iwe rahisi kuwawajibisha.

Mimi bado sielewi kuwa liliporomokaje?. Hakuna gari lililotumbukia ndani?. Je ilikuwa muda gani lilipoporomoka?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hili ndio daraja la kwanza kusombwa nafikiri kila ikitokea hatua za dharura huchukuliwa kwa haraka sana na hao hao unaowaponda hata jeshi wapo kwa mambo hayo!
 
Yaani hapo wala hilo hapo nafikiri from my layman knowledge halikuwa daraja bali wataalamu tunaita Ni culvert na inaweza kuwa ilikuwa ni concrete(pipe,or box culvert,precast/insitu , amco ( those with like round pipe corrugated iron sheet, with single or multiple cell options based on 50/100 yrs optimal rainfall return ambayo huwa yatumike kupata arrive kwenye dimensions za culvert au daraja zitakazo kuwa muafaka kupitisha salama maji ya mto...Naona rainfall intensity history info ya eneo waliyoitumia kudetermine size za culvert iliwa misslead.. hivyo ndoa madhara kama hayo hutokea... culvert size kushindwa kupitisha maji mengi kwa haraka..a big lesson..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana tumeshauri wabadilishe watumie bridge culvert.

Mfano mzuri ni jinsi estim alivyo jenga pale mbezi kibanda cha mkaa ambapo kukua na pipe culvert na miaka yote maji yaoikua yanapita juu na mara nyingine yanabomoa


Tatizo engineers wetu nadhani hawaoni mbele wanaangalia kumaliza kazi.
Kwani hili ndio daraja la kwanza kusombwa nafikiri kila ikitokea hatua za dharura huchukuliwa kwa haraka sana na hao hao unaowaponda hata jeshi wapo kwa mambo hayo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Gen Mabeyo keshatia timu, PM katika tu site la kwanza kamfutakazi meneja wa tanroad, Hadi muda huu magari yameshaanza kupita
POLENI SANA WAHANDISI NA WATAALAM WENGINE MNAOBURUZWA NA WANASIASA WAPENDA SIFA, NA WANAOZIDHULUMU NAFSI ZAO WENYEWE, WA AWAMU HII YA TANO!
 
Taaluma ya ujenzi ni pana sana kuliko watu wanavyoichukulia; uwepo wa wahandisi pekee pasipo kuweko na sera zinazompa nguvu mhandisi ni kazi bure!

Tanzania ina wataalam wabobezi wa ujenzi lakini Hatusikilizwi kabisa, wanasiasa wame-dominate field nzima ya ujenzi kiasi cha kuifanya isikue.

Kwa taaluma yangu niliyoipata China katika masuala ya ujenzi, Daraja la Kilosa halikutakiwa kuzidi masaa 6 liwe limejengwa upya.

Teknolojia inayotumika na nchi yetu kushughulika na Emergency Construction ni ya kizamani sana!

Tutawalaumu bure wahandisi wetu. Tatizo kubwa katika sekta hii nchi yetu haina sera nzuri za ku-hold wabobezi nguli wa ujenzi katika system kwasababu za kisiasa.

Na ikitokea mtaalam ukajitoa kuitumikia nchi unaonekana kama boya mwenye kiherehere utakwamishwa kila hatua na automatically mfumo utakushusha, either ufanane nao au utolewe kafara (yapo mengi ya kusema yanayokera kimfumo)

Ujenzi wa dharura unafanywaje?
Kila makao makuu ya mkoa au wilaya walipaswa kuyajua madaraja yote hususani yasiyo na njia mbadala na kuyaandalia pre casted beam, piers and slab, ambapo kukiwa na dharula inakuwa rahisi kubeba na kuzipeleka site na kuziunganisha ili kupata span inayotakiwa!

Temporary platform kwa daraja kama la Kilosa hazikutakiwa kuzidi hata masaa 4 ziwe tayali zipo site! (kikao cha maamuzi kama hayo Wahandisi wa mkoa walipaswa kufanya hata kwenye simu tu Call conference!. Maandishi yanakuja baadaye watu wakiwa site. Nguvu iliyotumika kupeleka wanasiasa site kwa helikopita ingefaa kubeba "Portland Cement"

Ni aibu kwa barabara inayounganisha inchi zaidi ya nne kufungwa siku 4, kwa kidaraja ambacho kilitakiwa kujengwa hata na fundi mchundo tu within 6 hrs lakini imeshindikana. Waziri wa Ujenzi yupo, Mkurugenzi wa Tanroads yupo, mameneja wapo, wahandisi wapo!

Ngoja nisiseme mengi lakini ukweli ni kwamba bila mikakati ya kisera Tanzania tutadumazana akili bure.

NOTE: Waliopo kwenye mfumo ni either wamedumazwa na mfumo ulivyo au mfumo uliwabeba kukalia nafasi za maamuzi pasi na uwezo.

........."Nothing will change".......
 
Ndio maana tumeshauri wabadilishe watumie bridge culvert.

Mfano mzuri ni jinsi estim alivyo jenga pale mbezi kibanda cha mkaa ambapo kukua na pipe culvert na miaka yote maji yaoikua yanapita juu na mara nyingine yanabomoa


Tatizo engineers wetu nadhani hawaoni mbele wanaangalia kumaliza kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengine wanapita humu wamekusoma na wamekuelewa!
 
Barabara ni issur ambayo ipo ndani ya uwezo wa engineers wa tanroad ndio maana wazuri mkuu kampiga chini manager wa tanroad mkoa.

1. Kwanza kwa uzembe wa kuto kagua eneo husika hadi culvert lina jaa mchanga na kuzuia maji kuto pita.

2. Pili kwa kuto mobilize nguvu ya kiufundi na kitaalam mapema ili kupata suluhu kwa wakati.

3. Kuto kua na kumbukumbu juu ya ukaguzi wa barabara.

Hili tanroad hawawezi likwepa.
Kwa dharura hii mie siwalaumu kabisa Tanroads,

Hizi huwa ni kazi za jeshi,iweje nao wasifanye jambo la kutukuka kama ilivyo ada kwao?

Mkuu wa majeshi unafeli wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu yawezekana una hoja. Ila hili unaloona kuwa daraja la Morogoro ambalo hadi waziri mkuu kafika, kwingine hali iko hivi:

Rusumo - Rusahunga njia kuu kwenda Dar taswira halisi ya awamu ya tano - ukweli mchungu

Barabara ya Rusahunga Benako: Imefunga tokea jana zaidi ya masaa 24 sasa

Kelele zimepigwa hadi tumekaa kimya. Maana kumpigia mbuzi gitaa ni shughuli pevu. Morogoro angalau manager tanroads kapata stahiki yake:

Meneja Tanroad arudishwa wizarani kwa kushindwa kukagua madaraja

Kwingine je?

IMG_20200229_191341.jpg

Hali ya Chatto ni tofauti sana. Barabara zote mjini takribani ni za lami inayoambatana na mitaro swafi. Barabara zote kuu kuingia na kutoka Chatto hapo usiseme (japo hakuna magari kihivyo) lakini barabara hizi ziko utadhani uko Marekani. Vivyo hivyo kwa traffic lights zao - classic:
 
Back
Top Bottom